CHANGAMOTO 10 ZA KUOA MWANAMKE ALIYEKUZIDI MIAKA MINGI

Jamii nyingi za kiafrika huamini kwamba siku zote mwanamke ni lazima awe na miaka michache kuliko mume wake.
Changamoto 10 za Mwanaume Kuoa Mwanamke Aliyemzidi Miaka Mingi:
i. Maneno maneno ya kuvunja moyo kutoka kwa jamii
Inapotokea mwanamke akawa na miaka mingi sana kuliko mumewe jamii huweza kuongea maneno ambayo wakati mwingine huwakosesha raha na amani. Unapogundua watu kila ukipita wanakusema wewe na kukusema kwenyewe ni kukusema vibaya sio kukusema kwa mema hilo jambo huumiza sana moyo wa mtu na kumfanya kuamini kwamba kila wakati watu watakuwa wakimsema yeye hata wakati ambapo watu watakuwa wakiongelea mambo mengine yeye atajihisi tu kuwa wanamsema yeye. Kadri miaka inavyozidi kwenda mmoja anaweza kuona vibaya kuongozana na mwenzake kutokana na hayo maneno ya watu wa nje kwamba hawaendani na kwamba ameoa mwanamke mzee au ameolewa na mwanaume mzee au wengine kumshambulia mwanamke kuwa ameolewa na mwanaume mdogo au mtoto hali hii huchangia kupunguza uhuru wa kimahusiano kati ya wanandoa hawa hasa mbele za jamii. Baadhi ya watu katika jamii wanaweza kuongea juu yao mambo ambayo yatawaumiza sana mioyo yao.
ii. Kukosa Uhuru wa kuwa na Mwenzi wako Hadharani.
Kutokana na maneno ya watu mitaani, kanisani, kazini na kwingineko mnaweza kukosa uhuru wa kuongazana pamoja au kumtambulisha kwa marafiki au inapotokea mmealikwa kwenye sherehe au hafla fulani unapata utata wa kuongozana kutokana na kuhofia kunyooshewa vidole na watu kwa kuwasema vibaya.
iii. Kupishana kwa mapendeleo na maslahi “Hobbies & Interests” Baina ya Wanandoa Hao
Moja ya changamoto inayowakabiri wanandoa ambao wamepishana umri wa miaka mingi ni kwamba mmoja atakuwa anaishi kwenye ulimwengu wa kiujana na mwingine atakuwa anaishi kwenye ulimwengu wa Kiutuuzima au ulimwengu wa uzee. Tatizo litakalotokea hapa kila mmoja anajaribu kumvuta mwenzake kwenye ulimwengu wake. Yule ambaye ni kijana atakuwa anajaribu kumvuta yule mtu mzima au mzee kwake kwa maana kwamba yeye kama kijana hataki kufanya mambo ya kizee anataka kwenda na wakati kwa kufanya mambo ya kiujana ujana. Wakati naye yule mzee atakuwa akimvuta kijana kwake kwamaana kwamba yeye kama mtu mzima au mzee hawezi kufanya mambo ya kitoto kwani hata watu wakisikia anafanya hivyo wataweza kumuuliza kwamba wewe mtu mzima bado unafanya mambo ya vijana!? Kwahiyo kutakuwa na vuta nikuvute ambayo itasababisha mmoja kuona kwamba huyu mtu naona haikuwa chaguo sahihi maana ananitesa badala ya kunifanya nifurahie maisha ya ndoa.
iv. Changamoto ya Kutoendana na Kuangalia Nje ya “Fance”
Kadri miaka itakavyozidi kwenda ile “gap” ya umri itakuwa ikijitokeza kwa ukubwa zaidi. Kijana ataanza kuona huyu mzee hatuendani namimi yupo nyuma ya wakati na kuanza kuvutiwa zaidi na mtu mwingine wa rika lake. Mfano kama kijana ameoa mwanamke ambaye wamepishana sana umri, kijana anaweza kutamani mkewe awe anavaa yale mavazi ya ujana ambayo huvaliwa na wasichana mitindo na mishono ya kiujana ili atakapokutana na marafiki zake waone kuwa ana mwanamke ambaye anakwenda na wakati. Kwa upande wake huyo mwanamke kulinganana umri wake hawezi kuthubutu kuvaa mavazi ya kiujana kama hayo na hapo mgogoro huweza kutokea na wote wawili kuona kuwa hawaendani kabisa.
v. Imani ya kwamba Ndoa ni Kwajili ya Kupata Watoto
Katika tamaduni na mazingira yetu ya Kiafrika, umri wa mwanamke anapoolewa ni wamsingi sana hasa linapokuja swala la kuzaa watoto. Kwa tamaduni za kiafrika swala la kuzaa watoto katika ndoa ni jambo la msingi sana kwa jamii nyingi za kiafrika. Kwahiyo mwanaume anapooa anakuwa na mategemeo kwa sehemu kubwa kwamba atapata watoto kupitia mke ambaye anamuoa.
vi. Jamii Huamini kwamba Mwanamke Mwenye Umri Mkubwa Atashindwa Kuzaa.
Jamii nyingi huamini kwamba kuoa mwanamke mwenye umri mkubwa anaweza kushindwa kumzalia watoto mumewe.
Kulingaana na watafiti wanasema kwamba kadri mwanamke anavyoziku kuongezeka umri ndivyo ambavyo viungo vyake vya uzazi hupoteza uwezo wake wa kushika mimba na kuzaa watoto.
vii. Kiwango Muafaka cha Kupishana Umri Kati ya Mwanamke na Mwanaume.
Kwa Mwanaume:
Inashauriwa kwamba kwa mwanaume miaka 5 hadi 10 inafaa kupishana kati ya mwanaume na mwanamke anayetarajia kumuoa. Kwamaana ya kwamba mwanaume anaweza kuoa mwanamke ambaye yeye mwanaume anakuwa amemzidi huyo mwanamke miaka miwili, mitano hadi 10.
Kwa Mwanamke:
viii. Inashauriwa pia kwa mwanamke kuzidi miaka miwili hadi 5 kwa mwanaume anayetarajia kuolewa naye. Hii inamaanisha kwamba mwanamke akimzidi mchumba wake au mume wake miaka miwili hadi mitano itakuwa ni sawa hakutakuwa na tofauti kubwa sana wala madhara makubwa.
ix. Kuna Athari kwa wanandoa wakipishaza zaidi ya miaka 10.
Wanandoa wanapokuwa wamepishana kwa zaidi ya miaka 10 kunakuwa na utafauti mkubwa katika kuhusiana kwao kama jinsi tulivyoelezea hapo juu.
x. Ushauri kwa Wachumba Waliopishana Umri Mkubwa
Wachumba ambao wana tofauti kubwa ya umri wao, wanashauriwa kutafuta ushauri kwa washauri wazuri (good counselors) kabla ya kuoana.


No comments: