HATUA ZA KUJUA PENZI LINAPOTEZA UELEKEO















1. MAWASILIANO KUWA DUNI

Mapenzi na sawa na jani la mti. Huendelea kuwa na mawasiliano na shina kwa kusaidiana na matawi. Ila siku ikifika jani linadondoka. Hii utokea pale jani linapochoka na maisha ya kujishikiza. Haya ndiyo sawa yalio kwetu binadamu. Mwanzo uanza kwa kasi zaidi na mwisho hufifia kwa mawasiliano. Mtu anaweza kukata mawasiliano kwa sababu zake binafsi zikiwemo hizo za hapo juu.
Kama mawasiliano yalikuwa ni mara tano kwa siku (kwa wale walio mbali, mfano masomoni.), basi mawasiliano yanaaza kushuka hadi mara mbili hadi mwisho wa siku mawasiliano kukaka kabisa. Hapa kila mmoja akiulizwa swali kwanini husema nilibanwa na kazi ndio maana sikuweza kukutafuta.
Kwa walio kwenye ndoa mawasiliano pia yanakuwa nyuma kidogo. Kama alikuwa anakusalimia kwa kukumbatiana, hapa hali hua tofauti kabisa. Muda mwingine kila mtu na kazi yake. Kila mtu shuka yake, na kukicha kila mtu kivyake.
Hii hua na athari sana pale mmoja wa wapenzi anapokuwa na mpenzi mwingine. Yule ambaye ulidhani umemchagua anakuja kuwa sumu kwako. Unapenda umwone yeye ataki. Unapenda umpe zawadi yeye ataki, unapenda kutoka naye out yeye ataki, na pale anaposema uwasiliane naye basi roho huweka pembeni. Utagundua kuwa kama analazimishwa aongee.
Ikifikia sehemu hii na kama ulimpenda kweli basi utaongeza jitihada za kutaka kuwa naye, wasio na imani hufikia mahali wanasema nitaendelea kukaa bila kuoa. Kauli hii ni udanganyifu tu. Akisahau yale yaliyomtokea, anaamua kusaka mke au mume mwingine. Unapoona hali hii imeanza jalibu kuwajilazimisha kuwa karibu yake sana. Na pale unavyoona hali ni mbaya zaidi basi mweleze rafiki yake wa karibu ambaye humwamini kwa kila jambo.
Au unaweza kumweleza mtu anayeheshimika ili asikilize kilio chako na mwisho wa siku utaona mafanikio. Hii ni kwa wachumba na hata kwa wanandoa itapotakiwa kufanya hili.
Kwa wanandoa ni muhimu wawaone pia wezee wa busara ambao wanaaminika na kukubalika na jamii. Ikishindikana basi waende katika ofisi ya kata au ustawi wa jamii kwa msaada zaidi.

2. USO HUONYESHA KUWA HAPENDI KUONGEA

Ni hali ya kawaida kuona mke au mme kuonyesha kuwa apendi kuongea na wewe. Sababu kubwa anayo moyoni na hataki kuisema. Uso mara nyingi unakuwa na asili ya mkunjo kwa wanawake. Na kwa wanaume sura inakuwa na asili na makunyanzi. Hapo ujue kuwa hali ni mbaya sana. Hapo hata ukimsesha anaona kama unajisumbua tuu. Na kama ataamua kusema ni kidogo tu na mwisho inaedelea kukaa kimwa.
Pia hata majibu yake uteyaelewa tu. Ni ya unyonge hivi, na sauti ya chini isiyo na mvuto au ushawishi kwa mwenzake. Pakifikia mahali kama hapa jalibu kumnunulia zawadi mzuri, kumkisi, kumwambia oooo mpenzi wangu….nakupenda sana…….leo umependeza namna hii….. Kweli mimi nimechagua mke mzuri au mme mzuri sana……kwani najivunia sanakukuona na kuwa na wewe muda wote.
Wakati mwingine unaweza kwenda kumsaidia kupika, kuosha vyombo na hata kumwambia mkaoge pamoja. Utaona jinsi anavyoanza kubadilika mpenzi wako. Hapa hakuna mchawi bali ni namna tabia yako ulivyomwonyesha. Hali hii haiwezi kwisha ghafla kama kimbunga bali huenda taratibu na mwisho wa siki hali inajirudia. Kwa hali ya kawaida uchukua kuanzia siku 21-22. Uendelea kumwambia maneno yenye baraka na busara bila ya kukata tama. Uwe na imanii ya hali ya juu kwani majibu utayokutana nayo si ya kawaida, lakini mwisho wa siku hali itarudi kuwa ya kawaida kabisa.

                                   3. HASIRA ZA MARA KWA MARA.

Hatua hii mpenzi wako huanza kuchukia kila jambo. Utende mema yeye kwake ni baya. Utajiongelesha ni kamaunamuongezea hasira. Hapa ndipo watu huwa wanafikia kuchukua hatua ya kujiua wenyewe kisa mpenzi wake amamsaliti. Mfano wa majibu utayokutana nayo ni kama haya:-
  1. mbona hivi mpenzi?
  2. mimi nifanyaje?
Wewe yanakuhusu nini?
Umepata hasara gani mimi kufanya hivi?
Fanya utakavyo?
Mimi ndo kila kitu?
  1. kwa nini yamefikia hapo?
  2. we ujui?
Hizi ni baadhi ya changamoto utazokutana nazo wakati wa maojiano yako na mpenzi wako. Usimpige kisa majibu ya mkato. Kama mwanaume hali ikizidi kuwa ni kelele tu, basi kaa kimya au ondoka na kwenda kufanya shughuli zingine. Utavyorudi atashindwa anzie wapi.
Kama ni upande wa mwanamke yanamtokea haya basi fanya hivi:- kaa kimya kwa muda, atakaa kimya mpenzi wako. Kasha usisite kumwandalia mmeo chakula cha kutosha na kizuri. Hata kama hali usichoke kuandaa. Mpe maneno matamu mkiwa kitandani na kujaribu kumgusagusa sehemu mbalimbali za mwili. Hapa mwanaume ujanja unaisha hapo.
Kama hizo njia zinachukuwa muda mrefu basi anza kwa kumuomba msamaha. Hata kumpigia magoti usione aibu. Piga huku ukionyeshwa kuwa hali hile upendezwi nayo. Ni ya bahati mbaya. Hakirudi katika hali ya kawaida na siku nyingi kupita anza kushusha makombola kwa njia ya utani kuwa pale mme wangu kosa lilikuwa lako. Kama muelewa ataweza kijirekebisha ipasavyo na mwisho wa siku mukarudi kama siku ya kwanza kuanza penzi lenu.


No comments: