JINSI YA KUJINASUA KWENYE MATESO YA MAPENZI

Kama ilivyo ada, hapa huwa tunazungumza yahu­suyo mahusiano. Tunazijadi­li kwa pamoja changamoto za mahusiano na kuzipatia majibu kwa pamoja. Kwenye ulimwengu huu wa sasa, matatizo kwenye masuala ya mahusiano yamekuwa mengi.
Usaliti umeshika hatamu, watu wana­fanya mambo bila aibu. Uaminifu umepungua hivyo kuwafanya wenza waingie kwenye mau­mivu ya mapenzi. Mtu anakuwa haridhiki, ana­kuwa na huyu huku bado anamtamani mwingine.
MAPENZI NI STAHA
Ndugu zangu, ni lazima tujifunze kwamba mapen­zi yanahitaji staha. Mapen­zi yanahitaji kujitambua na mtu kuridhika. Kuamua kwamba sasa nina uhusiano fulani basi hakuna sababu ya kuwa na mtu mwingine. Kila anayeaminiwa ana­paswa na yeye kutengeneza mazingira ya kuaminika.
Kutokana na watu wengi kutokuwa waaminifu au kuendekeza tamaa, tu­nashuhudia watu wengi wakijikuta wameingia kwenye maamuzi ambayo hawakuwahi kuyawaza. Mtu anampenda mpenzi wake lakini kutokana na vituko anavyofanyiwa, anashindwa kujizuia. Matokeo yake naye anasaliti.
TUJIFUNZE KIDOGO KWA MFANO
Rafiki mmoja aliyejitam­bulisha kwa jina la Mary, alinitumia ujumbe mfupi kunieleza kuwa anateseka sana kwenye uhusiano wake ambao hauna hata muda
ili kweli aweze kuwa mwenza wako wa maisha. Tumia kila mbinu kumbadil­isha kama kweli unampenda, usiwe mwepesi wa kukata tamaa. Jitahidi kumten­genezea mazingira ajione kwamba anachokifanya si sahihi na pengine anajid­halilisha. Ifike mahali aone kwamba anakukosea kufanya anayoyafanya bila wewe hata kutumia nguvu.
ANGALIZO
Ukiona umefanya hivyo kwa muda mrefu na makosa yamekuwa yakijirudia, anza kumuepuka taratibu. Hii ina­saidia wakati mwingine kum­fanya mtu ashtuke kwamba anapoteza mtu sahihi maishani mwake, akilibaini hilo atarudi na asipofanya hivyo basi wewe endelea na maisha yako.
Usikubali kuishi na mtu ambaye ana mambo mazito ambayo hayabadiliki. Mtu ambaye ni mhuni, malaya na ambaye hataki kubadilika kitabia haifai kudumu naye muda mrefu. Kweli muweke karibu, muele­keze taratibu lakini ukiona umefanya hivyo kwa muda mrefu na haelekei basi achana naye.


No comments: