MAMBO YA KUFANYA ILI KURUDIANA NA MPENZI MLIYEACHANA
Watu wengi wanaachana na wapenzi wao kwa sababu mbali mbali lakini unafanya Nini pale unapoachana naye halafu ukaja kugundua kuwa bado unampenda? Jibu ni rahisi ni kumrudisha tu kwa njia yoyote.
Watu hawajui kumrudisha mpenzi mlioachana ni jambo rahisi sana kwa njia chache tu nitakazokufundisha leo basi unaweza ukamrudisha mpenzi aliyekuacha au uliyeachana naye.
Fuata Njia hizi ili Kumrudisha Ex wako Kwenye maisha yako:
1. Kata Njia Zote Za Mawasiliano Naye
ILi kumrudisha mpenzi wako Kwanza anatakiwa ajue ni kwa kiasi gani anakumiss na njia pekee ya kufanya hivyo ni kukata mawasiliano naye hii itasaidia kumpa muda wa kufikiria ni umuhimu gani unao Kwenye maisha yake.
2. Jaribu Kuwa Bize na Mambo Yako
Muda wowote Mahusiano yakiisha kila mmoja anataka kujua ex wake anafanya nini na kama anaendelea na maisha hivyo ni muhimu kujikita katika mambo yako binafsi hii itakukosesha muda wa kuanza kumuwaza na kumtafuta Ex wako na endapo ataona unafanya mambo yako ya maendelo basi atavutiwa zaidi.
3. Muonyeshe Anachokikosa Kutoka kwako
Kama unataka kumrudisha Ex wako jaribu kumkumbusha sababu za kukupenda Mwanzoni ni muhimu kujua sababu za kuachana na kutumia zile sababu kujiboresha zaidi na kujionyesha kuwa umekuwa na kubadilika na kuwa endapo atakupa nafasi basi utakuwa tayari.
No comments: