MPENZI AKIDANGANYA KATIKA MAHUSIANO CHUKUA HATUA ZIFUATAZO
–Uhusiano wa kimapenzi huwa na changamoto nyingi. Baadhi ya nyakati, wachumba hufurahia pamoja na baadhi ya nyakati hujawa na huzuni
Lakini ikiwa uhusiano utasambaratishwa kutokana na kudanganya, usijitie kitanzi, unaweza kushinda yote.
Kwanza kabisa, lazima ujue kusoma ishara
Ulikuwa wakati wako wa kupata mafunzo ambapo siku za usoni utaweza kuepuka hali kama hiyo yenye kuvunja moyo.
Usijifanye kuwa hakuna chochote kilichotokea
Uchungu hauwezi kuisha ghafla na unaweza kufanya jaribio la kuibua uhusiano wenu tena. Lakini huwezi kufunika macho na kujifanya hakuna chochote kilichotokea kwa sababu ni rahisi kwa hali kama hiyo kujirudia.
Unafaa kujipa motisha
Udanganifu huletea muathiriwa uchungu mwingi, iwe ulikuwa uhusiano wa miezi michache au miaka. Lakini huo huwa wakati wako wa kujikusanya na kupata nguvu mpya.
Usitarajie usaidizi wowote kutoka kwa mpenzi wako wa zamani
Mpenzi wako alikuvunja moyo, hivyo usimtegemee hata kamwe kwa sababu alikataa kulinda uhusiano wenu. Nje ya uhusiano, usimtarajie awe na manufaa yoyote kwako
No comments: