SIFA KUU 5 ZA MWANAMKE AMBAZO MWANAUME ANATARAJIA KUZIONA







1. Mwanamke anapaswa kuwa na maisha yake na sio maisha ya kuiga. Wapo wanawake ambao hupenda kuiga kile kinachofanywa na wanawake wenzake na kudhani hivyo ndivyo anavyopaswa kuwa. mwanamke mwenye tabia hiyo huwa hana mvuto kwa mwanaume kwani atakuwa ni mwana mke fake.
2. Mwanamke anapaswa kuwa mtiifu na mwenye heshima na pia mwenye busara. Mwanamke hapaswi kuwa na kiburi na kutaka kuota mapembe ndani ya mahusiano. Heshima na utiifu haimaanishi kuwa tayari kunyanyaswa, hapana. Mwanamke anapaswa ampe mpenzi wake ama mumewe heshima inayotakiwa kama kichwa cha mahusiano yenu.
3. Mwanamke anapaswa kuwa na uwezo wa kujitegemea. Hapa utata kidogo, wapo wale wanaoamini kuwa mwanamke anapaswa kutegemea kila kitu toka kwa mwenza wake. lakini ukweli ni kwamba wanaume wengi wanapenda kuwa na uhusiano na mwanamke ambaye anaweza kusimama kwa miguu yake na kujitegemea pia.
4.Mwanamke lazima awe anajiamini. Naam, hapa haimaanishi kuwa anatakiwa kuwa kiburi na mbishi, hapana. Isipokuwa mwanamke anapaswa aonyeshe kujiamini kwa kile anacosema na anachotenda. Kujiamini kunamfanya mwanaume ajue kuwa ana mpenzi ama mke ambaye anaweza kukabiliana na mikwaruzo mbalimbali inayohitaji hoja na utetezi.
5. Mwisho, mwanamke anapaswa kuwa na mvuto. Hapa haimaanishi kuwa mrembo saaaana, hapana. Ina maana kuwa mwanamke anapaswa kuwa nadhifu kila wakati ili kumfanya mwanaume apende kuwa nawe na avutiwe kuwa nawe wakati wote.
Sifa hizi tano akiwa nazo mwanamke, basi atambue fika kuwa Mwanaume atavutiwa nawe na uhusiano wenu unaweza kudumu na kudumu na kudumu. Unaweza kuongeza sifa nyingine hapa chini.


No comments: