ZIJUE DALILI ZA MWENZA ANAYECHEPUKA

Kila mmoja atakubaliana na mimi kwamba kuwa na mahusiano baina ya watu  hawa wawili  hukusudia kuwa na upendo  ,kujaliana , kuthaminiana , kuvumiliana na kuwa na urafiki wa hali ya juu . Lakini kutokana na hali kuwa mbaya  kwa sasa mahusiano ya walio wengi huenda tofauti na m,akusudio  ya kuanzisha uhusiano huo,Watu wengi  wameumizwa na wapenzi wao kwasababu ya kutokuwepo kwa uaminifu  katika mahusiano yao .
Ninaposema kutokuwa mwaminifu hapa namaanisha hali ya mpenzi mmoja kuwa na mahusiano yasio rasmi  ya nnje na mpenzi au wapenzi wengine  pembeni kwa lugha ya kizazi cha sasa “michepuko”.
Jambo hili mara nyingi hufanywa kwa siri sana na mwenza huyo tena kwa kuogopa sana ili asije akaharibu mahusiano aliyonayo kwa kipindi hicho  n wapo baadhi ya wapenzi ambao waliachana  na penzi kufa kabisa  baada ya siri hiyo kugundulika  na wengine kuamua kujiua kabisa  ili asishuhudie  akiendelea kuumia nafsi.
Pia wapo ambao wameweza kuhimili machungu baada ya kugundua  wapenzi wao kutokuwa waaaminifu  lakini wapo ambao uvumilivu uliwashinda na kuamua kubaki binafsi au”single” pia wapo ambao hali hii imewaletea shida kabisa na kupelekea kupata shida za kisaikolojia  ,kihisia na hata kiafya .
Na kwa bahati mbaya wengi wetu hatuzijui hata dalili zozote zinazoonyesha   mabadilikowalionayo wapenzi  wetu ili basi wanapokuwa na tofauti basi tuanze kuzichunguza kabla mambo hayajafika pabaya.
Kutokana na uchunguzi nilioufanya kwa  njia ya majadiliano na marafiki zangu ambao wapo kwenye mahusiano na pengine wamepitia baadhi ya dalili hizo au zote  na pia kwa kusoma vitabu mbalimbali  pamoja na mitandao ya kijamii , asilimia 80 ya watu walio kwenye mahusiano si waaminifu na wenza wao wamekuwa hawayajui  mabadiliko yanayoonyesha   mtu au mpenzi anayechepuka .
Hivyo hizi ni baadhi  ya dalili zinazoonyesha mtu  anayechepuka
Kwa kawaida  mtu unapomzoea  mara kwa marakuwa anawahi kurudi Hapa ningependa uelewe sio  kwamba kila mtu anapochelewa  kutoka kazini bas anachepukaa au sio mwaminifu , lakini zaidi ya asilimia 80   ya ambao wamekuwa na mahusiano ya nnje ,  kunakuwepo na hali  ya kuwa na visingizio vya mara kwa mara  vinavyohusiana na kazi ,mikutano , na safari za kikazi yamkini ww ni mmoja wa shuhuda la hili.
Unaweza kukuta mtu alikuwa anafanya kazi  hiyo muda mrefu au  tangia muanze mahusiano lakini ghafula  hali inabadilika , siku hizi anakuwa mtu wa kuchelewa sana kurudi nyumbani na anaporudi unaweza kutegemea akirudi utamwona amechoka kimwili na hata kiakili kwa  majukumu ya kikazi kuhusiana na kazi anayoifanya  lakini utakuta mtu wala haonyeshi haaali   ya kuchoka na ana furaha kama kawaida, Hali hii inapojitokeza mara kwa mara usichelewe kuwa macho  na kudadis I mazingira maana yamkiniipo kazi ya ziada anayoifanya ila sio ile ya ajira unayojua wewe .
Kuwa mkali sana unapoishika simu yake
Yamkini katika mapenzi yenu mwanzoni ulizoea kuwa huru kuishika simu yake kwa wakati unaopenda na yeye anashika simu yako kwa wakati wowote  lakini inafika kipindi ghafla unapotaka kuishika tu simu yake utasikia sitaki uishike simu yangu  mana kila mtu anasimu yake pengine anadiliki kukuambia hata ukiona mtu anapiga sipo uiache hivyohivyo hata usiipokee  , wakati mwengine anaweka neno siri “password” ili usiweze kuifungua na kuitumia, wakati hapo mwanzo alikuwa anakupa namba za siri  kila anapobadilisha
Utakuta mda mwengine  anadiliki hata kuingia nayo bafuni wakati wa kuoga  na utashangaa mda mwengine hata ikiita mbele yako baadhi ya namba hapokei akiwa na wewe au anaenda  kuongelea  pembeni. tena akiwa katika hali ya wasiwasi utamuelewatu mana atakuwa katika haliya wasiwasi , ukiona dalili kama hizi basi anza kuwa macho na kufanya uchunguzi kwa nini mazaingira yamebadilika gafla , unaweza ukagundua  nini kinachoendelea.
 Kuwa na hali ya kujipenda kwa kupita kiasi
Inawezekana mpenzi wako alikuwa amezoea kuvaa mavazi ya kwaida, hapa simaanishi kutopendeza laa, na wewe ulikuwa umemzoea  katika hali Fulani ya mavazi na mitindo lakini ghafla  anabadilika nakuwa mtanashati Zaidi  anabadilisha mavazi , anapenda mavazi ya gharama na  nap engine alikuwa hatumii manukato yoyopte au ya kawaida sana mara anakuwa anapenda manukato tena ya gharama  .
Na pia anakuwa mtu anayejijali Zaidi kuliko kawaida yake  na ulivyomzoea  , katika hali kama hii hembu jaribu kuchunguza kwa  ukaribu ili ugundue nini kinachosababisha mabadiliko ya ghafla   kiasi hicho
Kupenda kutembea na mipira ya kinga “condoms”
Huwa inashamgaza sana mara nyengine  mpenzi mmoja kati yenu kuwa na tabia ya kupenda kutembea na mipira ya kinga  au kondomu kwa pochi au mfuko wake  kwa kusingizia kuwa anatimiza wajibu wa kujali afya zenu  cha kushangaza zaid unakuta yuko kwenye mahusiano ya ndoa  nikimaanisha mke na mume yamkinni kuwa anakujali  hilo sio jambo la kustua wakati mwengine imahitajika kutumia kinga ili kulinda afya zenu au kwa sabamu nyengine Zaidi
Lakini inakuwaje pale unapogundua kuwa ile kondomu uliyokuwa unaiona au uliiona ghafla haipo tena na yamkini wewe haukuhusika katika kuitumia    . ukiona hali kama hii chukua hatua ya kuchunguza kwanini kunakuwa na jambo kama hilo kati yenu.
Kutokuwa na hamu ya kuona uwepo wako
Katika jambo kama hili mara nyingi watu  wanapo anza mahusiano kunakuwa na hali ya kujaliana na kutamani kuwa karibu muda wote lakini kutokana na majukumu ya kujenga taifa katika shughuli mbalmbali kuna kuwa na nafasi chache za wapendanao  kuwa karibu lakini ukaribu wao wanaweza wakafanya hata kwa njia ya mawasiliano ya simu ya mara kwa mara  na kujitahidi kutafuta  nafasi ya kuwa karibu japo mara moja kwa wiki  hasa kwa wale ambao sio wanandoa yani ambao hawaishi pamoja  na kwa wale wanaoshi pamoja unakuta  wanaporudi  kutoka kazini  wakati wote wanafurahiana na  kupenda kushirikiana mambo yao kwa pamoja yanayohusu mapenzi yao likiwemo tendo la ndoa ,.
Uliizoea kuwa  mnaonana mara kwa mara saa nyengine mara tatu hadi nne kwa wiki kama akiwa hayupo na wewe utakuta anakutafuta kwenye simu mara kwa mara  hata kwa message lakini gafla  kila unapohitaji ukaribu wake  atakwambia yuko bize sana na kazi hivyo hatapata nafasi hadi siku za wikiendi au kukosa kabisa kwa wiki nzima mara anapunguza mawasiliano ya simu na wewe mara kwa mara  au akupigii kabisa hata siku tatu na utakuta kama ni wanandoa  mnaishi pamoja  akirudi hafurahi kama zamani anakuwa kama ni mtu mwenye stress au mawazo mda wote  na anapunguza kukushirikisha  mambo mengi wakati mwengine kama humuonyeshi hali ya kumuhitaji kimwili inaweza kupita hata mwezi au miezi miwili  hajisikii kabisa kukutana kimwili  na wewe na ni mzima kabisa ukiona hali hii anza kuchukua hatua .


No comments: