JINSI YA KUMTONGOZA MWANAMKE KWA NJIA YA KIRAFIKI

1. Kuwa mwanaume bora
Katika dunia tunayoiishi sahizi kila mwanaume anatamani kuwa na mwanamke bora zaidi. Hivyo kutaka kuwa na mwanamke unayempenda lazima uwe bora kuliko wengine. Hii ni kuanzia tabia zako, vile unavyohusiana na wengine, miondoko yako, unadhifu wako nk. Kuwa mwanaume bora hakuna njia ya mkato. Lazima ufuate mkondo ambao wengi hawaufahamu.
2. Tafuta muda wa kuwa nyinyi peke yenu
Kumsuka mwanamke huwa ni bora zaidi wakati ambapo mko nyinyi wawili pekeenu. Kumsuka mwanamke mbele ya marafiki zako kutamfanya kukuona wewe hauko serious na mambo unayotamka hivyo ni bora wakati ambapo unachukua muda na kuwa na yeye pekeenu mnaongea.
Unaweza kumsuka kwa kutumia mizaha wakati ambapo mko na marafiki zenu. Lakini wakati ambapo mko nyinyi wawili, tumia maneno ambayo hatayasahau kiurahisi. Mfano unaweza kumwambia “wewe ndie unafanya siku yangu kuwa ya shangwe”, “kukaa na wewe hapa najiskia niko huru” nk kutamfanya yeye kujiona spesho kwako.
Ujanja hapa ni kutumia maneno ambayo yatamfanya yeye kujiona spesho kuliko yeyote na amini usiamini mwanamke kama huyu atakuwa akifikiria mazungumzo yenu kwa muda mrefu.
3. Wanawake wanapenda ucheshi
Hivi wewe ni mcheshi? Kama jibu lako ni la basi usiendelee kusoma zaidi ya hapa mpaka uifahamu sanaa ya ucheshi.
Nadhani unafahamu ya kuwa njia ya kumvutia mwanamke lazima utumie lugha ya ucheshi mara kwa mara. Well, uzuri ni kuwa si lazima uwe na ustadi wa kuchekesha. Unaweza kuelezea matukio yako ya awali ambayo uliona yalikuchekesha. Kama mwanamke anaonyesha dalili za kukupenda, basi kila neno utakalolitoa kiutani atacheka.
4. Msumbue mara kwa mara
Wakati mwingine kumsuka mwanamke kunaweza kuonekana kuwa ni kazi ngumu, lakini kitu muhimu ni yale mambo madogo madogo ambayo mnafanya. Kumsuka mwanamke si kutumia maneno matamu ya kimapenzi pekee bali pia zile tabia ambazo mnafanya wakati mnapokuwa mnaongea. Hii ni kuanzia kucheka hadi migusano yenu ya mara kwa mara.
5. Cheza na mazungumzo machafu
Hatua tano za awali ambazo tumezitaja ni za kujenga mazingira ambayo yanawaweka katika hali ya kuleta nafasi ya kusukana kiurafiki.
Wakati ambapo utachagua kuvuka hii hatua, nyote wawili mtakuwa mumeingia hatua ya kuanza kutongozana.
Wakati ambapo umepata nafasi ya faragha ama unapompigia simu, jifunze kuchanganya maneno yako. Kufikia sasa najua nyote wawili kuna tenshen flani ambayo itakuwa imejijenga kati yenu hivyo usiingiwe na wasiwasi kama utajaribu kuingiza maneno ambayo yamevuka mipaka. Mara moja au nyingine unaweza kuingiza maneno ya kimapenzi katika mazungumzo yenu. Hata kama atakwambia uachane na hayo maneno utakuwa umechukua hatua kubwa kuonyesha hisia zako kwake.
6. Muombe mtoke out mara kwa mara
Mara moja wakati wa maongezi yenu unaweza kumuomba umtoe mwende mkahawani ama kumpeleka katika sinema siku ya pili. Wakati mzuri wa kumwambia haya ni wakati ambapo mmemaliza maongezi yenu ama wakati mnapokuwa mnatext. Kumuuliza hivi si lazima uonekane uko serious na vile unavyosema. Kumaliza maongezi yenu kwa ghafla kutamwacha mwanamke kama huyu kujiuliza maswali iwapo ulikuwa uko serious wakati wa kumwambia wataka mtoke out ama ilikuwa tu mizaha.
7. Zile simu za usiku wa kiza
Usiku huwa na mbinu ya kufurahisha kuamsha hisia zetu za mapenzi.
Marafiki wowote wawili ambao wanaongea kwa muda mrefu nyakati hizi za kiza mara nyingi hufikia hatua hii. Kama wataka kujua jinsi ya kutongoza mwanamke ili akupende chukua nafasi ya kumpigia simu ama kumtext nyakati kama hizi. Hakikisha ya kuwa unamrushia maneno ya kumtongoza.
Wakati huu wa usiku ambao umetulia ukiwa unaendelea na maongezi yenu ni rahisi sana kwenu kuivuka mipaka ya kuwa marafiki na kuanza kuonyeshana hisia zenu za mapenzi.
8. Mwonyeshe kuwa wewe unaweza kuwa mwenza mzuri wa kudeti
Ok kufikia sasa utakuwa umeshamwonyesha hisia zako zote, umemvutia na kujenga kemia za kimapenzi kati yenu, lakini utakuwa bado hujafunga mchezo. Atakuwa labda amependezwa na maongezi yenu na pia kukupenda kisiri, lakini kumfanya mwanamke akuone wewe kama una nafasi nzuri ya kuwa mwenza wake lazima uonyeshe dalili.


No comments: