JINSI YA KUWAVUTIA WANAWAKE BILA KUTAMKA NENO

Ushawahi kujikuta katika hali ambayo unashindwa kujua utaanza vipi kuongea na mwanamke? Ni mwanamke mzuri ambaye moyo wako unamtamani lakini akili yako inashindwa kutengeneza mawazo ya jinsi utakavyoanzisha stori na yeye. Unabakiwa ukimuangalia akikupita mbele yako, ama mbaya zaidi anakuja kuchukuliwa na wanaume wasiokuwa na thamani yeyote kwa maisha yake. Unabakia na majutio na mawazo ya "kama ningeweza kujiamini mbeleni si ningem...." Well, tatizo hilo halijawahi kutokea kwako pekee bali kwa kila mwanaume wakati flani katika maisha yake na hatutaki lijitokeze tena mbeleni. 

Related image

So chanzo cha wewe kutoweza kumtongoza huyu mwanamke ni kuwa akili yako ilikataa kutoa mazungumzo ambayo ungeweza kuyatumia kwa huyo mwanamke. Well, waonaje kwa mara moja tukubaliane na akili yako na tusitumie maongezi kuapproach mwanamke, na badala yake tutongoze kimya kimya?

Kutongoza kimya kimya ni mbinu rahisi sana, mwanzo ni rahisi kwa kuwa unapata kujua kama mwanamke anakupenda au la. So bila kupoteza wakati, hebu tuchambue mpango mzima.

Zama nami!

1. Kwa kutumia macho
Kila mtu anajua nishati inayotokana na kutumia macho. Macho ni kiungo ambacho wanaume wamebarikiwa nacho na akikitumia vizuri kinajeuka kama silaha nzito wakati ambapo unaitumia kwa mwanamke. Ushawahi kujiuliza ni kwa nini wakati mwingine mwanamke anashikwa na aibu/haya wakati unapomwangalia? Ama je ushawahi kumskia mwanamke akisema kuwa usimwangalie machoni mwake? Hii ni kwa sababu macho yanaweza kutumika kuongea maneno ambayo mdomo unaweza kushindwa kuongea.


Wakati utajipata ukimwangalia mwanamke, mwangalie machoni halafu utoe tabasamu. Kumuangalia kunaonyesha unajiamini. Kutabasamu unamwonyesha kuwa wewe ni salama na anaweza kuongea na wewe. Unaweza kusoma chapisho letu la awali ambalo linafafanua mbinu ya kutumia macho kuapproach mwanamke kwa kina.
2. Mfanye akugundue kupitia kutangamana kwako
Njia nzuri ya kusimama ili wanawake waweze kukutambua ni kupitia utangamano wako na wengine. Kujizunguka na wanawake wengi (haswa wale warembo) kutaashiria ya kuwa wewe ni aina ya mwanaume ambaye wanawake wanapenda kuwa naye. Hii itawafanya wanawake wengine katika hio sehemu kuwa na shauku ya kutaka kujua ni kitu gani ambacho kinakufanya wanawake wapende kuwa na wewe. Hii automatically itawafanya wanawake kuwa na umbea kukuhusu, kuvutiwa kwako, na hata kuingiwa na wivu wa kwa nini haujawaingiza katika kundi lako. 

Mbinu hii ni moja wapo ya sosholojia ya wanawake, kimaumbile wanawake hupenda vitu ambavyo wanawake wengine hupenda. Hivyo kama wewe unamtaka mwanamke flani na hutaki kutumia maongezi, anza kutangamana na marafiki wake wote isipokuwa yeye, mwishowe utamwona akijileta yeye mwenyewe, tena ujitayarishe na mapema kwa kuwa atakuja na presha ambayo kama hukujipanga vizuri inaweza ikakulemea.

3. Matumizi ya banta bila kuongea
Banta ni mbinu ya kuonyesha ucheshi, mchezo na mzaha wakati wa kuongea na mtu. Mbinu hii pia inaweza kutimizwa bila kutumia mazungumzo ili umfanye mwanamke aweze kuvutiwa kwako.

Kwa mfano, kama ulishatumia mbinu ya macho kuwasiliana na mwanamke na unataka kuendeleza shughli kwa kutumia banta, njia rahisi ni kumuonyesha nyuso za ucheshi. Jifurahishe na uwe mcheshi - toa ulimi wako nje - pinda macho yako - weka uso wowote ule wa kipuzi ambao unajiskia. Hii ni njia rahisi ya kumfanya mwanamke atabasamu akiwa mbali, na itakuwa rahisi kwako kumuapproach na kuendea na yeye iwapo ataonyesha dalili za kupendezwa na wewe.

4. Mvutie na mwonekano wako
Ukitaka kumvutia mwanamke kiurahisi basi ni muhimu kubadilisha mwonekano wako. Mbinu hii tuliieleza kwa kina katika chapisho la jinsi ya kubadilisha mwonekano wako uwavutie wanawake. Kwa kawaida, wanawake wanapenda kushufu wanaume ambao wanavalia kinadhifu.

Lakini hapa usichukulie makosa. Kubadilisha mwonekano hakumaanishi ya kuwa unapaswa kuvalia nguo ghali ama za thamani ya juu. La hasha. Kubadilisha mwonekano kunamaanisha kuvalia nguo safi, nadhifu na ambazo zinaashiria hulka yako. Usijitese kuvalia nguo ambazo haziwiani na wewe kwani kwa mwanamke ni rahisi kukugundua kama umejeuka mwigo.

5. Ishara ya mwili wako 
Wanawake wanaweza kujua mengi kukuhusu kwa kuangalia miondoko yako ya mwili pekee. Kama unataka kuonyesha ujiaminifu ambao utamfanya mwanamke akutambue, basi ni lazima mwili wako uonekana vile unapaswa kuonekana.

Kuonyesha confidence katika mwili wako unapaswa kufanya yafuatayo:
i) Simama wima - mwanaume thabiti akisimama anakuwa hivi; masikio yako yawe nyuma ya mabega yako, mabega yako yawe nyuma ya kiuno chako, kiuno chako kiwe nyuma ya kiwiko chako.
ii) Kaa kwa kujitanua - wakati umekaa katika kiti, hakikisha ya kuwa unachukua nafasi yote ambayo unaweza kuitimia. Egemea kwa kiti, itanue miguu na mikono yako, kichwa kiweke kiangalie juu.
iii) Jinsi unavyokaa - Usisogee sogee kama huna sababu zozote, usikunje miguu wala mikono, usiangalie chini, usijikune kichwa ama kutafuna tafuna.
iv) Unavyotembea - Tembea na sababu, tembea kwa kujiamini, tembea na njia thabiti.

Kuweza kukontrol mwili wako inakusaidia kuonekana mtu mwenye nguvu, wa kujiamini ambaye anapendwa na wanawake.

6. Kuwa na hadhi ya juu
Mpaka sasa hili chapisho linaongea kuhusiana na kuwasiliana na mwanamke bila kuongea naye. So iwapo unataka mwanamke akunotice, wakati mwingine inahitajika kuwa na jitihada za ziada. Kukaa sehemu moja kungojea mwanamke akugundue haitakuwa ya fanaka kama vile ambavyo utaamka na kujifanya uonekane wewe mwenyewe.

So utafanyaje mpaka mwanamke akunotice? 

Tangamana na marafiki, jamiiana na kila mtu ambaye unamjua. Wakati umetoka matembezi au sehemu yako ya kujivinjari, ongea na kila mtu - wanaume, wanawake, wateja, wafanya kazi nk. Wanawake watauona uwezo wako wa kutangamana na kila mtu na watakuwa na interest ya kuongea na wewe. Ziada ni kuwa utakuwa unaonyesha ujiaminifu, urafiki, na uko na uwezo wa kujicontrol katika jamii - tabia zote ambazo wanawake wanaziona nzuri katika mwanaume. 


7. Wafanye wanawake wakufukuzie
Kufanya wanawake wakufukuzie inaweza kuwa rahisi sana.  Kile ambacho unahitajika ni kutoka nje umakinike na kujifurahisha muda wote. Weka tabasamu katika uso wako na ujiinjoy wewe mwenyewe. Hii itamfanya mwanamke kukunotice na kutamani kuungana na wewe ili muinjoy pamoja.


No comments: