MAMBO MAKUU 3 YATAKAYOWASAIDIA KUJENGA MAHUSIANO BORA YA MAPENZI

Ili muweze kudumu katika mahusiano yenu ya kimapenzi yapo mambo muhimu mnayopaswa kuyafahamu ili mahusiano yenu yazidi kushamiri kila wakati na mambo hayo ni pamoja na:
Jengeni Urafiki
Ili mapenzi yenu yadumu ni lazima muwe na ukaribu na urafiki. Ili mpenzi wako aweze kukwambia kitu chochote ni lazima mjenge ukaribu ilI muambiane kila kitu. Mkiweka mahusiano yenu katika mazingira haya kutawafanya muwe wawazi katika kushaurina mambo ya maana pia.
Kukiri kosa na kuomba radhi
Ili mapenzi yenu yadumu lazima mjue kuna kukosea na ni muhimu pale unapokosea umuombe mpenzi wako msamaha hii itawasidia kiheshimiana zaidi. Wote tunakosea hakuna binadamu mkamilifu hivo ni muhimu kujifunza kutoka kwenye makosa yetu.
Kuheshimiana
Hakuna kitu muhimu kwenye mapenzi  kama heshima ni muhimu kila mmoja amheshimu mwenzie hii itasaidia kuweka mipaka fulani katika mahusiano na hii itoke pande zote mbili mwanamke amheshimu mwanamke na mwanaume hivyo hivyo.


No comments: