MAMBO YANAYOCHANGIA KUPOTEZA HISIA ZA MAPENZI
Kwanza ni lazima uitosheleze akili yako, lakini pili, unapaswa kuamini kwamba uliyenaye ni bora na hata ikiwa kuna kasoro, jambo la msingi ni kuzungumza kuondoa tatizo hilo, siyo zaidi.
Anachanganya mambo, hatosheki
Ukweli ni kuwa wengi wa watu wanaodai hawatosheki katika mapenzi ni wale wanaoziachia akili zao zitake tendo la ndoa zaidi, bila kuangalia uwezo, nafasi, hisia na afya yao ya kukutana kimwili.
Lakini pia wengine ni kwa sababu wanavuta hisia za wapenzi wao wa zamani, ambao labda walikuwa wana uwezo mkubwa zaidi katika tendo hilo kuliko sasa.
Hata hivyo, wakati mwingine wanashindwa kuelewa kuwa hata wale wanaofikiri ni wazuri, kama wangekuwa nao hadi leo, huenda wasingeweza kuendelea kuwa imara.
Hii ni kwa sababu, watu wengi baada ya kukaa pamoja kwa muda mrefu hupoteza nguvu au shauku ya tendo hilo.
Zipo sababu nyingi za hali hiyo, mojawapo ni kutobadilika kwa mazingira au wapenzi kuanza kutoelewa kwa sababu mbalimbali kama vile kutojaliana na kadhalika.
Nguvu za kijinsia
Kama hukuwa unafahamu; ni kwamba, idadi ya wanaume wasiyo na uwezo wa kufanya vyema tendo la ndoa inazidi kuongezeka. Tafiti zinabainisha kuwa wastani wa ndoa nne kati ya 10 zenye umri wa miaka 3 na kuendelea zinakabiliwa na tatizo hilo.
Pia wanaume sita kati ya 10 wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume, kwamba kama siyo kuwa na uwezo mdogo, basi hukosa kabisa nguvu za kuendelea.
Wengine wanaweza kuanza, lakini hawawezi kuendelea au wengine hata kuanza ni shida.
Ingawa tiba yake ni ndogo, hasa mchanganyiko wa vyakula kama nilivyowahi kueleza mara kadhaa.Idadi kubwa ya wanaume bado wanasumbuliwa na tatizo hili, hasa kwa sababu ya kutokuwa tayari kuchukua hatua hasa za kuzingatia ushauri.
Ziko sababu nyingi za kukumbwa na hali hii, ikiwamo ulevi, kutofanya mazoezi, kujichua au utumiaji holela wa vyakula, hasa vyenye mafuta. Hata hivyo, kwa kuzingatia tiba sahihi ya vyakula bora, mtu anaweza kupona.
Kwa mfano kuna baadhi ya vyakula vikichanganywa kwa ustadi kama pilipili, parachichi na kadhalika vinaweza kumfanya mtu kuondokana na tatizo hilo.
Wapenzi wa siku nyingi
Wengi wa watu walio kwenye ndoa za miaka mingi, wanafanya mapenzi kwa sababu tu wamepata nafasi ya kuwa pamoja, lakini siyo kwa sababu ya kuwa na hisia kali.
Matokeo yake ni wanandoa wengi hupata msisimko mdogo katika tendo la ndoa wanapokuwa na wenzi wao. Hata hivyo, kwa kuzingatia utaalamu, wanaweza kuwa na furaha katika ndoa yao.
No comments: