SAUTI INA RAHA YAKE KATIKA MAPENZI
Sauti Siku Zote Ina Maana Kubwa Sana Katika Mtiririko Wa Wewe Kujua Mwenzako Ana Maanisha Nini.Sauti Vilevile Inaweza Kukupa Picha Jinsi Alivyo Kutegemeana Na Ongea Yake.Sauti Huwezesha Lugha Yako Unayoiwasilisha Kueleweka Vizuri Kwa Msikilizaji Endapo Utaitumia Ipasavyo.
Je wajua sauti ya mtu kwa harakaharaka inamtambulishaje kwa msikilizaji?
• Mpole
• Mkali
• Hekima na busara au
• Hasira
Linapokuja suala la mahusiano,ni vizuri uzingatie matumizi ya sauti kutegemeana na muda na hali Fulani ya maongezi.
Pale mnapokoseana, ni vizuri ukatumia sauti yako kumshusha mwingine ili muweze kufikia muafaka.Ukiendeleza sauti ya ukali hatakama haumaanishi kubishana, si rahisi kufikia muafaka sanasana mtaishilia kuchukizana zaidi.
Sauti hutumika katika kubembeleza ,yale mahadhi yakupanda na kushuka kwa sauti yako humjengea mtu hisia na ladha Fulani tofauti na unapokua katika maongezi ya kawaida au ya wewe na rafiki yako.
Unapokua na mpenzio hakikisha unatumia sauti yako ipasavyo katika kunakshi maongezi yenu na kuyafanya yawape furaha nakuwa na hamasa zaidi ya muendelezo wa mazungumzo au shughuli nyingine bila kuchoka.
Siimaanishi uige sauti ya Fulani,hapana.Bali kuwa mbunifu wa utumiaji wa sauti yako.
Kuwa miongoni ya wale ambao wanapendwa kusikilizwa na wapenzi wao,sio kwa ajili ya mapenzi ya dhati tu ,bali kwa jinsi wanavyoteka nafsi ya mwenziwe kwa matumizi mazuri ya sauti yanayoipamba lugha na maongezi kwa ujumla.
Nadhani ulishawahi sikia mtu anasifiwa kwa jinsi anavyoongea au umewahi kumsikia wewe binafsi na akakufanya uvutiwe na ile hali.Jua unavyopangilia sauti yako ipasavyo kutokana na mazingira na aina ya mazungumzo unapokua na mpenzi wako; unamvutia (draw attention) na ni rahisi kwa yeye kukusikiliza and act accordingly….Una maoni yako juu ya sauti?…tupia hapa
No comments: