WANAUME HII NI KWA AJILI YENU



1. Mwanamke si ruler iliyonyooka kwamba hakosei, bali anapokosea adhabu yake si ngumi bali ni mawaidha. 

2). Usihuzunike mkeo hapendezi au hanukii hali ya kuwa hujanunua nguo wala perfume ,wewe ndiye ulaumiwe. 

3). Usifichue udhaifu wa mkeo kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mkeo, naye ni mlinzi wako. 

4). Usimkataze mkeo kushika simu yako baada ya kuita kwa kuiwahi wewe kabla hajaona anayekupigia, unachokichukulia tahadhari kikigundulika ndoa yenu itapata mitikisiko. 

5). Usiogope kuchekwa kwa kumsaidia mkeo shughuli za ndani, mke si mtumwa isipokuwa ni msaada kwako. 

6). Usipendepende kusifu wanawake wengine mbele yake, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka. 

7). Usimgombeshe mkeo kwa kutoweza kupika vyakula unavyovipenda ,kwao hakukua na chuo cha upishi alipika kulingana na kinachopatikana, bora ni kumfundisha. 

8). Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia mkeo, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za mkeo ni jukumu lako mwenyewe. 

9). Hakuna mwanamke ambaye atamvumilia mwanaume dhaifu kitandani ,tumia kiwiliwili chako vizuri. 

10). Peracetamol na dicloper isiwe ndio tiba ya kila ugonjwa anaoumwa mkeo ,suala la kumtibu ni lako usilikwepe. 

11). Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na mkeo. 

12). Usimlinganishe mkeo na wanawake wa nje hao hawajui thamani yako ,ukiendelea na hilo mapenzi ndani yatapungua. 

13). Muheshimu mkeo hata kama wewe ndio mkuu wa familia kwani heshima ndio msingi wa ndoa yenu. 

14). Usiwe mume mwenye dhana potovu juu ya mke ,uwaminifu dhidi ya mkeo ndiyo chanda njema. 

15). Usimkosoe mkeo hadharani anapokosea ,hakuna anayekubali kukosolewa hadharani ,matoke ya hilo siku zote huwa hasi. 

17). Maamkizi mema yapambanishwe na kugusana miili yenu ,jambo hilo huondoa madoa yaliyo katika nafsi zenu. 

18). Neno "nakupenda" litawale kumwambia mkeo kwani mwanamke hufurahi kuambiwa neno hilo. 

19). Penda kumshirikisha mkeo katika mipango ya kimaendeleo, mwanamke ni mshauri mzuri. 

20). Watoto ni watoaji nje kila habari iliyo ndani kwenu, hivyo sehemu ya kumkosoa ni chumbami si mbele ya watoto.





















No comments: