Aina Mpya ya virus vya HIV yagunduliwa



Wanasayansi wamegundua aina mpya ya virusi vya HIV, kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2000.


Aina hii mpya ni sawa na ile iliyogunduliwa wakati wa janga la virusi hivyo mwaka 1981 katika eneo la Sub-Sahara barani Africa, na kusambaa kote ulimwenguni na ambayo imesababisha vifo vya watu milioni 32.

Aina hii iligunduliwa kwa watu watatu huko Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo na mwanasayansi katika maabara ya Abbott Labs, ambayo hufanya uchunguzi wa HIV.

Virusi hivyo ndivyo huambukiza zaidi binadamu.

 Wanasayansi wanasema kugundulika kwa aina hii ya virusi pamoja na aina zote zingine, huenda ikawa ni hatua muhimu katika kuelewa vinavyobadilika virusi hivyo, jinsi ya kuvitambua na kuvitibu na katika kusaidia kuundwa kwa chanjo ya kukomesha janga hilo kabisa.

https://ift.tt/2XonPVn

 Ugunduzi huu ni ncha tu, amesema daktari Mary Rodgers,mwanasayansi mkuu wa Abbott.

‘Abbott inatoa aina hii kwa watafiti kote ulimwenguni kutathmini athari zake kwa vipimo vya uchunguzi, matibabu na chanjo.’

Hii ni mara ya kwanza aina mpya ya virusi vya HIV imegunduliwa tangu  mwongozo wa aina za virusi hivyo ulipotolewa mwanzoni mwa karne hii.

Watafiti wanasema ugunduzi huu itawafanya kuwa na ufahamju iwapo virusi hivyo vitabadilika na hivyo kuzuia majanga mapya.

Photo Credits: Courtesy






No comments: