Hatupendi Kuwa na Historia Mbaya kuwa na Wanaume weng ila Inabidi



Mwanaume wa kwanza, nilikutana nae kidato cha tano lakini baada ya matokeo kidato cha sita aliniacha eti kwa sababu mimi nimefauru hivyo chuo lazima nitamsaliti nilimsihi sana kwa sababu niliamini,kuna maisha zaidi ya elimu but ugomvi kila siku nikaamua kuachana nae japo tulipendana sana.

Mwanaume wa pili huyu alinipenda sana lakini kumbe alikuwa na mtu mwingine before ambae ni rafiki yangu nae hakutambua kuwa mimi na yule dada ni marafiki. 

Lakin baada ya kungundua alinambia anamuacha coz ni kweli alinipenda nikamweleza mimi namuacha coz sipendi zaidi, aendelee na rafiki yangu na nilimuacha.

Mwaume wa tatu huyu nilianza nae nikiwa second year first semister, kijana ni mchaga jamani wachaga wanapenda asikwambie mtu nilienjoy aisee huyu kaka, kaka alipenda mpaka kasahau kusoma na course yake ni ngumu kisa kakolea mapenzini akadisco mwaka wa 3.

Kaenda kitaa na bado alinipenda zaidi kumbe huyu kaka nae ni yatima hivyo alikuwa anasomeshwa na mdada ili baadae waoane kaka kakutana na mimi kasahau fadhila za yule dada.

ATM ya mdada mimi niliishi nayo na kuchukua pesa nitakavyo bila kujua ni ya mwanamke jamani huruma. Kijana kafeli kaenda kwa mdada wake lakini bado anawasiliana na mimi.

Siku ya siku mdada kanitafuta analia vibaya mno jamaa kamwambia hampendi ananipenda mimi kwa kweli niliona machozi ya yule dada yananiletea mkosi, nilimwacha japo mpaka sasa ananipenda sikuweza kuendelea nae sitaki ni muongo.

Mwanaume wa 4, jamani huyu ni Dk hosipital 1 hapa Dar jamani, kaka sikujua ni mhuni kiasi hiki, ajabu alinipenda mpaka sikuweza kutambua tabia yake.
Kila akisema anataka kujitambulisha home moyo wangu ulisita sana, jamani nilimfumania, nikamwacha.

Sasa kumbe sikujua ameniweka moyon na alinitegemea kuwa mke now ninavyosema alichanganyikiwa mpaka alikosea kumtibu mgonjwa kamletea matatizo alisimamishwa kazi. Ila karudishwa now mimi sikumuhitaji sio mwaminifu angenisumbua sana.

Mwanaume wa tano huyu alikuwa anaishi Marekani kule alienda kimasomo ,kumbe tayari alikwisha oa ila waliachana na mkewe baada ya miaka 3 tena kaoa kwa taratibu za kikanisa, mimi sikujua kabisa, alinipenda sana but ukweli hawezi kuoa tena kwa taratibu za kikanisa ila mtaishi kama wazinifu tu,pia sikumumini sana.


Mwanaume wa sita, jamani before sijampata mwanaume huyu kwanza nilikaa miaka 3 single, nilimuomba mungu sana msamaha na kuvunja mikosi, sasa mimi nilibadilishwa na kuwa mwingine.

Tena roho mtakatifualizidi kukaa ndani yangu na hata sasa, nilipata mume na sasa nimeolewa, mume wangu nampenda na ana hofu ya mungu.

Ushauri, mume bora hutoka kwa mungu , na acha historia yako ya nyuma wala isikuumize wanaume waoaji wapo, tena ukiomba kwa kumaanisha

Pili usivunje amri ya sita wala usiruhusu kujuana na mwanaume kabla ya ndoa nimejifunza mengi sana.



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: