Inawezekana Una Ndoto Nyingi Unazoziota Kichwani ila ili Ufanikiwe Chagua Chache ndio Uamke Nazo






Katika harakati za kutafuta maisha huwaga watu wengi wanakuwa na ndoto nyingi sana ambazo wanaziota na wanatamani sana siku ndoto hizo zije kuwa kwelii.

Lakini uhalisia ni kwamba ukitaka kufanikiwa lazima uchague ndoto chache zenye mashiko ndio uamke nazo na zingine uziache zibaki kama ndoto tu.

Kwenye maisha ni rahisi sana kumuona mtu labda kafungua biashara flani kabla haijawa kubwa sana kafungua nyingine nayo kabla haijawa sawa anaongezea nyingine mwisho wa siku unakuta biashara zote zinakuwa za kawaida na zikifa zinakuja kufa zote na hapo ndio unajua kwamba mtu huyo ndoto zote alizoota alitaka zote ziwe kweli akasahau alitakiwa kuchagua chache mdio azipambanie.

Au katika maisha mengine unaweza kuta mtu mmoja anataka kuwa mwanamuziki hapo hapo anataka kuwa muigizaji hapo unagundua huenda alilaa akaota anafanya show moja kubwa sana akiwa kama mwanamuziki halafu akajikuta tena yuko hollywood anaigiza huko sasa kw haraka akataka kuzitimiza zote akasahau kwanza alitakiwa kuchagua kama anaamka kwanza na ndoto ya show kubwa au na kuigiza hollywood sasa bahati mbaya ndio unaweza shangaa ndoto zote hizo zinafeli.

Ukisimamia ndoto moja kwa nguvu zote ikasimama na ukafanikiwa vizuri inaweza kuwa rahisi hata kwa ndoto zingine kuziamsha na kuwa na uhalisia.

JIPANGE LEO NA CHAGUA NDOTO SAHIHI YA KUAMKA NAYO





No comments: