JE UNAFAHAMU FAIDA ZA KUWA KUTENGA MUDA WA KUWA KARIBU ZAIDI NA MPENZI WAKO.





Kuspend time na mpenzi wako mkiwa pamoja haitoshi kuyaelezea mapenzi yanu kuwa ni mazuri sana, bali kitakachoelezea uzuri wa mahusiano yenu ni misingi mliojengeana pamoja. Misingi ambayo ndio itaelezea uelekeo wa mahusiano yenu. Itaeleza uimara wa mahusiano yenu. Mbali na ninyi wawili kupendena na kutamani kuwa pamoja muda mwingi lakini ni lazima mkazingatia mambo yafutayo:-
KUJENGEANA UAMINIFU:
Hii itamsaidia mpenzi wako kukuamini hata kama uko mbali nae.. hatokuwa na shaka na wewe, hataangaika kutafuta ninani leo umezungumza nae, nani huyo aliyekupigia simu nk. Atakuwa na amani na penzi lake.
KUONEANA HURUMA
Kila mmoja wenu atakapoona jambo la mwenzake kama lake na kuonekana kujali hasa kipindi ambacho unapitia changamoto zako, bila kurudi nyuma akasimama na wewe hii itawasaidia kutengeneza bond ambayo ni vigumu kuvunjika.
KUWEKANA WAZI MAMBO AMBAYO KWA NAMNA MOJA AMA NYINGINE YANAINGIA KATIKA MAHUSIANO YENU.
Mwenzako anapotaka kujua jambo kutoka kwako ni vema ukamjibu kuliko kuanza kuona kama vile unasumbuliwa. Unapoanza kuona unasumbuliwa kwa sababu tu mwenzako ametaka kujua uwenda uko wapi au labda unafanya nini, ndio mwanzo wa kuanza kumuona mwenzako kama karaha, msumbufu, na kimsingi haitakiwi kumuona hivyo. kinachotakiwa ni wewe kumuelewa mpenzi wako nini anahitaji.
KUJENGANA KIIMANI.
Tafuteni muda wa kusali pamoja hata kama ni kupitia kwenye simu, hii itafanya kuachiana alama nzuri ndani ya mioyo yenu. Japo jambo hili linawashinda wengi lakini ni jambo ambalo linafanya connection yenu kuwa imara sana, anza kuanzia leo.
Kama mkiweza kuyafanya mambo haya kwa upendo, mapenzi yenu yatakuwa na muelekeo mzuri na wenye mguso, mguso ambao utakuwa unagusa mioyo yenu.


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: