KANUNI BORA ZA MAISHA ZISOME HAPA




👉Usitumie Nguvu Nyingi sana Wewe Kutafuta Umaarufu mbele za Wanadamu.

👉Usitumie Pesa,Uchawi,Nguvu nyingi Kutafuta Kujulikana mbele ya Wanadamu.

👉Wala Usitumie Nguvu nyingi Wewe Kutafuta Kutambulisha Huduma,Karama au Kipawa ambacho Mungu amekiweka Ndani yako.

✍Nakuambia Kwa kutumia Nguvu zako Mwenyewe Hakika Utaangaika na Kugharimu vitu vingi bila Mafanikio.
Unaweza Ukajitangaza Wewe Mwenyewe ukajulikana ndio,Lakini Kwako kukawa kwa Muda Mfupi sana.

Hivyo Ndugu yangu nikuambie

👉Mungu Anakujuwa Tangu ulipokuwa Katika Tumbo la Mama yako,Na hata kabla ya Kuzaliwa kwako Mungu alikujuwa na Kukutambua Vema sana,Hivyo Wewe Fanya Mausiano Mazuri na Mungu.
Baada ya wewe kuwa na Mausiano Mazuri na Mungu wako sasa Yeye ndiye:

👉Atakayekutambulisha mbele ya Wanadamu Na Kuitangaza Huduma,Karama au Kipawa alichokiweka Ndani yako kupitia Kazi yake Ndani yako.

✍Acha Mungu akutambulishe na Kukuinua kwa Wakati Wake Yeye,sio wewe Kujitangaza mwenyewe.
Wewe Kuwa Mnyenyekevu na Mtiifu Mbele zake Mungu tu.

Acha Acha kabisa Kutumia Hirizi mpendwa wangu, Nguvu za Mungu Ziko juu ya Nguvu zote.

👉Kaa Vizuri na Mungu.
Utakaa Vizuri na Mungu kwa ▶Kujitenga Mbali na Dhambi.
▶ Kuishi Katika Neno lake.
▶Kutokwenda Katika Shauri la Wasio haki wala Kukaa barazani pa wenye Mizaa.
▶Fanya Mapenzi ya Mungu maishani Mwako.

Mawazo ya MUNGU ni Wema kwetu,Wewe Simama na Utulie ndani yake tu.
Mungu akikutambulisha Nakuambia Hakuna Mwanadamu wa Kupinga.

👉Haijalishi wanadamu Watakudharau Kulingana na Mitazamo na Fikra zao ; wewe Usife Moyo kwa Maana aliyekuinua na Kukushika Mkono ni Mungu sio Wanadamu.

♦Nyenyekea chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili Mungu akuinue kwa wakati wake Yeye.
Kumbuka kwamba Unyenyekevu na Utii wako mbele za Mwenyezi Mungu Ni vitu muhimu sana Katika Maisha yako.
by Ibrahimu kakulu.





No comments: