Kumwaga mbegu za kiume walau mara 21 kwa mwezi hupunguza uwezekano wakupata tezi Dume
Kwa mwanaume unayehofia kuja kupata saratani ya tezi dume, kuna hatua angalau moja rahisi unayoweza kuichukua kukukinga dhidi ya hatari hii, na urahisi wake ni kutokana na kujiondolea hatari ya kupata ugonjwa mkubwa kiasi hiki ukiwa chumbani kwako tu.
Tafiti nyingi zimehusisha utoaji wa mara kwa mara wa mbegu za kiume (manii) — kwa kufanya mapenzi, kupiga punyeto au ukiwa usingizini — na kupunguza kwa kiasi kikubwa hatari za kupata saratani ya tezi dume.
Jambo hili linaweza kuleta tofauti kiasi gani?
Kwa mujibu wa tafiti iliyochapishwa mwaka 2016 kwenye jarida la European Urology, tofauti ya kufanya na kutofanya hivi ni kubwa sana.
Wanaume 32,000 walifanyiwa utafiti kuanzia mwaka 1992 mpaka mwaka 2010 na matokeo waliyoyapata ni kwamba wanaume waliripoti kumwaga mbegu za kiume angalau mara 21 kwa mwezi walipokuwa na umri wa miaka ya 20 (20’s) maishani mwao walikuwa na asilimia 19 zaidi ya kutokutwa na saratani ya tezi dume ikilinganishwa na wale waliokuwa wakimwaga mara saba tu kwa mwezi mzima au chini ya hapo.
Kumwaga mbegu za kiume mara kwa mara ukiwa kati ya miaka ya 40 (40’s) pia inakupunguzia hatari ya kupata saratani ya tezi dume kwa asilimia 22, utafiti huo umeonesha.
“Ingawa matokeo ya utafiti wetu inabidi yathibitishwe na tafiti zinazochambua utendaji kazi wa kibaiolojia, bado matokeo haya yanasema kuwa kutoa mbegu za kiume na kufanya ngono salama katika ujana wako wote yawezekana ikawa ni mbinu yenye manufaa makubwa kwa mwanaume katika kupunguza hatari ya kupata saratani ya tezi dume,” amesema Jennifer Rider, kiongozi wa utafiti huo katika mkutano na waandishi wa habari.
Hakuna idadi maalumu kwa mwezi ambayo mwanaume anatakiwa anamwaga mbegu ili kupunguza hatari hiyo. Kilichobainishwa kutokana na utafiti huu ni kwamba huwa inategemea sana na mahusiano ya kingono kati ya wapenzi ambapo hatari ya kupata saratani hii inapungua sana endapo mwanaume anapata fursa ya kutoa mbegu za kiume mara nyingi zaidi.
Hii si mara ya kwanza kwa watafiti kuendesha utafiti kubaini ni kwa jinsi gani kutoa mbegu za kiume kuna uhusiano na kupunguza hatari za kupata saratani ya tezi dume. Mwaka 2003 timu ya watafiti wa nchini Australia walilinganisha idadi ya mwanaume kumwaga mbegu za kiume kwenye utafiti uliohusisha wanaume 2,300 — ambao nusu yao walibainika kuwa na saratani ya tezi dume. Matokeo yalionesha kuwa wale waliotoa mbegu za kiume mara tano hadi saba kwa wiki walipunguza hatari ya kupata saratani ya tezi dume kwa asilimia 36 wakilinganishwa na wale waliomwaga mara mbili au pungufu ya hapo kwa wiki.
Ingawa tafiti hizi zimekuwa zikileta matokeo yanayofanana, watafiti bado hajapata sababu maalumu ya kwa nini kumwaga mbegu za kiume mara kwa mara kunapunguza kwa kiasi kikubwa hatari za mwanaume kupata saratani hii.
Jennifer Rider aliliambia Shirika la habari la Reuters kuwa timu yake ilikuja na dhana moja inayoelezea uhusiano huo: kwamba “Utoaji wa mbegu za kiume mara kwa mara, kwa kiasi fulani, ni kielelezo cha afya bora kwa mwanaume kwa sababu wanaume waliobainika kumwaga mbegu mara chache zaidi kwenye utafiti wao — ambao hawakumwaga kabisa au walimwaga chini ya mara tatu kwa mwezi mzima — walikuwa na uwezekano mkubwa sana wa kukutwa na magonjwa mengine na pia walikufa mapema kutokana na sababu mbalimbali zaidi ya saratani ya tezi dume. Pamoja na matokeo haya, tafiti zaidi zinatakiwa kufanyika ili kuelezea uhusiano wa kibaiolojia unaohusika kupunguza hatari hii.”
NOMA ZAIDI YA NOMA TAZAMA ROSA REE ALICHOKIFANYA KWA VIDEO:
No comments: