RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU 06

RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU

MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO (Mwandishi wa kitabu cha “ SIKU 71”)

SEHEMU YA 6

Kama unavyojua wabongo tunapokutana sehemu yoyote ile. Tuliongea kiswahili na sikusita kumpatia namba zangu za simu na nilimuahidi kumtembelea nyumbani kwake siku moja baada ya kunialika.

   Aliniambia anaishi Philadelphia.  Niliifurahia mualiko huo kwakua ni mji ambao sikuwahi kuukanyaga. 

   Siku mbili baadae niliwasiliana na Farhan illi niweze kumtembelea. Naye alinielekeza treni za umeme zilipo na kufika kwenye mji huo.

   Farahani alikua na usafiri binafsi. Hivyo alifika kunipokea na kwenda nyumbani kwake. Hakika alifurahi sana kupata ujio wangu kwake.

Farahani alikua ameoa Mmarekani na amezaa naye watoto wawili mpaka muda huo. Mmoja ana miaka minne na mwengine mdogo kabisa wa kunyonya. Ila mama yake alikua anampa maziwa ya kopo na si kunyonyesha kama waafrika tulivyozoea kuwapa watoto wetu maziwa asilia yatokanayo na tezi za mamalia wote ulimwenguni.
   “karibu sana Mwandishi jagina. Jisikie upo nyumbani.”
Farahani alinipa cheo hicho kilichonifanya nitabasamu tu.

   Kwa mazingira ya nyumbani kwake, Idadi ya wafanyakazi pamoja na idadi ya magari ya gharama niliyoyaona. Hakika Farahani alikua anaishi maisha ya kifahari sana. Naweza sema hakua na kipato cha kati. Sio tajiri anayetambulika, ila alikua na uwezo wa kwenda viwanja vya matajiri na akakidhi vigezo na masharti ya sehemu husika.  Alikua ni moja ya watu wanaishi vizuri nchini humo.

   Basi nilipokelewa vizuri na shemeji yangu wa Kimarekani na kuandaliwa vyakula vyao vitamu kabisa. Vingine nilishuhudia vikija kwa gari baada ya  kutoa  oda. Ilimradi tu vurugu zikawa nyingi kwa ajili ya kuonesha ukarimu wao kwa mgeni.

   Niliandaliwa mahala pazuri pa kulala. Japokua sikuwa na lengo hilo, Ila niliheshimu tu maamuzi yao kwakua nilipata watu ambao wamekithamini kipaji changu na kuufurahia uwepo wangu nyumbani kwao. 

   Maana niliona kitabu kingine cha Siku 71 kilichotafsiriwa kwa lugha ya kiingereza kikiwa kwenye kabati lao la kuhifadhia vitabu. Nikagundua kua hao watu wanapenda sana kusoma vitabu na wamekiamini kipaji changu.

   Basi nikalala nyumbani kwao siku hiyo na baada ya mapambazuko,niliamshwa na mwenyeji wangu kwa ajili ya kufanya mazoezi na kupasha misuli moto kwa kukimbia. 

   Kiukweli hua sifanyi mazoezi kabisa. Ila nilikubali tu kutii taratibu za wana familia. Maana kwenye nyumba hiyo kuna chumba kikubwa cha kufanyia mazoezi mbalimbali ya viungo. 

   Niliweza kumshuhudia shemeji yangu naye akifanya mazoezi. Hadi yule mtoto wa miaka minne naye niliona akifanya mazoezi ya viungo. Basi nikaungana nao na kufanya mazoezi kiasi.

   Baada ya kuweka mwili safi kwa kuoga. Tulikusanyana asubuhi hiyo na kupata kifungua kinywa. Hakika safari ya mji huo niliifurahia baada ya wenyeji wangu kuamua kunizungusha sehemu mbalimbali. Tulimaliza mizunguko hiyo saa tano usiku.

   Siku iliyofuata niliaga na kuondoka huku nikifurahi kuongeza familia huko Marekani. Waliniomba siku nyingine nikienda Marekani nisifikie hotelini, nifikie nyumbani kwao. Nilikubaliana nao na wao wakaonyesha wazi kufurahia kukubaliwa ombi lao.

   Ila nikikumbuka kua sina maelewano mazuri na Haiba na kuna uwezekano huo ndio ukawa mwisho wetu, basi hamu ya kuendelea kukaa Marekani huniisha na kutamani tu kurudi nchini kuendelea na uandishi wa kitabu changu kingine.

   Nikiwa hotelini, nilijiandaa kwa kuweka kila kitu changu sawa ili niweze kusafiri usiku wa siku hiyo kurudi nchini Tanzania.

   Ni kweli Haiba aliyatawala mawazo yangu kwa asilimia kubwa na kuushika moyo wangu hasa, ila nilitakiwa kukubali matokeo na kuachana na mawazo hayo kwakua Haiba mwenyewe hajavutiwa na mimi si wakati ana kumbukumbu zake wala wakati huu ambao tumeanza kufahamiana upya.

   Kitandani kulikua na kitabu ambacho nilikitia sahihi kabisa kwa madhumuni ya kumpatia Haiba kama zawadi pindi nitakapoonana naye. Nilikichukua na kukirejesha wenye begi. Hakika kilikua kipindi kigumu sana kwangu kukipitia.

   Baada ya kupanga vitu vyangu sawa na kuhakikisha kua muda ukifika ni kubeba tu na si kuanza kuhangaika tena, Nilitoka nje kwa ajili ya kuogelea kidogo japo kwa mara ya mwisho kabla sijarejesha funguo rasmi kwa mtu wa mapokezi hotelini hapo na kurudi nyumbani.
   “mambo..una muonekano mzuri.” 
Wakati nikiwa nayakata maji, nilipata sifa kutoka kwa msichana mzuri wa kimarekani aliyekua mita chache mbele yangu. 
   “nashukuru..” nilijibu na kujilazimisha kuachia tabasamu. 
   “tunaweza kuogelea wote?” yule binti aliuliza na kunisogelea mpaka pale nilipo huku akijichekesha  chekesha.
“mimi sipo vizuri sana kwenye idara ya kuogelea. Hivyo siwezi kuogelea na mtu mwengine. Niache nijifunze tu mwenyewe taratibu.” 
nilitoa majibu hayo huku nikitabasamu. Sikuhitaji kumkwaza ila niliona wazi kabisa kupitia uso wake kua sio jibu alilolitegemea kutoka kwangu kwa vile alivyonichangamkia na mimi nilivyompokea. 

   Msichana huyo aliondoka na kwenda kuogelea peke yake mbali kidogo na nilipokua. Nilimtazama kwa sekunde kadhaa, lakini sikumjali tena.

   Kiukweli hata sijui Haiba alikua amenipa kitu gani kilichokita kwenye moyo wangu. Maana toka nimeonana naye basi liile jalada la kupenda wasichana likawa limefungwa hapo.

   Hata mzazi mwenzangu nilianza naye mahusiano ya mapenzi kama bahati mbaya tu kwakua nilikua na hamu ya kufanya tendo. Tendo moja likasababisha mimba iliyotufanya tuishi pamoja. 

   Hivyo ilikua rahisi sana kwake kuondoka kwangu kwakua tu hatukupendana kiukweli. Mapenzi yangu yale ya dhati kabisa kutoka moyoni mwangu, yote aliondoka nayo Haiba na kuniacha nikiwa mchezeaji na si mtu wa kujali hisia za wengine.

   Nilimtazama msichana huyo, kisha nikaangalia kushoto na kulia. Kusema ukweli hapo kwenye bwawa la kuogelewa watu karibia wote walikua wanaogelea wawili wawili. 

   Nilimshuhudia akitoka kwenye maji baada ya kuboreka. Hakika nilijihisi nina hatia, hivyo na mimi nikatoka kwenya maji na kumfuata.
   “naomba ukanifundishe kuogelea.” 
Nilitoa sauti baada ya kumsogelea na kumafanya msichana huo ageuke na kukutana na mimi uso kwa uso. Hakika uso wake ulionesha wazi kuwa na hasira kwa jinsi ndita zilivyojikunja kwenye paji la uso wake.

   Nilimtazama usoni na kumfanya hata yeye kulegeza kidogo macho yake na sura yake ikakunjuka na kujaa nuru.
   “mimi si mwalimu mzuri... Najua kuogelea mwenyewe tu na si kumfundisha mtu.” alinijibu hivyo na kutaka kuondoka. Nilimuwahi na kumshika mkono.
   “naitwa Molito. Nitafurahi nikikufahamu mwalimu wangu mpya wa kuogelea.” nilijitambulisha na kumfanya atabasamu.
   “naitwa Alice.” alinijibu na kunifanya nikumbuke moja ya majina niliyoyatumia kwenye riwaya yangu pendwa ya Alice the superstar. 
   “nimefurahi kukufahamu Alice.... Twende tukaogelee.” niliongea maneno hayo na kumkonyeza.

   Hakika niliweza kurejesha uso wa furaha aliokuja nao mara ya kwanza kabla sijaipoteza furaha yake. Alikubali kurudi kwenye maji na kuogelea na mimi.

Hakika tulifurahi pamoja na baada ya kutoka kwenye maji tayari tulishakua marafiki. Na kuongea hiki na kile.
   “kwa hiyo hautarudi tena huku Marekani?”
Alice aliniuliza swali hilo baada ya kumwambia kua usiku wa siku hiyo nitasafiri na kurudi nyumbani kwetu.
   “sidhani... Labda kwa ishu maalumu naweza kuja tena.” nilimjibu na kumtazama Alice ambaye alionesha wazi kuufurahia ukaribu wangu kwake.
   “siku moja nitakuja mimi mwenyewe huko Tanzania kwa ajili ya kukutembelea. Niaminishe kama utaweza kunipokea.” 

   Alice aliongea kauli hiyo iliyonifanya  nishuke sana. Sikutegemea kuisikia kauli hiyo kutoka kwa msichana huyo mgeni. 
   Nilimtazama machoni na kujaribu kuyasoma macho yake. Nilijiaminisha kua msichana huyo alishanipenda.
   “unaweza kusafiri kutoka huku Marekani hadi Tanzania kwa ajili yangu?” nilimuuliza swali hilo  na kumtazama tena kwenye macho yake. 
Aliona aibu kidogo kisha akarejesha uso wake kwangu na kunitazama.
   “nimevutiwa sana na wewe.... Ni mvulana mzuri sana. Unajali na pia unaonesha ni mkarimu sana. Nimejisikia unyonge baada ya kusema kua unaondoka leo hii ili hali ndio siku ya kwanza kukuona. Kama tatizo ni pesa za kuendelea kuishi huku naomba uniambie, nitakulipia wiki moja zaidi hapa hotelini ili  mradi tu usiondoke leo hii.” 
Maneno ya Alice niliyasikia vyema na kunifanya nizidi kumuona msichana huo ni wa ajabu sana kuwahi kutokea. Nilitamani Alice angekua Haiba. Ila ndio hivyo tena, moyo wa Haiba umenikataa kabisa.
   “kuna kazi naenda kuifanya. Nitakuja tena kwa ajli yako Alice.” niliongea hivyo na kumfanya msichana huyo afurahi sana.
   “kweli Molito?” aliniuliza ili kupata uhakika zaidi.
Nilitabsamu na kumuhakikishia kua nitarudi tena Marekani kwa ajili yake.

   Tulibadilishana namba za simu na msichana huyo akaondoka.
Wakati huo kiza kilikua kimshaanza kutanda. Magazeti ya jioni yakapitishwa na mimi nikachukua gazeti moja ili kupitisha macho.

   Nilipatwa na mshtuko mkubwa sana baada ya kuangalia kurasa ya mbele kabisa ya gazeti hilo.
Kichwa cha habari kilisema mfanya biashara auwawa kwa kupigwa risasi nyumbani kwake. Picha ya mfanya biashara huyo ilikua ya Farahani.

   Habari hiyo ilinitatiza sana na kufungua ukurasa wa pili ili niweze kuisoma habari hiyo.
Dah, hadi jina lililoandikwa chini ya picha ya marehemu  iliyokua ndani ya gazeti hilo ni la Farahani. 

   Niliumia sana na kuchanganyikiwa pia. nani aliyefanya mauji ya Farhani na alikua anataka nini kutoka kwake?  Maana maelezo yaliyoandikwa kwenye ukarasa wa ndani, yalisema kua hakuna kitu kilichoibiwa kwa maelezo ya awali ya mke wake. Farahani alikua mtu mpole na mwenye upendo sana, nyuma ya pazia alikua na matendo gani yaliyompelekea mpaka watu kuamua kumuua? 

   Nilimkumbuka mke wake na watoto wake wadogo kabisa, hapo roho ilizidi kuniuma kwakua familia  hiyo ilikua moja ya ndugu zangu wapya. Na ukizingatia nimetoka kuonana nao masaa machache tu yaliyopita.

   Kufumba na kufumbua, askari kadhaa wakafika hotelini hapo wakiwa na silaha za moto.
Nilibaki nashangaa tu. Askari mmoja aliyekua na picha alinisogelea na kuniangalia.
   “upo chini ya ulinzi, weka mikono kichwani na upige magoti.”
Sauti hiyo ilinifanya nifanye vile nilivyoelekezwa na kumfanya askari huyo kuwaita wenzake.
Nilifungwa pingu na kupandishwa kwenye moja ya magari yao ambayo hayakuniruhusu nione nje tena.

   Hisia zangu ziliniambia moja kwa moja  kwamba nilikua nahisiwa na askari hao kuhusika na mauaji ya Farahani. 
   Maana kwa maelezo yao wenyewe pindi nilipokua nyumbani kwao, ni muda mrefu sana toka wahamie huko Philadelphia hawakupata kutembelewa na mtu yoyote yule.hivyo ujio wangu mimi kwenye familia hiyo ulileta hiyo dhahma kwao.

   Nilikua mpole mpaka gari liliposimama na kuamrishwa kushuka kwenye gari hilo. Nilitii amri hiyo kuingia kwenye kituo cha polisi.

   Baada ya muda wa masaa matatu kupita, nilichukuliwa na kupelekwa kwenye chumba cha mahojiano.
   “naomba nitajie majina yako yote matatu.” 
hilo ndilo lilikua ombi la kwanza la askari huyo mpelelezi ambaye alikaa na mimi meza moja kwa ajili ya kunihoji.
   “Naitwa Hussein Omary Molito.” 
nilijibu na kumtazama Askari huyo kwa macho yaliyojaa mashaka.
   “ndugu Molito, unaweza kuniambia umemfahamu vipi marehemu Farahani Salim?”
 askari huyo aliniuliza swali hilo na kumwaga picha za marehemu tulizopiga pamoja kupitia simu yake huku zingine nikiwa na familia yake kwa ujumla.
   “nimemfahamu muda mfupi sana. Hata siku nne sidhani kama zimefika toka tufahamiane mpaka umauti ulipomfika. Ila kilichotuweka karibu mimi na yeye ni vile nilimuona akiwa na kitabu changu cha Siku 71. Nilimkuta akikisoma pale Hotelini. Nami  nikamfuata na kumsalimia shabiki yangu. Maana kilichonivutia ni vile alikua anasoma kitabu cha kiswahili. Hivyo nikajua ni ndugu yangu tu kutoka Afrika ameniungisha kwa kununua kitabu changu cha Kwanza. Kiukweli hata yeye mwenyewe alifurahi sana kuniona Mwandishi wa kitabu hicho kilichomvutia. Tukapeana namba za simu na mwishoni akanialika niende nyumbani kwake. Basi baada ya siku mbili nikaenda kumtembelea na nikalala kabisa. Hakika walinipokea kwa furaha sana na kunizungusha mji huo mgeni kwangu. Siku ya kuondoka ndio matukio ya kupiga picha za kumbukumbu kama hizo yakafuatia. Hivi mnavyoniona nimekata tiketi ya ndege ya usiku huu kwa ajili ya kurudi nyumbani.” 
nilitoa maelezo ambayo bila shaka yalikua yanarekodiwa. Maana mpelelezi huyo hakua na peni wala karatasi.
    “nyumbani kwenu ni wapi?” nilikumbana na swali hilo.
    “Tanzania.”
    “unamjua huyu?”
nilitupiwa picha kadhaa na kunifanya nizichukue na kuanza kuzitazama. Niliweza kumgundua mtu aliyekua kwene picha hizo. Alikua ni Alice.
   “huyu msichana ndio kwanza nimeonana nae leo.... Ndiyo mara yangu ya kwanza.” nilijibu na kumfanya mpelelezi huyo arejeshe picha zote kwa bahasha moja na kunitazama usoni kwa muda wa dadika mbili bila kuongea kitu chochote.
   “umeshawahi kung’atwa na ng’e?” 
Nilikutana na swali hilo baada ya kunitazama muda mrefu huku na mimi nikijaribu kushindana naye ili asihisi uoga niliokua nao muda huo.
   “mara nyingi sana.” nilijibu na kumfanya atabasamu kidogo na kunitazama usoni.
   “bila shaka uchungu wake unaukumbuka vyema?” niliulizwa swali lingine.
   “ndio.” 
nilijibu na kumfanya  mpelelezi huyo asimame nakutoka kwenye kiti chake na kuanza kuzunguka zunguka. Alifika kwenye sikio langu la na kuninong’oneza.
   “kama hautokua mkweli kwa chochote kile nitakachokuuliza.... Basi ujue utapata mateso yaumayo kama sumu ya ng’e, na mwisho wa kila kitu utaishia kwenda jela na utakaa huko maisha yako yote.” 
Askari huyo aliiongea maneno makali yaliyonifanya nimeze mate.  Maana ujasiri  wote uliniisha na kujiona kabisa nikiwa hatiani na naweza kufungwa kweli iwapo nikishindwa kujitetea bila kufanya kosa la aina yoyote ile.

   Yule askari alizunguka tena na kusimama mbele yangu.
   “sasa naomba uniambie... Ni kitu gani hasa kilichokufanya umuue Farahani?” niliulizwa swali hilo na askari huyo aliyegandisha macho kwangu bila kupepesa.

   “kusema ukweli wangu ule wa haki kabisa na Mungu ni shahidi kwa hiki nikiongeacho. Mimi sijamuua Farahani.” niliongea huku nikiwa nimepoteza ile hali ya kujiamini. Machozi yalianza kunilengalenga na vipele  vya woga vilinitoka mwili mzima.
   “kijana naomba unisikilize kwa umakini sana. Mimi hua sihoji watu muda mrefu bila kuwatesa kidogo. Hivyo naomba ushirikiano wako kwa kila swali nitakalokuuliza. Mimi nahitaji kujua sababu ya kuua kwako. Na si kujua kama umeua ama laa. Maana nina uhakika wa asilimia mia moja kua umeua. Ila nahitaji tu kujua sababu za kuua kwako ni zipi hasa........ Huenda ukapunguziwa adhabu.” askari huyo alipaza sauti na kunizidisha uoga. Maana toka nimezaliwa sijawahi kupelekwa polisi hata mara moja. Hivyo kitendo cha kukaa humo tu, kilinifanya nikose amani kwenye moyo wangu tena ukizingatia kwa kesi nzito ambayo inanikabili mbele yangu.
   “nisemacho kweli kabisa ndugu Askari.... Sijaua mimi.” nilongea maneno hayo huku machozi yananitoka.

   Yule askari alienda kukaa kwenye kiti chake na kufungua droo iliyokua kwenye meza hiyo. Alitoa nyundo na msumeno.
   “sheria yetu ya huku Marekani kwa makosa kama yako tunaruhusiwa kukukata hata kidole katika kuutafuta ukweli kwa watu wajeuri kama wewe. Na kukiri kwako kwa makosa ambayo tuna uhakika nayo ndo kupona kwako. Sasa utachagua mwenyewe kwa ridhaa yako. Unatamani  kwenda jela ukiwa umepungukiwa kidole kimoja au utasema sababu ya wewe kumuua mfanyabiashara Farahani?”
Yule askari aliongea maneno hayo na kunifanya nizidi kutetemeka na kuzidi kulia. kiukweli nilikua sijui nifanye nini ili niaminike.
   “umegoma kusema?”
 nilishtushwa na swali hilo lililonifanya nikatae kwa kutikisa kichwa.
   “sema sasa... Muda unaenda .... Tuna kazi nyingi za kufanya na sio kusumbuana na wewe mshenzi mmoja.” asari huyo alifoka na kunifanya niendelee kulia bila kutoa jibu lolote.
   “kumbe ni jeuri eeh... Vijana, niwekeeni vidole vake mezani niifanye kazi yangu.” 
Askari huyo alitoa amri na kuwafanya askari waliokua wamesimama pembeni yangu kunikamata na kunilaza kwenye meza. Walichukua mkono wangu na kuuweka mezani. Vidole vyangu vingine walivikunja na kubakisha vidole viwili. 

   Sura yangu iligeuzwa pembeni ili nisishuhudie kile kinachotaka kutendeka.
Niliweza kuhisi msumeno ukiwekwa kwenye vidole vyangu. Alisugua kidogo na kunisababishia majeraha. Hisia zangu ziliniambia kua sasa alikua ananyanyua nyundo na kupiga kwenye ule msumeno na kuvikata vidole vyangu kikatili.
   “nitasemaaaa.”
Nilipaza sauti kabla hatua nilizohisi kuchukuliwa muda huo hazijachukuliwa.
   “sema hapahapa.... Nikiona unaongea ule upuuzi wa mwanzo...nakata vidole.”
Askari huyo aliongea huku akionyesha wazi kudhamiria kufanya kitendo hicho.
   “ni kweli nimemuua Farahani.”
Nilijikuta nmeongea hivyo ili niachiliwe. Maana kadri yule askari alivyokua anasugua msumeno kwenye vidole vyangu nilikua napata maumivu makali. Hata wale askari wengine walivyokua wananikandamiza kwa nguvu kwenye meza walikua wananipa adhabu ambayo sikuitarajia kuipata kwenye maisha yangu.

   Baada ya kukiri kumuua Farahani. Waliniachia na kunifanya nikae sawa huku nikiviangalia vidole vyangu vilivyokua vina alama ya michubuko  na damu kiasi.
   “toka mwanzo nilikuambia.... Ukitaka amani. Ni lazima ujibu maswali yangu kwa ufasaha. Kwa sasa nakuacha upumzike na daktari atakuja kukubandika plasta vidoleni. Mimi na wewe tutakutana tena kesho eneo hili hili. Ila nikuhabarishe tu, hutakaa kwenye kiti kama leo hii. Bali utafungwa pale kwenye kitanda ambacho kina mashine za umeme. Nadhani ukiwa unatekenywa kidogo pale kwa shoti za umeme hutaleta usumbufu kama huu wa leo. Kwa heri Mr. Molito.”
Askari huyo aliongea na kutoka kwenye chumba cha mahojiano.

   Nilichukuliwa na kurudishwa rumande. Nusu saa baadae dakatari alifika na kuvisitiri vidonda vilivyopo kwenye vidole vyangu.

   Mawazo yaliniandama. Nilihisi huenda uongo niliomuongopea mpenzi wangu ndio unanihukumu. Maana sikuenda kusaini mikataba na wazungu kama nilivyomwambia wakati namuaga, badala yake nimeenda kutafuta majanga japo dhumuni lilikua ni Haiba.
“Haiba umeniponza.”
Niliongea peke yangu huku nikijutia maamuzi yangu.  Hakuna aliyenisikia. Kwenye chumba hicho nilikua peke yangu na kitanda kidogo kwa ajili ya kupumzika.

   Nililetewa chakula japo sikuweza kukila pia kutokana na mawazo yaliyo nitawala. Usiku nilikosa usingizi na asubuhi napo pakawahi kukucha. Nilikua nawaza pindi ambapo nitawekwa kwenye kitanda chenye umeme nakurushwa kama vile nilivyokua naona tu kwenye filamu zao jinsi ambavyo hata makomando wanalia.

   Kufumba na kufumbua,mlango ukafunguliwa, na mimi nikatolewa ndani na kupelekwa kwenye chumba hicho ambacho sasa kilikaa kwa ajili ya mateso na si mahojiano ya kiamani kama hapo awali. 

   Moyo wangu uliniambia nikubali kila kitu ili niepukane na mateso. Ila nikipelekwa mahakamani ndio nikane kua sijahusika.

   Baada ya kuwekwa kwenye kitanda cha chuma kilichosimamishwa na kufungwa vizuri. Nilishuhudia mabetri makubwa ya kipangwa na kuunganishwa vizuri ili kusafirisha umeme na kuuleta kwenye kitanda. Niliweza kuona akijaribu kugusanisha vifaa kama vibanio kwa mbele  na kutoa cheche.
   “unaweza kusema kwanini ulimuua Farahani?” niliulizwa swali hilo na askari aliyepewa kazi ya kunihoji toka siku iliyopita.
   “naweza kusema mkuu... Usinipige shoti.” niliongea maneno hayo kwa woga na kumfanya yule askari atabasamu.
    “haya... Elezea ni kipi hasa kilichopelekea kumuua Farahani?”
 nilikumbana na swali hilo. Kiukweli sijui chochote, ili kutoka kwenye mateso ambayo nilikua nahisi nitayapata, ilinibidi nitumie kipaji changu cha kutunga riwaya kuongea chochote kile ili ninusurika na shote hizo..
   “kiukweli mimi na Farahani tulikua tunafanya kazi pamoja miaka saba iliyopita na tukafikia hatua ya kudhulumiana pesa toka tukiwa nyumbani kwetu nchini Tanzania. Hivyo nilipopata habari kua amekua mfanya biashara mkubwa huku nchini Marekani, ndipo nilipoamua kufunga safari na kumfuata huku ili aweze kunilipa pesa zangu.Baada ya kufika nilimtafuta sana. Na mwisho nikafanikiwa kumuona. Nilimfuata na kumuambia kua sikuja kwa shari ila tuongee tunawezaje kulipana lile deni ninalomdai. Basi naye akanipeleka nyumbani kwake na kunikarimu. Kisha tukatoka na kwenda kuongea. Bado kiswahili kilikua kingi na hakuonyesha dalili zozote za kunilipa pesa zangu zaidi ya kumsakizia mtu mwengine kua ndio kachukua. Ndipo nilipokasirika na kwenda kuwapa pesa wahuni na kuwaelekeze wakamfundishe adabu. Sikuwatuma wamuue, hao wahuni wamenitafutia tu matatizo.Huo ndio ukweli wangu jamani.”
   Maneno na sura yangu yalionyesha hatia niliyokua nayo juu ya kosa hilo. Nilishuhudia wakijipongeza kwa kuwarahisishia kazi na mimi kutolewa kwenye kitanda hicho na kusubiri siku inayofuata RIWAYA: PENZI LANGU LINAVUJA DAMU

MTUNZI: HUSSEIN O. MOLITO (Mwandishi wa kitabu cha “ SIKU 71”)

SIMU: 0718 97 56 59

   Maneno na sura yangu yalionyesha hatia niliyokua nayo juu ya kosa hilo. Nilishuhudia wakijipongeza kwa kuwarahisishia kazi na mimi kutolewa kwenye kitanda hicho na kusubiri siku inayofuata nipelekwe mahakamani.
ITAENDELEA................nipelekwe mahakamani.
ITAENDELEA................

  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO

No comments: