TATIZO LA HARUFU MBAYA UKENI NA MATIBABU YAKE



Leo tutazungumzia tatizo linalowasumbua wanawake wengi, tatizo la kutokwa na uchafu unaotoa harufu mbaya sehemu za siri. Kitaalamu hali ya mwanamke kutokwa na majimaji yenye rangi nyeupe au ya njano. Ni hali ya kawaida na wala siyo tatizo endapo majimaji hayo siyo mazito sana na wala hayatoi harufu mbaya. Lakini endapo majimaji yanayotoka yapo katika hali ya ute mzito wenye rangi nyeupe au kahawia, yanatoa harufu kali na yanawasha, basi hiyo ni ishara ya ugonjwa uitwao Vaginosis.

Majimaji au ute unaoteleza kutoka sehemu za siri ni njia inayowezesha viungo vya uzazi vya mwanamke kujisafisha na kuutoa uchafu wa seli zilizokufa na mabaki ya damu ya hedhi nje ya mwili. Pia huvikinga viungo vya uzazi dhidi ya maambukizi ya bacteria au fangasi wanaoleta magonjwa.

Kwa kawaida huwa hayatoi harufu na huwa na rangi nyeupe au ya njano. Pia huwa na asidi ya Lactic ambayo huzuia kuzaliana kwa vijidudu vya maradhi na huzalishwa kwenye tezi za Bartholin (Bartholin's glands) zilizopo kwenye shingo ya mlango wa uzazi (Cervix). Kwa kawaida, mwanamke hutoa kiasi cha gramu 2 za seli zilizokufa kutoka kwenye mji a uzazi na gramu 3 za ute mwepesi kila siku. Kiwango hiki huweza kuongezeka au kupungua kutegemeana na mzunguko wa hedhi. Kuna wakati ute huwa mwepesi na unaovutika (kama ute wa yai la kuku) na kuna wakati huwa mzito kiasi na wenye rangi ya njano. Ute huu ni wa kawaida na huwatoka wanawake wote hususan baada ya kuvunja ungo.

Sababu za kutokwa na uchafu huo Kuna sababu nyingi ambazo husababisha mwanamke kutoa ute au majimaji yasiyo ya kawaida kutoka kwenye sehemu zake za siri. Maambukizi ya bacteria wanaosababisha magonjwa kama Trichomoniasis, Candidiasis, Gonorhear au uambukizo wa bacteria Candida albicans, Vaginosis Bacteria n.k husababisha mwanamke kutokwa na uchafu unaoambatana na harufu mbaya.

Pia mabaki ya vitambaa, tissue au pedi ambazo hazikutolewa wakati wa hedhi huweza kusababisha tatizo hili. Usafi wa sehemu za siri usipozingatiwa hususani mwanamke anapokuwa kwenye siku zake za hedhi, huweza kuwa mazalia mazuri ya bacteria wanaosababisha harufu mbaya.





  WAKUBWA TU :Tazama Video za kikubwa hapa




No comments: