Unachofanya leo kwa mwenzako ndicho kinaenda kutengeneza tafsiri yako katika fikra zake kesho

.



Anaweza kuwa anakupenda na kujitolea sana kwako, anaweza kuwa ameapa kwamba hata iweje hawezi kukuacha ama kukuumiza, ila fahamu yote anayosema ama kuyafanya nikutokana na ULEVI wa mapenzi alionao juu yako unaotokana ama na upya wa penzi lenu ama uzuri wa matendo yako kwake.

Ili kila siku ajihisi hatia kukufanyia tofauti, ni jukumu lako kuijaza picha yako katika akili yake kupitia vitendo na maneno yako.

Matendo yako ya hovyo yanafanya akili yake iwe na picha ya hovyo juu yako, athari ya suala hili ni kwamba abadani hawezi kuhisi hatia pale akipata ushawishi wa kukufanyia ujinga kwa sababu atakuwa na excuse kwamba mtu mwenyewe hueleweki.

Hali ya hisia za mwenzako inabadilika kutokana na matendo yako(WE CALL IT EMOTIONAL ECONOMY)

Waliopendana miaka ile na kuachana leo si-kwamba walidanganyana walipokuwa wakiambiana wanapendana sana, hapana, ila leo imefika hatima ya uhusiano wao kutokana na jinsi walivyokuwa wakitendeana.

Unaweza kuwa unapendwa sana ila hiyo haina tafsiri kwamba unaweza kupendwa daima hata kama ukiwa kivuruge kila siku.

Fikra za mwenzako ni kama maji ya kunywa, kadri zinavyokuwa safi juu yako ndipo afya ya penzi lenu linavyozidi kuwa timamu, ila zikianza kuchafuka na kukawa hakuna jitihada za makusudi kuzisafisha, kama ambavyo maji machafu ya kunywa yanavyoweza kukatisha uhai wako ndivyo fikra zake chafu juu yako zitakavyoharibu hisia zake na kupelekea kifo cha penzi lenu au matatizo ya kila siku.

Ujinga wa kila siku kwa mwenzako hata kama unaambatana na "Babe Am sorry" jua unaenda kutengeneza uasi katika fikra zake, uasi ambao baadaye utajionesha ktk tabia zake kitu kitakachoweka rehai uhai wa penzi lenu.

Share





No comments: