Wanaume mnawakosea Sana wanawake kwenye tendo la ndoa Amkeniak
WANAUMEUkipata bahati ya kuzungumza na wanawake kumi, nane kati yao kama si tisa watakuambia hawafurahii tendo la ndoa kabisa. Wanalifanya tu kwa mazoea au wajibu kwamba ana mke au mpenzi wake na lazima afanye.
Tatizo hili linawatafuna sana walioko kwenye ndoa. Wanawake wengi kwenye ndoa ni waathirika wa hili, tatizo wengi wao wanalificha labda kwa sababu ya usiri wenyewe. Ni jambo ambalo kiasili lina usiri fulani hivi, wanachagua kuitunza siri hiyo.
Nimepata nafasi ya kuzungumza na baadhi yao, malalamiko yao ni kwamba wanaume wengi wanashindwa kuwaandaa. Wanalifanya tendo chini ya kiwango, hivyo kujikuta maisha yao yote hawafurahii tendo la ndoa.
Inafika mahali mwanamke anakuwa hatamani kabisa kukutana na mwanaume wake. Au akikutana naye anafanya tu ili kumridhisha, halafu yeye anakuwa akili wala haipo pale. Inawaza mengine kabisa na ikitokea amejaribu tu kuchepuka, basi haachi.
Anakuwa na mume kama jina, lakini furaha ya tendo la ndoa anaipata kwa mwanamke mwingine. Ana kidumu chake pembeni kinachompa furaha. Bahati mbaya sana, malalamiko ya wanawake wengi ni kwamba wanapowashirikisha wanaume wao wamekuwa wazito kukubaliana nao.
Mwanaume anaelezwa ukweli kwamba kuna kitu hakipo sawa kwenye penzi lake, halifurahii tendo, lakini badala ya kuangalia nini cha kufanya kupata suluhisho, anakuwa mkali. Anahisi amekosewa adabu na ugomvi mzito unaibuka.
Marafiki zangu, lazima mambo haya tuyazungumze kwa upana wake ili kuweza kupata suluhisho la kudumu. Tusiishi kwenye uhusiano au kwenye ndoa kimazoea. Madhara yake ni makubwa mno, hivyo kila mmoja wenu anapaswa kuchukua hatua.
Mwanaume ukubali kujifunza kutoka kwa mwanamke, lakini pia uwe tayari kuyatekeleza yale yanayopaswa kufanywa ili tendo lako liwe na kiwango. Ndugu zangu, tendo la ndoa linahitaji utulivu wa akili na mwili.
Ili ulifanye kwa ukamilifu wake, linahitaji utulivu wa akili zenu wote wawili. Hivyo kama mwanaume upo tayari, lazima uhakikishe akili ya mwenza wako nayo inakuwa sawa. Usiwe mbinafsi kwa kuiweka tayari akili yako tu, halafu ya mwenzako ukaachana nayo.
Tendo la ndoa halihitaji kushtukiza kama vile unazima taa. Linahitaji maandalizi ya mwili na akili. Mwanaume unatakiwa umpange mwanamke wako. Mathalan siku hiyo unahitaji kufanya tendo hilo, unapaswa kumtengeneza mwenza wako kisaikolojia kwamba ajisikie mwenye furaha.
Mfanyie mambo madogomadogo ambayo yatamfanya ajisikie umemjali. Unaweza kumbebea zawadi, unaweza kumtumia ujumbe wa kuonesha unamhitaji kwa kumpa maneno matamu ya ushawishi wa kimapenzi. Usimuonee aibu, mueleze jinsi anavyokuvutia.
Mueleze jinsi anavyokufurahisha mnapokuwa dimbani na ikiwezekana mueleze kabisa siku hiyo unahitaji akufanyie utundu gani ambao huwa unakufurahisha. Mueleze nawe utafanyaje ili kumtendea haki, unapompa maneno hayo yanamuandaa kisaikolojia.
Yanampa mshawasha wa kulifikiria tendo. Yanamjenga kisaikolojia kwamba tendo hilo linakwenda kumfurahisha, hivyo kweli mnapokwenda kulifanya linakuwa na furaha kwa pande zote mbili na hiyo ndiyo maana halisi ya uhusiano.
Mnapofurahia wote, maisha yenu yatakuwa na furaha kila siku. Anapolifurahia mmoja, halafu mwingine anateseka, ni hatari na madhara yake ni makubwa. Kama unahisi una tatizo linalohitaji utalaam wa kidaktari, waone ili wakusaidie.
Usiwe mbabe, tendo hili linahitaji utulivu. Linahitaji ushirikiano wa watu wawili, shirikianeni mwanzo hadi mwisho. Kila mmoja amuone mpya mwenzi wake kila siku. Msikubali kuishi kwa mazoea!
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: