Wanawake Acheni kupekenyua simu za wapenzi wenu
Habari ya wakati huu msomaji wetu, leo tutazungumzia kipengele cha ukaguzi wa simu katika mahusiano.
Nataka nikuelimishe jambo moja katika mahusiano yako jifunze kuacha kupekenyua simu ya mwanaume wako.
Wengine wanapekenyua simu yaani kama inauwezo ya kuchanika ingechanika embu achana na hiyo tabia haiwezi kukusaidia chochote sana sana utaambulia maumivu bila tiba.
Kuna mahusiano yamekufa kwa ajili ya kukaguana simu nadhani jambo la msingi ni kuangalia mwenza wako anakupenda? Je anakujali? Je anakuthamini? Je anakupa amani ya moyo? Je anakubembeleza pale unapokuwa naye? Je anakutimizia mahitaji yako?
Watu wengi wanapoanzisha uhusiano huwabana sana wapenzi wao kwa kuwapekulia simu, kuwachunga watokapo na waingiapo, jambo ambalo huwafanya wahusika kujilinda sana wakiamini wanafuatiliwa.
Ndugu yangu usimbane mpenzi wako, mwache huru, atembee atakavyo na awasiliane na amtakaye, wewe kaa nyuma yake ukimchunguza bila mwenyewe kujua.
Na kama mume wako ameanzisha tabia mbaya au ana mchepuko utamgundua haina haja kila wakati kumnyang’anya simu na kumkagua haiwezi kukusaidia
Hivi kwa mfano huyo mwanaune wako kanunua simu anawasiliana naye akiwa ofisini na akirudi nyumbani simu anaiacha ofisini akirudi nyumbani unapekua huoni kitu utaanza kujisifu mume wangu hana mchepuko ha ha ha ha wanawake wenzangu tunapotea embu tuangalia vitu vya msingi.
Acheni kupekua hizo simu utakutana na mambo mazito yakufanye ukose amani ya maisha.
Huwa najiuliza mbona wanaume sio wapekuzi kama wanawake. Wengine mmewasababisha hadi wanaume zenu wanakwenda kuoga na simu.
Kuna vitu vingi vya kugundua mume wako kama ana mchepuko bila hata kumkagua simu yake kwani kuna tabia zitaanza kubadilika.
Hivi mumeo akianza kurudi asubuhi ni mpaka uchukue simu yake na kuikagua? Hivi ifike usiku wa manane unampigia simu hakupokelei wakati alikuwa anakupokelea hapo pia utachukua simu kukagua?
Na ukiona mwanaume wako alikuwa anakupa simu yake siku hizi hataki ushike ujue hapo kuna kitu kinachoendelea.
Pia ukiona mwanaume wako kila mara anakubadilishia password ujue kuna tatizo hapo yaani hataki uingi kwa simu yake.
Ni vizuri ukafanya busara kama kabadilika mjulishe maana kupekua simu hazitakusaidia.
Kuna mmoja alikuwa anamkagua mume kila anapirudi usiku siku hiyo alikutana na message nzito katika simu ya mumewe tena anamuambia asante kwa penzi ulilonipa naomba kesho turudie.
Huyu dada alikuwa anaona hakukuchi usingizi haupati ni kulia muda muda wote hadi kazini kashindwa kwenda mwanaume ndio kwanza hana muda wa kumsikiliza.
Ndio kwanza alimuambia naona ndoa itakushinda kwa ajili ya hii simu. Nataka kukuonyesha maumivu ambayo unajitengenezea alafu mume hana muda na wewe.
Usipende kukagua simu ya mume wako kila mara kwani haitakusaidia kurekebisha tabia zake. Utakuta mwingine akushakagua anashindwa kumuuliza mume wake kile ambacho amekuona anaendekea kubaki na maumivu moyoni.
No comments: