Kwanini Wanaume Wengi ni Waoga Kuoa Wanawake Wazuri Lakini Wako Tayari Kuwafanya Wapenzi wa Pembeni?



Wanaume wengi walioulizwa sababu za kuwatumia na kuwatelekeza wanawake wa jinsi hii walisema kuwa, kwa kutembea, kuonekana nao au kufanya nao mapenzi, wanaume hawa hujihisi sifa sana, hususani wanapoonekana na wanaume wenzao, yani ni kama vile timu ndogo iliyopata nafasi kucheza katika kombe la dunia. 

Unajua tena wanaume wanavyopenda kujionyesha wanapokuwa na wanawake wazuri mbele ya macho ya wanaume wenzao. Wamesema kwamba wanapowaza kuishi na wanawake hawa kama mume na mke, huwa wanazidiwa na hofu ya kuelemewa au kujihisi kutokuwa salama “sense of insecurity”. 

Wanaume wengine walioulizwa walijibu kwamba,wanawake wa jinsi hii ni wa gharama sana, sio rahisi kuwaweka mjini na kuhakikisha wanaishi maisha yao ya kawaida kama hauna fedha ya kutosha. Hata wale wanaume wachache waliokuwa na hao wanawake kwa muda wa maswali haya wameeleza jinsi wanavyohisi wanatumia fedha nyingi na yamkini zaidi ya wanavyojiweza. 

Wanawake wa aina hii watahitaji mitoko ya nje ya mji, sehemu zilizojitenga, sehemu za faragha ambazo ni za bei ghali, wanataka zawadi za gharama, ukitaka kuwapa zawadi za kushtukiza “surprise” basi ujipange, sio vitu vya kitoto vitakavyomsisimua aweze kukwambia “waoooooow…this is wonderful” hapo lazima ujipinde mfukoni haswa. 

Na wengine wameenda mbali zaidi kueleza kwamba hata unapotaka kuzaa na mwanamke wa jinsi hii basi yeye anataka mtoto mmoja au wawili tu akiogopa asije kuliharibu umbo lake, tofauti na kiu ya mwanaume ya kupata watoto zaidi ya wawili. 

Imeelezwa kuwa hata ujuzi wa kupika kwao ni shida maana kutwa kucha wako “bize” na sura zao, na hata ukikaa nao sio watu wakufurahisha zaidi ya kutumia tu hela zako “they are boring”



  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: