Simulizi: KAHABA (08)





story Tamu:
Simulizi: KAHABA (08)



ILIPOISHIA
“Hayo ndiyo maneno. Siyo unakuwa unaleta ngonjera zako hapa ambazo hazieleweki kama siyo mwanaume bwana!”. Jasmine a liongea huku akionesha wazi kwamba alikuwa na furaha kutokana na maneno yangu.
SASA ENDELEA
Ujauzito wa Jasmine ukazidi kuyaimarisha mapenzi yetu. Mimi nikampenda sana Jasmine na yeye pia akanipenda sana. Tulithaminiana na kuheshimiana. Tuliweka ahadi na mipango mingi na kabambe katika kuliimarisha penzi letu.
Ujauzito wake ukazidi kukua kwa kasi. Miezi ikazidi kukatika. Kichwa changu kikawa na mawazo mengi sana ambayo yalikuwa yakizidi kuongezeka kila uchao.
Nilikuwa nikiwaza ni namna gani nitaweza kukabiliana na varangati la mama Careen pindi ambapo atakuja kuyagundua mahusiano yangu ya kimapenzi na Jasmine.
Hilo lilikuwa ni dogo kati ya yale ambayo nilikuwa nikiyawaza. Jambo kubwa ambalo ndilo liliniumiza kichwa hasa ni suala la ujauzito wa Jasmine. Suala la mimi kutembea na Jasmine niliona ningeweza kulizima endapo moto wa mama Careen ungewaka lakini suala la ujauzito mh!
Hili lilikuwa kubwa na nilishindwa kulibeba kabisa. Nilikuwa nikiliona kabisa jahazi likienda mrama na mimi kama nahodha nilikuwa sina uwezo wa kulinusuru jahazi hili katika gharika hili kubwa.
“Lakini haya yote ameyataka yeye mwenyewe mama Careen. Mwanamke ni mshari balaa. Hajui hata kuibembeleza na kuitunza ndoa. Kila siku ni ugomvi tu ambao hauna hata sababu ya msingi”. Niliwaza siku moja nikiwa chumbani wakati mama Careen akiwa nje uwanjani akicheza na Careen.
“Furaha ya ndoa yetu ilipotea miaka mingi nyuma. Siku za mwanzo za ndoa yetu ndipo nilipolifurahia penzi langu na mama Careen lakini baada ya hapo, ndoa yetu ilibadilika na kuwa chungu kabisa”. Niliendelea kuumizwa na mawazo kichwani mwangu.
“Na kila nikijaribu kumsogeza jirani mke wangu ili tuitengeneze ndoa yetu, yeye alikuwa mbali nami zaidi ya kuzidisha ushari wake. Hajali kabisa ustawi wa ndoa yake”. Nilizidi kutiririkwa na mawazo lukuki mengine yakiwa ni maswali ambayo yalikosa majibu.
Hatimaye taratibu machozi ya uchungu yakaanza kuniporomoka. Niliumia kwa sababu mimi na mke wangu tulikuwa tumeshindwa kuitengeneza ndoa yetu na hatimaye ilikuwa ikielekea katika misukosuko.
Baadaye usingizi ukanipitia na kunisahaulisha yale yote ambayo yalikuwa yakiniliza. Nilianza kuota ndoto nzuri na tamutamu juu yangu na Jasmine. Niliota tukiyafurahia maisha pamoja.
***********
Siku moja mama Careen akawa amepata mgeni. Mgeni huyu alikuwa ni mwanamke. Mwanamke huyu alikuwa ni mzuri na mrembo sana.
“Mh! Mdogo wangu wewe una mambo makubwa sana”. Mama Careen aliongea pindi walipokuwa wamekaa sebuleni.
“Kwa nini waongea hivyo dada?”. Mgeni aliuliza.
“Yaani tumepoteana miaka mingi sana hatuonani. Halafu jambo la kushangaza eti sote twaishi katika jiji hilihili la Kano”. Mama Careen aliongea.
“Nisamehe dada yangu. Ni maisha tu ndiyo yamesababisha yote haya”. Mgeni aliongea.
“Wala hata usiyasingizie maisha. Maisha ndiyo yakufanye ushindwe hata kunijulia hali nduguyo?”. Mama Careen aliendelea kuongea kwa kutoa lawama kwa mgeni ambaye alikuwa ni mdogo wake.
“Halafu naona mambo yako si mabaya. Yaani safari hii umeamua kabisa kutundikwa mpaka mimba. Mbona siyaamini macho yangu!”. Mama Careen aliongea kwa mshangao huku akilitazama tumbo la mdogo wake ambalo kwa sasa lilikuwa kubwa.
“Dada yangu. Mimi safari hii ninataka kuolewa. Nimepata mchumba ambaye ananijali na yuko tayari kabisa kunioa”. Mgeni aliongea.
“Ha ha ha ha haaaaaaaa! Yaani Jasmine wewe leo hii unataka kuolewa?. Mh! Haya bwana. Je, na biashara yako ya ukahaba unamwachia nani?”. Mama Careen aliuliza.
“Ile biashara nilikwishaiacha dada. Huyu mchumba wangu ndiye ambaye amenibadilisha na kunifanya niiache biashara hii kabisa. Nimeamua kubadilika kabisa na kuanza maisha mapya dada yangu”. Mgeni aliongea huku machozi yakimlengalenga.
“Yaani leo ndiyo unatambua kwamba biashara uliyokuwa ukiifanya ilikuwa ni mbaya. Je, wakati mimi nakukanya juu ya biashara ile mbona hata ulikuwa hunisikilizi?”. Mama Careen aliongea.
“Nisamehe dada yangu. Na ndiyo maana leo hii waniona niko hapa mbele yako niki

wa nimebadilika kabisa. Mimi si yule Jasmine wa zamani, kahaba. Mimi ni Jasmine mpya. Naomba unisamehe kwa yote ambayo nilikukosea dada yangu mpenzi”. Jasmine aliong ea huku akiporomokwa na machozi.
“Haya nimekusamehe mdogo wangu”. Mama Careen aliongea huku akimkumbatia Jasmine.
Ghafla simu ya Jasmine iliita.
“Hallo! Baby”. Jasmine aliongea mara baada ya kubonya kitufe cha kupokelea simu.
“Uko wapi? Mbona nimefika hapa kwako sijakuona?”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Nisamehe mpenzi wangu. Leo nimeenda kumtembelea dada yangu yule ambaye nilikwambia”. Jasmine aliongea.
“Sasa mbona hukunitaarifu?”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Naomba unisamehe mume wangu. Mimi nilifikiri kwamba hutakuja nyumbani kwa wakati huu ndiyo maana sikukutaarifu. Nisamehe sana mpenzi wangu”. Jasmine aliongea.
“Ok, nimekusamehe”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Halafu mpenzi, nilipenda jioni ya leo twende pamoja huku kwa dada yangu ili nikutambulishe kwani dada ana hamu kubwa sana ya kukuona”.
“Ooooh! Hilo wala usijali. Nitajaribu kuziweka sawa ratiba zangu ili kusiwe na usumbufu wowote”. Upande wa pili wa simu uliongea.
“Ahsante sana mpenzi”. Jasmine alishukuru.
“Ok, usijali”. Upande wa pili wa simu uliongea.
Baada ya Jasmine kuongea na ile simu, basi maongezi yake na mama Careen yakaendelea. Wakaendelea kupeana michapo ya hapa na pale ambayo iliwaletea furaha tele katika nyoyo zao.
“Ndiyo hivyo dada. Hakika utampenda kwani ni mwanaume mzuri, mtanashati, anayejali na ambaye anajua nini maana ya pendo la dhati”. Jasmine aliongea.
“Mh! Haya bwana. Waswahili walisemamtu chake . Tutaona hiyo jioni kama hizo sifa unazompamba kweli anazo?”. Mama Careen aliongea huku akicheka.
************
Tukutane katika sehemu ya 09
(sehemu ya mwisho je itakuaje usikose)


  🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO




No comments: