SMULIZI: HOUSE GIRL WA KITANGA 20
SMULIZI: HOUSE GIRL WA KITANGA
MTUNZI : KIZARO MWAKOBA
SEHEMU 20
ILIPOISHIA
“Hivi unajua kama nimerudi mapema kwaajili yako?” alieleza kaka Imran kwa hasira kidogo.
“Basi sawa nakusikiliza” nilizungumza na kuketi tena kwenye kochi.
“Haya njoo ukae hapa” alizungumza kaka Imran huku akinioneshea kuketi kwenye paja lake.
Nilivuta pumzi na kuziachia kwanguvu, nilitaka kuinuka na kwenda kuketi pale kwenye paja lake lakini moyo wangu ulisita na kukumbuka ahadi yangu niliyokuwa nimejiwekea ya kutokuwakaribia wanaume wa ndani mle.
ITAENDELEA…
“Hapana kaka Imran, siwezi kukaa hapo” nikazungumza kwa sauti ya wasiwasi.
“Hivi huo woga umetokea wapi, mbona zamani ulikuwa unakubali?” alihoji kaka Imran kwa mshangao.
“Sio hivyo kaka Imran, unajua hata mama akinikuta hapo itakuwa sio vizuri” nilizungumza kwa msisitizo.
“Duh kweli mabadiliko! Haya na nguo nilizokuletea mbona huvai?”
“Sipendi kumuudhi mama” nikasema kwa upole.
“Mama yako gani, Bi Fatma?”
“Ndio, nilipovaa zinle nguo ulizoniletea mwanzo, mama alikasirika sana” nilieleza.
“Ah mbona hayo yaliisha na mother aliruhusu uvae nguo yoyote ile” kaka Imran akanieleza.
Pasipo kuzungumza neon lolote nilijiinua kutoka kwenye kochi na kuelekea jikoni tayari kwa kuanza maandalizi ya chakula cha jioni.
Kaka Imran akabaki ameduwaa akinikodolea macho huku akiwa haamini kile nilichokuwa nimekionesha. Ndio, hakutegemea kabisa kama na mimi ningeweza kuwa ni mwanamke mwenye msimamo kama aliouona. Najua hata wewe ndugu msomaji ulifikia hatua ya kunidharau na kuniita kichehe, sijui Malaya, mara maharage ya Mbeya wengine wakasema sijui nini! Maneno kibao. Kwahiyo naomba nisilaumiwe kwa misimamoyangu.
***
Miongoni mwa watu ambao walikuwa wakiteseka juu yangu alikuwa ni pamoja na baba mwenye nyumba mzee Sekiza. Mzeeyule ndiye aliyekuwa ananipa mtihani wa hali ya juu. Mitihani aliyokuwa ananipa kwakweli ilikuwa ni zaidi ya mitihani ya chuo kikuu, halafu mwanafunzi mwenyewe nilikuwa na elimu ya darasa la saba.
Nikiwa peke yangu ndani ya nyumba ile baada ya Fadhili na kaka Imranmn kuondoa, Mawazo yangu yote yalikuwa kwa Endrus kijana niliyekutana naye kule mgahawani kwa dada Bupe. Pamoja na kwamba Fadhili alikuwa amenipinga kwenda kwa dada Bupe lakini bado nilihii kumpenda Endrus. Naomba nisilaumiwe jamani, nimeamua kuachana na wanaume wote wa ndani, hakuna cha Fadhili wala nani.
Nikiwa nimesimama pembeni ya jiko la gesi nikigeuza geuza mboga iliyokuwa jikoni, ghafla nikashituliwa na mikono ya mtu aliyekua anajaribu kunishika kiuno kwa nyuma.
Ndugu msomaji, mar azote nilipokuwa nikiguswa nilikuwa najiuliza mara mbilimbili kuwa anaweza kuwa ni nani? Lakini siku hiyo ni miongoni mwa siku ambazo sitoweza kuja kuzisahau maishani mwangu. Nilinga’ta mdomo wangu wa chini kwa hasira kisha nikageuka na mwiko wa kukorogea mboga ambao ulikuwa mkononi na kumtandika kwa nguvu sana mtu aliyekuwa amenishika kiuno. Nikasikia mtu anaguna Mnh!
Mungu wangu! Sikuweza kuamini baada ya kugeuka na kubaini nilikuwa nimempiga baba mwiko wa pua.
“Tumu umeniua!” baba alilalamika huku ameinama na viganja vya mikono yake vikiwa vimeshikilia pua yake. Alikuwa akikagua kagua kuona kama ilikuwa ikitoa damu masikini baba wawatu.
“Ooh pole baba sikujua kama ni wewe!” nikazungumza kwa kuhamaki huku nikisimama kwa wasiwasi uliochanganyikana na woga.
“Mungu wangu, kwanini usingenipiga sehemu nyingine Tumu? Yani umenilenga katikati kwenye pua” alizungumza baba huku akisimama na kusogelea kioo cha ukutani kilichokuwepo pale jikoni.
Jamani nyie mwenzenu nilikuwa nimemtengeneza baba kisawasawa kwenye sura yake. Yani ile pua iliumuka utafikiri ilikuwa imetiwa hamira na kuwa na muonekano kama wa kikombe cha chai.
“Jamani Mwantumu, kwanini umenifanya hivi?” baba alilalama baada ya kuona pua yake jinsi ilivyopamba sura yake. Alikuwa anaonekana kama katuni hivi.
“Nisamehe baba ni bahati mbaya” nikazungumza kwa kujihami.
“Bahati mbaya wakati umevuta mwiko kwanguvu zote kabisa!” baba alizungumza kwa kulalamika masikini ya mungu.
“Sikujua kama ni wewe baba”
“Inamaana kuna mtu mwingine humu ndani ambaye anakushika hivi?” baba alihoji kwa umakini.
“Hakuna mtu yoyote anayeweza kunigusa na ndiyomaana nikahamaki na kukupiga bahati mbaya” nikajieleza.
“Inamaana kama ungejua ni mimi usingenipiga?” baba akahoji swali la mtego.
Nikaitika kwa kichwa kuwa nisingempiga. Nikamuona akiachia tabasamu la matumaini.
“Kama ndio hivyo basi nimekusamehe” alizungumza baba huku akivuta hatua kutoka jikoni.
“Ndio ukome!” nilizungumza kwa sauti ya chini huku nikicheka wakati baba alipokuwa anatoka jikoni.
Niliuinua mwiko wangu juu na kuuangalia kwa kujidai huku nikiachia tabasamu la matumaini.
“Kumbe hii ndio dawa yao! Nitatembea na mwiko wangu kila nitakapokuwa” nilizungumza huku nikiangua kicheko kwa kuziba mdomo nisije kusikiwa na baba akagundua kama nilikuwa namcheka yeye.
Nikiwa naendelea na shughuli zangu za upishi kule jikoni, nikasikia sauti ya baba ikiniita. Nikanyamaza na kujifanya kama vile sikuwa nimesikia wito ule.
“We Mwantumu!” baba aliita tena, safari hiyo aliita kwa sauti kubwa zaidi.
“Abee..” sikuwa na namna ikabidi niitike.
“Njoo mara moja?” baba aliamuru.
Nilisita kidogo lakini nikajipa moyo na kuutazama mwiko wangu kwa skund kadhaa kisha nikauweka chini.
“Nisubiri hapa mtoto wangu nakuja” nilizungumza wakati naweka mwiko ule chini.
Nikavuta hatua kuelekea kule sittingroom alipokuwa ameketi baba.
“Abee baba” nikaitika kwa heshima mara tu nilipofika sebleni.
“Umemaliza kupika?” baba alihoji
“Bado sijamaliza lakini ndio namalizia baba”
“Mbona sikuhizi hauvai zile nguo zako nzuri?” baba alihoji huku akitabasamu na kusababisha ile pua yake niliyoipiga mwiko kuzidi kuonekana kubwa.
“Nguo gani baba?” nikahoji na kujifanya sielewi alichokuwa anakizungumza.
“Zile zilizokupendeza juzi” baba alieleza.
“zile fupi?”
“Ewaaa!, mbona hujavaa tena nikakuona?”
“Sina nyingine baba” nikajaribu kuongopa huku nikimtazama baba kwa jicho la kuibia kwenye ile pua yake iliyokuwa imefutuka kwa kupigwa mwiko na binti wa kitanga. Sijui hata mke wake angemueleza nini.
“Huna nyingine? Sasa mbona husemi” baba alizungumza.
Nilikaa kimya huku ndani ya moyo wangu nikiomba amalize haraka kuongea ili niondoke na kumuacha mwenyewe. Siku hiyo nilikuwa makini sana na kujitahidi kutomkaribia hata kidogo.
“Hebu nenda chumbani kwangu ukaniletee briefcase yangu” baba aliagaza.
Maagizo yale niliyokuwa nimepewa na baba yalinifanya nikumbuke
siku ambayo kaka Imran alinituma niende chumbani mwake kumtafutia kituhalafu matokeo yake akanifuata na kutaka kunanihii.
“Tumu si nimekutuma au haujasikia” baba akahoji kwa sauti kidogo baada ya kuniona bado nimesiamama utafikiri sikuwa nimesikia agizo lake.
Nilitamani kukataa agizo lile lakini sikuwa na sababu ya msingi ambayo ningeitoa na kunitetea. Ikabidi nigeuke na kuelekea chumbani kwa baba kwa mwendo wa haraka huku nikiwa nimejawa na wasiwasi. Nilipoukaribia mlango wa chumbani nikasita kuingia. Nikakumbuka kituambacho kilinipa nguvu. Niliacha kufungua mlango na kuelekea jikoni kitendo ambacho kilimshangaza baba.
“Wewe imekuwaje tena” baba alihoji baada ya kuniona narudi na kuelekea jikoni.
“Naleta baba” nikajibu huku nikiingia jikoni.
Moja kwa moja nilinyoosha hadi pale nilipokuwa nimeweka mwiko wa mboga na kuuchukua.
“Naomba nisindikize mdogo wangu” nilizungumza huku nikiuficha ule mwiko kwenye kanga niliyokuwa nimejitanda kichwani.
Nilitoka haraka jikoni na kuelekea chumbani kwa baba kuchkua hiyo friefcase niliyokuwa nimeagizwa. Safari hii nilikuwa najiamini kwasababu nilikuwa nimekamatia mwiko wangu kisawasawa.
“Akijipendekeza tu atajuta kuzaliwa” nikazungumza kwa kujiamini huku nikikamata kitasa cha mlango na kuzama chumbani.
Wakati wote huo baba alikuwa akinikodolea macho nilivyokuwa nikiingia na kutoka. Hakuwa anaelewa mipango yangu siku hiyo. Maumivu ya pua yaliyotokana na kupigwa na mwiko yaliendelea kumfanya awe kama zezeta.
Tofauti kabisa na ambavyo nilikuwa nimetarajia. Niliingia chumbani kwa baba na kuchukua briefcase kisha nikafanikiwa kutoka salama pasipo kubugudhiwa na mtu yeyote.
Nilirejea sittingroom nikiwa nimekamatia vyema briefcase ya baba na kwenye kwapa langu la kushoto nimeubana vizuri mwiko wa mboga. Nilipotokelezea tu, pua ya baba ikanikaribisha, ilikuwa imezidi kuvimba na kuonekana kama pulizo. Masikini ya mungu nikamuonea huruma kwa kiasi fulani baba wawatu. Nilifika na kumkabidhi ile briefcase yake.
“Haya asante mtoto mzuri” baba alizungumza huku akipokea.
Baada ya kumkabidhi nikataka kuondoka kuelekea jikoni kwaajili ya kuendelea na maandalizi ya chakula cha jioni.
“Unakwenda wapi sasa?” baba alinizuia.
“Nakwenda kumalizia kupika”
“Aah kupika nini bwana njoo kwanza. Utapika hata baadae” alizungumza baba huku akifungua briefcase yake.
Nikasimama kama vile nilikuwa namsikiliza amalize kuzungumza niondoke zangu. Lakinimacho yangu yalikuwa yamekodoka kwenye ile briefcase aliyokuwa anaifungua. Mnh! Sikuweza kuamini kile ambacho nilikuwa nimekiona.
“Haya kazi kwako sasa” baba alizungumza huku akitoa nguo kutoka kwenye briefcase ile.
Sikuweza kuamini maho yangu, lakini hicho ndicho kilichotokea. Kwakuwa alikuwa ni baba yangu hivyo sikuona sababu ya kukataa zawaidi ile, nilipokea kwa shukurani kibao. Yani nyie pamoja na kupigwa na mwiko baba wa watu lakini bado alinipa zawadi, Mnh!
“Asante sana baba” nikatoa shukurani za dhati huku nikiachia tabasamu laini.
“Haya mtoto mzuri ndenda ukavae sasa nikuone” baba alizungumza kwa sauti ya upendo. Nilipokea viwalo vile na kuelekea chumbani kwangu huku nikiwa nimejawa na furaha ndani ya moyo wangu.
Nilijikuta macho yakinitoka baada yakuzikunjua nguo zile, zilikuwa ni kama zile ambazo alikuwa ananinunulia kaka Imran.
“Mbona kila mtu ananiletea nguo za hivi! Au ndio swaga za mjini hizi?” nikajiuliza huku nimeketi kitandani. Alikuwa ameniletea miniskate na blauzi pamoja nguo za ndani kama zile alizokuwa ameniletea kaka Imran zenye Kamba kwa nyuma.
“Ngoja leo nitoe ushamba, hizi nguo inawezekana ndio mpango mzima” mtoto wa kike nikasogea karibu na kioo na kuanza kusaula mavazi yangu na kujivisha zile nguo ambazo mwenyewe nilikuwa nikihisi ni nguo za kijanja kwa watoto wa mjini.
Naam! Nilikuwa nimetokelezea hasaa na nikajikubali mwenyewe. Nakumbuka zilikuwa ni kimini cha jeans kilichokuwa kifupi kilichoishia juu ya magoti, na kiblauzi cha rangi ya orange ambacho kilikuwa na kitambaa lainii kilichoweza kuonesha alama za sidiria yangu nyeusi niliyokuwa nimeivaa kwa ndani huku mikono yake ilikuwa ni ile ya kukata na kifuani kameacha nafasi kiasi na kupelekea mashina ya madafu yangu kuonekana. Nikajigeuza geuza pale kwenye kioo mara mbilimbili huku nikijichezesha chezesha pekeyangu.
“Hapa nakwambia Endrus akiniona lazima achanganyikiwe” nikajizungumzisha mwenyewe.
Nilipojiona kuwa nilikuwa sawa na nguo zimenikaa vyema nilivuta hatua kuelekea sebleni ambako baba alikuwa akinisubiri kwa hamu.
“Woow! Wonderfull! “Baba alishindwa kuzuia hisiazake mara tua aliponiona nikitokelezea.
Itaendelea
🔞WAKUBWA TU:TAZAMA VIDEO ZA WAKUBWA LIVE UJIONEE STAILI KALI ZA KUMFIKISHA KILELENI MPENZI WAKO
No comments: