MREMBO WA KIJIJI. SEHEMU YA NNE-04





MREMBO WA KIJIJI.


       SEHEMU YA NNE-04

Alipagawa mrembo Chaudele baada kuitafuta barua ile ya vitisho iliyotoka kwa Chitemo.

"Ikowapi barua?" Alijiuliza huku akiendelea kuitafuta wakati huo upande wa pili nyumbani kwa mwenyekiti wa kijiji alionekana mzee J akibisha hodi, bahati nzuri alimkuta mwenyekiti akijiandaa kuelekea msibani.
"Habari yako ndugu mwenyekiti" alitoa salamu mzee J, mwenyekiti aliposikia sauti hiyo alisitisha zoezi la kufunga mlango ikabidi ageuke ili atazame nyuma yake ajue ni nani aliyemsalimia. Ni mzee J.

"Anhaa kwema tu sijui wewe hali yako" Alijibu mwenyekiti.

"Niko salama pia. Aahm! Ndugu mwenyekiti. Nina maongezi na wewe ya muda mfupi tu na wala haihitaji kunipa kiti, naweza kuongea nikiwa nimesimama " Alisema  Mzee J.

"Enhee leta maneno, maana nina haraka kidogo nikitoka msibani natakiwa kwenda shamba kukagulia mazao yangu" Alisema mwenyekiti huku akionekana kukaa mkao wa kumsikiliza mzee J.  Hapo mzee J alishusha pumzi kidogo kisha akasema "Naomba ukamwambie mzee Nhomo kuwa mimi sio mtu wa kuchezewa?  Mwambie kama hakutaka binti yake aolewe kwa nini alipokea kishika uchumba? Mueleze sihitaji anirejeshee posa yangu ila tunamtaka binti yake la sivyo atakuja kukiona cha mtema kuni" Aliongea mzee J kwa msisitizo.   Mwenyekiti alishtuka  na maneno hayo.

"Kwanini mzee mwenzangu? Na mbona kama mmefika mbali kiasi hicho?.." Aliuliza mwenyekiti kwa taharuki kubwa. Lakini mzee J hakujibu neno lolote zaidi aliondoka zake huku akionyesha kujawa na jazba. Jambo hilo lilimshangaza sana mwenyekiti   hakuwa na chakusema zaidi ya kumsindikiza kwa macho mzee J ambaye alionekana kuzipiga hatua za haraka haraka kuondoka nyumbani kwa mwenyekiti.  Mwisho wa yote mwenyekiti alishusha pumzi na kisha kujisemea "Mafahari wawili wapiganapo siku zote ziumiazo ni nyasi, acha waonyeshane umwamba sababu Nhomo naye sio wa kubenza " Alitabasamu baada kujisemea manano hayo  kisha akafunga mlango wa nyumba yake tayari  kwa safari ya kuelekea msibani.

  Kwingineko lilionekana kundi la wasichana wakielekea kisimani, katika kundi hilo alikuwemo Pendo ambaye hapo awali alikuwa na urafiki wa karibu mno na Mrembo Chaudele. "Pendo mbona Chaudele hauko naye?"  Moja ya wasichana aliyekuwemo ndani ya kundi hilo alimuuliza Pemdo. Swali hilo liliweza kuzua mjadala wa aina yake, kila mmoja akawa anazungumza lake. Lakini mwishowe Pendo mwenyewe alijibu "Nafikiri kila mmoja anapenda kuishi, ukweli ni kwamba mimi na Chaudele urafiki tumeua" hayo maneno yaliwashtua   wasichana hao.

Mwingine akauliza "Sababu? Unamaanisha Chaudele anataka kukuua?"

"Hapana sina maana hiyo. Bila shaka  mnafahamu kuwa Chitemo anamtaka Chaudele, na juzi tu Chaudele aliletewa barua kutoka kwa Chitemo ikimsihi kwamba anampenda napia atawafanya kitu kibaya vijana wa kijiji hiki watakao mtongoza. Mimi nikamshauri, barua hiyo ya vitisho tuipeleke kwa mwenyikiti ili  ajue cha kufanya. Ajabu usiku huo huo mzee J, baba yake Chitemo akani...." Kabla Pendo hajamalizia alichotaka kukisema, mara ghafla alitokea mzee J.  Alimuona peke yake tu pasipo wale wasichana aliokuwa nao kumuona. "Itakughalimu nakwambia" Alisema  mzee J ikimuasa Pendo.

Pendo alishtuka akaogopa kuendelea kusema alichotaka kukisema ilihali muda huo huo mzee J alipotea ikisalia vumbi ikitimka, vumbi ambayo nayo haikudumu.  Wale wasichana aliokuwa nao Pendo walitaharuki kumuona mwenzao amepigwa na bumbuwazi huku macho yake yakiwa yamekodelea sehemu ile iliyotimka vumbi baada mzee J kupotea.

"Pendo! Ndio nini sasa?" Alihoji moja ya wale mabinti huku akimgusa  kwa kumtingisha.

"Eeh eeh hapana twendeni twendeni" Alishtuka na kusema  huku akizipiga hatua za haraka haraka kuongoza njia ya kuelekea kisimani. Mabinti hao nao walikazana wakati huo wasimuelewe Pendo, na mwishowe walichota maji kisha wakarejea nyumbani ilihali mioyo yao ikijaa sintofahamu baina ya Pendo na rafiki yake  wa karibu mrembo Chaudele.  Wakati hayo yanajili huko, kwingineko Pili alionekana akizipiga hatua kuelekea nyumbani kwakina Chitemo. Binti huyo ambaye alikuwa mpenzi wa Chitemo, siku hiyo aliamuwa kufika nyumbani kwa kina Chitemo kujua mstakibali wake wa kimapenzi na Chitemo, moyo wa Pili ulionekana kutokukubaliana na maamuzi ya kukurupuka aliyo chukuwa Chitemo sikuile. Hivyo aliamini huwenda labda  siku ile amtamkie mabaya hakuwa sawa, yamkini alichanganywa na mambo mbali mbali ya kimaisha.

"Hodi hodi.." Pili alibisha hodi baada kuikaribia nyumba yakina Chitemo.

"Karibuuuu" Ilisikika sauti ya mama Chitemo akimkaribisha, punde si punde alitoka ndani.

"Shikamooo mama" Pili alimsalimia mama Chitemo huku akikunja magoti kidogo ishara ya kumuheshimu. Mama Chitemo hakuitikia salamu ya ile,  alimfyonya na kisha akasema "Unamuamkia nani mwanahidhaya mkubwa wewe. Hivi wewe binti mbona unamganda  mwanangu kama ruba?  Eeh amekupa nini hasa kiasi kwamba unashindwa  kumuacha. Alishakutamkia hakutaki wala hakupendi lakini bado tu unaendelea kumfuatafuata. Kwanini lakini hutaki kuelewa? Sasa basi naomba unisikilize tena nisikilize kwa umakini Pili. Punguza ushamba wa mapenzi, ukiachwa achika, Chitemo hakutaki anayempenda ni mmoja tu hapa kijijini, simwingine ni Chaudele na sio wewe mwenye chogo kubwa kama mpini wa shoka" Aling'aka mama Chitemo. Maneno hayo aliyokuwa akiyaongea yaliweza kumchoma moyoni Pili kitendo kilichomfanya kudondosha machozi huku akikukumbuka ni namna gani alivyokuwa akiwakataa wanaume waliokuwa wakimuhitaji ndani ya kijiji hicho  na kijiji Jirani yote ikiwa shauri ya kijana Chitemo aliyemuahidi kumuoa.

  "Mama, tambua mwanao  aliniahidi kunioa. Iweje aivunje ahadi yetu kisa binti mgeni aliyekuja juzi juzi tu? Haya nitaificha wapi sura yangu mimi? Wakati nilikataa wanaume kisa mwanao, sikutaka kumsaliti wala kuvunja ahadi niliyoweka moyoni mwangu, lakini leo hii kisa Chaudele.. Chitemo anavunja ahadi?.." Alisema Pili huku akiangua kilio mbele ya mama Chitemo. Kilio na majonzi yake katu hayakumfanya mama Chitemo kumuonea huruma, zaidi aliongeza kusema "Nadhani unajua ni wapi ulipo msiba, hivyo basi nenda kalilie kule na sio kuniletea uchoro mimi"

  "Potea nyumbani kwangu mshenzi mkubwa, Kila muda Chitemo Chitemo, wnaume wingine huwaoni?" Aliongeza kusema mama Chitemo.

 "Mama mbona jasho?" Aliuliza Chitemo, hiyo ni mara baada kumuona mama yake akitokwa na kijasho chembamba kwa usoni. Alikuwa ametoka shamba.

 "Amna we acha tu mwanangu, nimemtoa mbio Pili alikuja kukuona" Alijibu mama Chitemo.

Chitemo baada kusikia jibu hilo kutoka kwa mama yake alishusha jembe chini na panga halafu akasema "Doh huyu Pili anataka nini lakini? Nilishamwambia simtaki ila bado hataki kunielewa. Lakini pia mama mbona hamtaki kuniambia maendeleo ya barua tuliyopeleka kwa mzee Nhomo, inamaana mpaka sasa majibu bado hajaleta? Na kama tayari tunangoja nini kwenda kuchukua mke?"

"Mwanangu maswali hayo msubiri umuuluze baba yako bwana, mimi sijui chochote" Mama Chitemo  alimjibu  kijana wake baada kaonekana kutaka kufahamu mstakibali wa barua ya kishika  uchumba waliyopeleka kwa mzee Nhomo. Hakika alikuwa na uchu mithili ya fisi aliyeona mzoga.

Msibani, mwenyekiti alipofika tu. Jambo la kwanza alimtafuta mzee Nhomo ili ampashe habari alizonazo kutoka kwa mzee J kabla hajasahau. Hatimaye alimuona, alimuita kando.

"Ndio habari yako bwana" Mwenyekiti alimsabahi kwanza mzee Nhomo kwa tabasamu la aina yake.

"Njema tu mzee mwenzangu" Aliitikia mzee Nhomo ilihali uso wake ukionyesha shauku ya kutaka kujua dhamira ya mwenyekiti kumuita faragha.

"Aah salama tu, nina ujumbe wako"

"Ujumbe? Ujumbe gani tena?" Aliuliza mzee Nhomo.

"Kutoka kwa mzee J" Alijibu mwenyekiti kwa utashi zaidi. Hapo mzee Nhomo alishtuka baada kusikia kuwa ujumbe huo alionao mwenyekiti umetoka kwa mzee J. Alishusha pumzi ndefu kisha akasema "Haya nipe maneno, anasemaje J!"

"Bwanaaa mzee J anasema kwamba yeye sio mtu wa kuchezewa, anadai kuwa kama hukutaka binti yako aolewe mbona ulipokea posa?  vile vile amesema hataki mmrejeshee posa yake ila anachotaka yeye ni mke la sivyo utakiona cha mtema kuni" Alieleza mwemhekiti. Mzee Nhomo alitaharuki kusikia maneno hayo ya mzee J aliyomtuma mwenyekiti  ili amfikishie.

"Ahahaha hahahaha" Aliangua kicheko cha madaha  kisha akasema "Mwenyekiti ahsante sana kwa taarifa yako, kamwambie imemfikia mlengwa ila na wewe na kutuma kwake. Tena naomba unisikilize kwa umakini sana. Nenda kamwambie hivi mzee Nhomo amesema kuwa siku zote  Ng'ombe hutikisa mkia na sio mkia kumtikisa Ng'ombe"

"Mmh una manisha nini mzee Nhomo?" Mwenyekiti alimuuliza akistaajabishwa na kauli hiyo. Kwa mara nyingine tena mzee Nhomo aliangua kicheko, akicheka sana halafu akasema "Wewe ni mtu mzima, siku zote chuma huliwa na nini?"

"Aah kutu" Alijibu mwenyekiti.

"Je, chuma kwa chuma huzuka nini?"

"Cheche" Akianza kwa tabasamu pana alijibu mwenyekiti samba na kumaliza kwa kicheko.
 
"Naam! Vizuri kama umelitambua hilo, sikufichi mwenyekiti mzee J anataka kukanyaga ardhi ya kifo. Binti yangu haolewi na Nguchiro wake, na posa yao nimeshaiywea gongo. Nenda kampe ujumbe nilio kwambia"

Mmmh! VITA HIYO. me simo wenye timu mjigawe mapema. Timu #Nhomo na Tim #J. HILI NI BALAA KIJIJI CHA NDAULAIKE 😋
   Vipi jioni nilete sehemu ya TANO? kama upo tayari shea mara nyingi pia usisahau kulike page Yangu. Ili usipitwe na kigongo hiki.



No comments: