MREMBO WA KIJIJI. SEHEMU YA TATU-03




MREMBO WA KIJIJI.

      SEHEMU YA TATU-03

"Chaudele unahabari kama Ezlom kafariki?.." Aliuliza Pendo rafiki yake Chaudele. Taarifa hiyo ilimshtua sana Chaudele, kwa mshangao akauliza "Ezlom huyu huyu niliyemtuma jana akamwambie Chitemo kuwa simtaki? "

"Ndio. Nasikia jana jioni alikuwa mzima kabisa, baadhi ya watu wanasema mzee J ndio kamuua. Kwa sababu toka zamani   J baba  alikuwa akishutumiwa kuwa ni mchawi. Halafu ,jana hiyo hiyo baada Ezlom kumwambia Chitemo vile ulivyomtuma. Chitemo ikatishia kupiga ila watu waliwaamulia akawa ameondoka. Leo hii taarifa inasemekana Ezlom hatupo naye" Alisema Pendo kwa sauti ya majonzi. Chaudele alishusha pumzi kisha akajibu "Basi kama ni hivyo kazi ninayo, unajua kwanini? Baba alipokea kishika uchumba kala. Sasa sijui itakuaje na mimi sitaki kuolewa katika familia ile, sio mimi tu bali hata mama na baba hawataki jambo hilo"

"Pole sana shoga yangu, najua uzuri wako ndio unakuponza" Aliongeza kusema Pendo. Na muda huo huo wakati wanazumngumzia kifo cha  Ezlom, mara ghafla alikuja kijana mdogo kwa baiskeli alipofika alimpa karatasi Chaudele. Kwa taharuki Chaudele akauliza "Ni nini hii?.."

  "Nimetumwa na Chitemo" Alijibu kijana huyo. Chaudele alishtuka, akamgeuki Pendo halafu akasema "Pendo hivi huyu Chitemo ananitakia nini?.."

"Sijui shoga yangu lakini fungua uisome tuone barua hiyo inaujumbe gani"

"Sawa " Alikubali Chaudele kisha akaifungua barua hiyo na kuisoma "Chaudele wewe ni mchumba wangu, sitopenda  kumuona kijana  yoyote hapa kijiji akikutongoza. Kwani kufanya hivyo ni kuhatarisha maisha yake. Nimeanza na kibaraka uliyemtuma jana, sasa watafuata wengine utakao watuma. Jichunge sana usije kuyaghalimu maisha ya vijana hapa kijijini. Ni wako nikupendae Chitemo, nikutakia siku njema" Chaudele alishtuka baada kusoma maneno hayo yaliandikwa kwenye hiyo barua. Ghafla mapigo ya moyo yakamuenda mbio.

Kitendo hicho kilimshtua pia Pendo, kwa sintofahamu akamuuliza "Mbona unashtuka? " Chaudele alishusha pumzi kwanza halafu akajibu "Chitemo anatafuta ubaya, na hata kifo cha Ezlom yeye ndio sababu. Shika hii barua usome mwenyewe" Upesi alimkabidhi Pendo barua hiyo kutoka kwa Chitemo. Pendo aliisoma barua kwa hisia kali, alipomaliza akasema. "Sawa, nafikiri huyu mtu atakuwa anacheza na serikali. Hii barua iweke  mbali ili isipotee baada ya msiba kumalizika tutampelekea mwenyekiti aisome"

 Chaudele alikubaliana na ushauri wa rafiki yake kipenzi. Hivyo aliificha barua hiyo ya Chitemo sehemu ambayo mtu yoyote hawezi kuiona, lakini pia jambo hilo Chaudele hakutaka kumfikishia baba yake kwani alifikiria na kuona kuwa kufanya hivyo huwenda ikamghalimu baba yake kama barua ilivyoelezwa achilia mbali suala hilo lakini pia Chaudele alitambua baba yake ni mkorofi sana  kiasi  kwamba anaweza kuanzisha ugomvi baina ya pande hizo mbili mzee Nhomo na mzee J.
   Siku hiyo hiyo hiyo, usiku kabla hapajakucha. Pendo rafiki yake Chaudele aliingiliwa na mtu chumbani kwake, mtu huyo Pendo hakuweza kumtambua kwani chumbani kwake palikuwa na giza.

"Pendo"  Aliita mtu huyo, sauti hiyo ilimshtua  na kugundua kuwa mtu huyo aliyeingia chumbani ni mzee J, sababu aliitambua vyema sauti ya mzee huyo. Hakuitika, alitetemeka kwa woga sambamba na kutokwa kijasho chembamba.

Mzee J akaongeza kusema "Unajua ni rahisi sana Ng'ombe kutikisa mkia kuliko mkia kumtikisa Ng'ombe. Hivyo basi kile mnachokipanga wewe na rafiki yako, angalia yasije yakakutokea puani. Kijiji chote hiki kipo kiganjani mwangu, jambo lolote linalo famyika popote pale huwa nalipata kwa haraka iwezekanavyo. Chunga sana tusije kuonana wabaya. Na ole wako umwambie mtu yoyote jambo hili. Nitakupoteza" Alipokwisha kusema hayo mzee J alipotea. 

Pendo alitaharuki akapiga kelele "Mama nakufaaa "

 Punde si punde  mama yake aliingia chumbani akamkuta binti yake akiwa amekaa kutandani huku akihaha mithili ya mwanariadha aliyekimbiza upepo.

"Pendo kulikoni, umekumbwa na nini?"  Aliuliza mama Pendo lakini kabla Pendo hajamwambia mama yake kinacho msibu, maneno yale ya mzee J yalijirudia kichwani mwake "Na ule wako umwambie mtu yoyote " Maneno hayo yalimuogopesha  sana Pendo, upesi aliamuwa kudanganya "Hapana mama wala hamna kitu, ni..ni nindoto mbaya tu nimeota ndio maana nimeshtuka. Kwahiyo usijali"

"Sawa mwanangu lakini umesnishtua sana" Alisema mama Pendo. Pendo alicheka kidogo wakati huo huo mama yake akaongeza kusema "Mbona huwashi kibatari? Mafuta yameisha? Aah utakuwa unaogopa kulala na mwanga"

"Hahaha ndio mama, unajua nikilala taa inawaka sijui najisikiaje yani. Kwanza usingizi unachelewa kuja" Alijibu Pendo akianza kwa kuangua kicheko.  Baada ya hapo mama Pendo alimtakia binti yake usiku mwema.

 "Na wewe pia mama" Alijibu Pendo.  Alipolala usingizi ulichekewa kumjia, aliwaza na kuwazua juu ya jambo hilo lililomtokea muda mchache uliopita. Akili akajisemea "Mmh leo ndio nimeamini baba Chitemo ni mchawi. kapitia wapi wakati wa kuingia ndani? Na wakati wa kutoka? Daah ama kweli ukistaajabu ya Musa itayaona ya Filaun. Chaudele kazi anayo" 

Baada kuhitimisha maneno hayo aliyokuwa akijisemea alisikia mtu akimsonya nje ya nyumba kisha akasema "Mshenzi mkubwa wewe" Alishtuka Pendo, sauti hiyo haikuwa ya mtu mwingine bali ni sauti ya mzee J. Hapo Pendo alijifunika blanket kuanzia miguuni mpaka kichwani na kisha kupumua pole pole kwa woga.
 
    Kesho yake asubuhi  aliamka akiwa mchovu mwili mzima, kitendo hicho kilimfanya kushindwa kumpitia rafiki yake ili waende kisimani kama ilivyokuwa kila siku  kumpitia Chaudele. 

"Huyu Pendo leo vipi? Haendi kisimani?.." Alijiuliza Chaudele ni mara baada kuona muda unasogea Pendo pasipo kutokea. Baadaye aliamuwa kumfuata nyumbani kwao, alipofika alimkuta Pendo yupo nje akiota jua.

 "Pendooo" Aliita Chaudele, Pendo aliposikia akiitwa aligeuka kutazama kule ilipotokea sauti akamuona Chaudele. "Wee ishia huko huko" Alisema Pendo kwa sauti kali. Chaudele alishtuka na kumshangaa, lakini akaamua kuvunga akiamini kuwa huwenda rafiki yake yupo katika masihara.  Na hivyo alicheka kidogo kisha akasema "Pendo acha utani.twende kisimani bwana kabla jua halijawa kali au mwenzangu leo huendi?.."

 "Ndio siendi, tena nakwambia hivi kuanzia leo mimi na wewe urafiki basi.  Naupenda ugali bwana, aka niache endelea na maisha yako" Alizidi kung'aka Pendo. Majibu hayo  yaliendelea kumshangaza Chaudele. Lakini hakutaka kuendelea kupingana na maamuzi hayo ya rafiki yake, alirudi nyumbani kichwa chini huku kichwani akijifikiria picha gani ambayo Chitemo anaionyesha mbele yake na ni kipi ambacho kimemsibu rafiki yake mpaka ambadilikie kiasi kile. 

 Wakati hayo yanaendelea kujili kijijini Ndaulaike, upande wa pili ndani ya jiji la Dar es salaam ilionekana gari ikiingia ndani ya nyumba iliyoonekana nzuri ya kuvutia.  Punde si punde akashuka kijana wa makamo akiambatana na baba yake. Kijana huyo aliitwa Saidon.

 "Saidon nafikiri muda huu ambao umehitimu  chuo, ndio muda wa kwenda kumtembelea babu yako kijijini. Lakini bwana chondechonde sitopenda kusikia tabia chafu kule, kama unavyojua kule yupo babu yako tu. Bibi yako alishafariki zamani sana kipindi hicho wewe bado upo baharini. Kwahiyo tegemea kuishi maisha ya kijeshi na sio kukaa kama tunguli"  Ilikuwa ni sauti ya baba yake Saidon akimuasa kijana wake.

"Sawa baba nimekuelewa " Alijibu Saidoni wakati huo akitamani muda huo huo anze safari ya kuelekea kijijini kwa babu yake. Shauku hiyo ilisababishwa na maneno aliyokuwa akiyasikia chuoni marafiki zake wakimwambia kuwa asilimia kubwa wadada wa vijijini hupenda kushobokea vijana wa mjini, hilo ndilo lilomfanya Saidoni kutamani kuianza safari muda huo huo ya kuelekea kijiji cha Ndaulaike akiamini kuwa kule anakwenda kuwakamata wasichana wote wa huko, asijue kuwa tayari kuna mwamba ameshaweka kizingiti kwa binti mzuri kuliko wote kijijini hapo, hivyo hatakama atashobokewa na wadada wa kijijini hapo basi itamlazimu awe na mipaka kwa kiasi fulani.

 "Watanitambua mimi ni nani kama kweli mademu wa vijijini wanahitikadi hizo.kitu cha kwanza naenda na kondom box tatu, maana nisiwadharau hata wa vijijini nao wamebungua" Alijisemea kijana Saidoni, maneno yaliyomfanya kuachia tabasamu kwa mbali. 

Huko Ndaulaike, mrembo Chaudele aliona tena hakuna haja ya kusubiri msiba umalizike ndipo ampeleke mwenyekiti barua ile ya vitisho kutoka kwa Chitemo, alijawa na ghadhabu kubwa.

 "Usipo ziba ufa, utajenga ukuta.  Hakika nisipo shughulikia hili suala mapema, nitajikuta nakosa hata rafiki wa kuongea naye hapa kijijini" Alijisema Chaudele na kisha akazipiga hatua kuingia ndani kuchukuwa barua  ili mwenyekiti akishatoka msibani amkabidhi. Lakini alipotazama pale alipoificha  ghafla hakuikuta..!!

Mmmh hapo hatamu aisee. TUKUTANE SEHEMU IJAYO ILI KUJUA KILICHO ENDELEA. Huyu mzee J huyu mmmmh. Hatari baba Lai. 😋 Kuna Saidoni niletee na mimi box moja aisee.
      SHEA MARA NYINGI KWENYE MAGROUP YOTE ULIYO ILI USIPITWE NA KIGONGO HIKI CHA KUSISIMUA.



No comments: