RIWAYA: MAISHA YANGU YA UVUVI SEHEMU YA THELATHINI NA MBILI 32





ENDELEA………………………
……………Mshana alinilazimisha nikimbie baada ya kumueleza kuwa yule kiumbe anakuja kwa kasi ya ajabu sana. Ndipo niliungana nay eye kumfuata kule ambako anaelekea. Tulitumia nguvu nyingi sana katika kuhakikisha kuwa yule kiumbe hatukuti. Lakini cha ajabu Zaidi alikuwa ana hema karibu yangu hata kila ninapojaribu kuongeza spidi ni kama nakimbizana na chombo cha moto kama vile pikipiki ama gari maana nilizidi kuchoka mimi tu.
              Tulipofika mbele Zaidi kulikuwa na njia pacha ambazo ziliweza kutuchanganya kwa kweli, ghafla tulisimama pale tukihangaika huku hatufahamu wapi tunaelekea, Mshana alinihoji kujua kama yule kiumbe anakuja ama laa!.
“Mnali vipi anakuja huyo kiumbe unamsikiaaa?”
Aliniuliza Mshana.
“Hapana simsikii kabisa kwa sasa ehee wapi tunaelekea?”
“Eheee huku hapa twende haraka”.
Tulisonga mbele lakini jambo ambalo lilinishangaa ni kwa kutosikia sauti ya yule kiumbe tena. Tuliendelea kukimbia hadi eneo Fulani lenye miti mingi sana alafu kupo na kiza nene.
              Maeneo hayo Mshana alisimama na kuniangalia kisha akasema jambo Fulani kuhashiria kuwa tumefika. Tulipunguza mwendo tukaanza kutembea mwendo mdogomdogo sana.
“Mnali sikia kwanza”
Nilsimama kumsikiliza anataka kuniambia nini
“Unasikia tumefika unatakiwa kuvua viatu vyako mpaka tunafika kule sehemu husika sawa fanya hivyo sasa”.
Nilimshangaa kuwa nivue viatu na kwa kuwa sikuwa na sauti pale nay eye ndie anapafahamu pale na sikuweza kumtilia shaka kuwa atanifanyia unyama ndani ya pori lile. Nilivua viatu kisha tukaanza kutembea peku japo miba zilitusurubu sana.
“Mshana..huku wapi tena”.
“Tukifika ndipo utafahamu ni wapi wewe nifuate mimi tu”.
Sikuwa na neno jingine Zaidi ya kuvumilia maumivu ambayo nilikuwa nayapata kutokana na zile miba kali, wasiwasi wangu pale ulikuwa kwa yule kiumbe ambae alikuwa nyuma yangu japo sikuwa namsikia lakini nilihofia sana endapo akiwa karibu yangu.
                Tulitumia ndani ya dakika kama nne kutoka pale tulipovua viatu hadi eneo Fulani kwenye kibanda kimoja hivi hapo ndipo Mshana akaniambia kuwa tmefika. Hapakuwa na mtu kabisa na pia eneo lilikuwa linatishia sana kwa kukaa mtu.
“Mnali hapa sasa tumefika tayari”.
Aliniambia Mshana, kitu ambacho kilifanya nimuulize swali
“Hapa wapi”
Huku nikimkodolea macho kama mtu aliyebanwa na mlango.
“Sikia hapa ni kwa mganga tulipo..”
“Khaaa! Mshana kwa nini hukuniandaa kutoka kule nyumbani uniambie huku eeeh!”
Nilimlaumu sana kwa kile kitendo ambacho alikuwa amekifanya cha kunipeleka kwa mganga bila hata mimi kunitaarifu kwanza.
“Mnali unajua kuwa mwanzo tuliliwaza swala la kwenda kwa mganga yakatukuta yapi na tuliyapanga yapi baada yay ale”.
“Hata kama lakini…….”
“Ahaaa! Kwa hiyo mnali leo nimejitolea japo na mambo yote ya ajabu yanayotokea lakini leo unanifanya kuwa mimi mjinga sana haya twende turudi nyumbani”.
Mshana alikasirika na ninavyomjua rafiki huyu hachelewagi kununa. Nilimkubalia na kumfanya kama ulikuwa ni utani na namshukuru sana.
 “Mnali acha utani tupo sehemu hatari hizi na wewe mwenyewe ndio ulisema kuwa tufute mawazo ya kwenda kwa mganga ili yule kiumbe kisijue na kikatufanyia mabaya hapa”.
“sawa basi twende huko haraka”.
Tulisogea hadi pale kibandani ambapo palitengenezwa kwa miti na udongo kwa chini kisha pakafunikwa kwa kaniki zenye rangi nyekundu na nyeusi. Eneo hilo lilikuwa linatishia sana.
                 Maana mambo mengi yalikuwa ya kutisha sana tunguli nyingi pamoja na mafuvu ya wanyama pamoja na ngozi za wanyama baadhi. Niliogopa sana baada ya kuona yale mambo kwa kuwa sikuwahi kuja kabisa haya maeneo.
“Mshana sasa mwenyewe yuko wapi sasa”.
“Ngoja atakuja sasa hivi…..”
Kabla hata hajamalizia sentensi ambayo alihitaji kusema tulisikia sauti ambazo zilisambaa yale maeneo. Sauti zenyewe zilikuwa za kicheko kikali sana tulihangaika kutafuta mwenyewe yuko wapi lakini hatukuweza kufanikiwa kumuona, ndipo ghafla anaonekana mzee mmoja kwenye kile kibanda akiwa amevalia nguo nyekundu pamoja na kilemba chekundu.
“Hahaaaa! Vijanaaaa karibuni sanaaa…”
Tulikaa pale ambapo alisema kuwa tukae.
aliendelea kuongea lugha yake ya ajabu ambayo sikuweza kuifahamu kisha akaniangalia na kuendelea kucheka tena.
                   Tulibaki kuangaliana tu pale ndipo akachukua Kibuyu kimoaja kisha akanipatia kwa kunielekezea mimi ili nikichukue. Nilikuwa na wasiwasi kiukweli lakini rafiki yangu Mshana alinisihi nisiogope. Baada ya kukichukua na kukiweka mkononi ndipo yule mzee akaanza kwa kuimba nyimbo zake huku akiniangalia na kupiga chafya kali sana kama mtu mgonjwa wa chafya.
“Kijanaa shika hiko kibuyu….”.
Nilikishika barabara.
“haya kinuse hiko kibuyu kisha pumulia mara tatu”.
Nilikinusa kisha nikapumulia kama alivyohitaji mara tatu. Baada ya kumaliza ndipo akakichukua kisha akakinusa nay eye akavutia hewa yake ndani kama mara tatu.
“Kijanaaa…wewe ni shujaa si ndioo”.
Tulibaki kuangaliana tu pale kuwa mimi ni shujaa tangu lini.
“Babuu hapana bwanaaa mimi si shujaa kabisa”.
“Unadhani nakutania!, je? Kama si shujaa umewezaje kuingia kwenye kisiwa ambacho hakijawahi kuingiliwa na mtu na akatoka salama?”. Niliduwaa maana kitu ambacho amekiongelea kimenigusa moja kwa moja mimi.
“Najua mmekuja hapa kuna kitu ambacho kinawasumbua sana hasa wewe hapo…una matatizo makubwa sana”.
“Ndio babu ni kweli nina matatizo makubwa ambayo nahitaji unisaidie kuyaondoa”.
“Sikia kijanaaa!...siku umekwenda kupeleka kile kitu kwenye sanduku uliambiwa nini kwenye ndoto yako ya usikuu?”.
“Mzee umejuajeee lakinii” nilimuuliza
“Usihofu naona kila kitu hapaaa! Tatizo lako wewe unapenda huruma san ahata sehemu ambayo haihitaji huruma alafu pia Mnali wewe ni mzembe sana wa mambo yanayokutokea unayadharau, najua kuna kiumbe kinakusumbua sana kweli au si kweli?”.
Mimi na mshana tuliangaliana.
“Kweli mzeee”.
“Haaa! Haa! Haaa! Haaa! Unaonaaa….nimewaambia nafahamu kila kitu na tena kiumbe mwenyewe hujawahi kumuona kabisaa machoni mwako je kweli si kweli?”
“Kweli mzee”.
“Unaonaaa sasa na huyo kiumbee anakusaidia hamna siku mlipanga kwenda kwa mganga na mkakwamisha na huyo kiumbeee?”
Hapo ndipo tukakumbuka kuwa ile siku ilitokea na tukapigwa Makonde kama wezi vile na tukashindwa kabisa.
“Sawaaa! Mnali unakumbuka siku ambayo ulienda Kisiwani na vijana wawili na wakapotea kwenye mazingira yasiyojulikana je? Unaweza kuniambia wapo wapi?”.
“Babuu! Kiukweli wale vijana sifahamu kwani walikamatwa na viumbe vikali sana mbele yangu kwa hiyo sijui kabisa”.
“Mnaliii unajidanganya sana. Jee? Mnapoishi karibu na bahari hamsikii watu wanakufakufa kila taarifa inapokuja wanakufa wawili kweli si kweli?”
“Kweli mzee”.
“Sasa wale vijana ambao uliwapoteza huko ndio hao ambao wamegeuzwa viumbe hatari sana wanamaliza na wataendelea kuwamaliza Zaidi watu wenu, na huyu kiumbe anaekusaidia ni uongo mtupu anashindwa kukumaliza kwa kuwa una kinga na chembechembe za hao viumbe havijaisha sasa nakuhitaji ufanye jambo ili nikusaidie”.
Nilibaki kung`aa sharubu pale mimi na Mshana ili tujue nini ambacho mzee huyo ambae anafahamu kila kitu kuhusu maisha yangu.”
“Vijana nahitaji muwe tayari kufanya jambo hili ili mufanikiwe kupoteza haya mambo kabisaa, kazi hii itafanyika baharini lakini naombeni utayari wenu”.
Tulibaki pale kusubiri nini ambacho mzee anataka kutuambia.
JE NINI MZEE HUYO ATAWAAMBIA?

TUKUTANE TOLEO LIJALO.



No comments: