Riwaya:: NDOA NDOANO SEHEMU YA 13




Riwaya:: NDOA NDOANO

           SEHEMU YA 13

Endelea......
Maposo furaha yake ilikuwa kubwa sana kwani hakuwahi kufikiria kwamba atakuja kumkamata mtu huyu ambae alikuwa anamsumbua kwa muda mrefu. Kutokana na kuwa mchafu sana Mumwa haraka hakuweza kujulikana ni nani walifikiri ni mtu mwingine tofauti kabisa na huyo.
Maposo aliweza kutangaza rasmi kuwa vita ambayo mtu huyo aliitangaza kwa kuwaua watu wake basi yeye atailipiza kwa wote pia kwa Mwamvita aliyeonja joto la amani basi lilimwagiwa na ubaridi wa shida kwa mara nyingine tena. Maposo aliamua kumtoa nje kijana huyo na alivyomkagua alimfananisha na Mumwa lakini hakuwa na uhakika kabisa. "Hee haya leteni maji mumwagie huyu mtu usoni mana hata kuoga kwake kazi". Mumwa aliweza kumwagiwa maji yaliyo ondoa uchafu wake usoni uliozibwa na nywele nyingi na akaonekana vyema kuwa ni mumwa jambo lililowashtua.
"Khaa kumbe ni wewe ndio unayafanya haya sasa utatueleza kwa nini uliua watu wetu kipi ambacho tumekufanyia mpaka unakuja kututisha hapa maisha yetu eeeh!".
Walimuadhibu sana Mumwa kwa kumpiga makofi pamoja na mijeledi iliyomuathiri ngozi yake kwani alitokwa na damu nyingi sana. Mwamvita aliumia sana huku akiwa analia kwa kukumbuka mengi mno. Alikumbuka kipindi wana anza mahusiano yao akiwa na mumwa na kipindi yanaanza kuwa mazuri ndo hivyo tena yanaingiliwa na mashetani kama Maposo.
Hakuona faida ya yeye kuolewa kabisa mpaka muda ule. Kila mwanakijiji aliipata habari ya kupatikana kwa Mumwa hata mzee Mashauri alivyoipata aliweza kuja mkuku mkuku hadi kwa Mzee Mbei ili aweze kumuona. Alijikuta anatokwa na machozi kwani si kwa hali ambayo alimkuta nayo Mumwa. Aliumizwa sana.
Mzee Makalani ndipo alipojua kweli Maposo pamoja na baba yake ni wakatili wa hali ya juu.Alijikuta anatokwa na machozi ya huruma mzee huyo alimsogelea Mumwa na kumuangalia majeraha yake. Punde si punde Maposo alifika pale huku akiwa anacheka sana. "Haaaa haaa Mzee Mashauli dawa ya mtu mkorofi ndio hiyo hawezi kutuchezea akili yetu mtoto mdogo kama huyu" Mzee mashauli alipatwa na ghadhabu za haraka sana Alijikuta anaenda kumvamia Maposo na kumkunja shati "yani wewe kijana unataka kulazimisha mambo ambayo hayawezekani kweli hivi unyama gani unaotufanyia sisi wanyonge tena namtaka mwanangu ni bora nife lakini nimpate mwanangu".
Maposo alimshika mzee huyo na kumsukuma pembeni kwa bahati mbaya mahali hapo alipodondokea palikuwa na mti usiomaliziwa kukatwa hivyo ulikuwa na ncha kali iliyomuingia Tumboni. Mwamvita alilia sana baada ya kumuona baba yake mzazi anafanyiwa unyama ule tena mbele yake. Mahali alipolala Mumwa baada ya kupigwa sana palikuwa ni bondeni na mahali alipojichoma Mzee Mashauri palikuwa na muinuko hivyo zile damu zikawa zinatiririka na kuja hadi alipo Mumwa. Joto la damu ya Mzee mashauri liliungana na damu yake Mumwa. Alizinduka kutoka usingizi mzito wa kupoteza fahamu.
Alipata ahueni kidogo huku Maposo na Baba yake wakishitushwa na ile hali "ahh hii sasa kazi mbona huyu mzee kiherehere mpaka anajiua bwana. Mwamvita kwake lilikuwa pigo kubwa sana.
Majira ya usiku mmoja wa walinzi ambao  kwa upande wake aliona mambo wanayofanyiwa wale wanandoa wawili si mazuri. Aliandaa njia ya kuweza kuwaondoa wale wawili. Kwa bahati nzuri alifanikiwa na kuwatoa usiku huo wawili hao bila kujulikana. Asubuhi Maposo aliandaa Mtu wa kwenda kumtoa mzee Mashauri pale alipolazwa kutokana na hoja ya jana. Lakini hakuonekana walinzi wote walimtafuta lakini hakujulikana wapi yupo. Walikwenda kumuangalia Mumwa sehemu waliyomhifadhi napo hawakumkuta. Hawakuchoka wakaenda kwa Mwamvita nako hakukuwa na mtu walishangaa kwanza.
Asubuhi hiyo Kumbe mzee Mashauri alishapata nafasi ya kwenda nyumbani bila hata yeye kuonekana kwa msaada wa yule kijana aliyewatoa Mumwa na Mwamvita.  Mzee huyo japo kuwa na hali yake aliomba mkewe monalisa pamoja na Mwanae wa mwisho Sikitu wajiandae wakimbie kwani sasa kijiji hiko di kizuri wataenda kukutana kijiji ambacho Mumwa mzazi wake wa kike yupo huko. Walikubali ndipo msafara ukaanza huku akiwa hoi baada ya kupata kidonda cha tumbo.
Upande wa Mumwa na Mwamvita walijitahidi usiku huo kutoroka japo Mumwa alikuwa hoi zaidi alijikakamua mwanaume ili afike huko aendako. Majira ya asubuhi waliweza kupata msaada wa mtu mmoja aliyekuwa anatoka mahali fulani kwenda kijiji hicho ambacho Mumwa yuko mzazi wake wa kike.
Safari wakati inaendelea tayari Maposo katuma kundi lake kwenda kwa Mzee Mashauri na kundi jingine kwenda msituni kumtafuta Mwamvita na Mumwa. Damu zilionyesha wapi Mzee Mashauri alifika hadi kwake ikawa rahisi kufika kwake japo hawakumkuta. Upande wa msituni waluona michirizi ya damu ikielekea mahali lakini walifika hadi sehemu ambapo kuna mnyama aina ya nguruwe poli aliyevamiwa na mnyama mkali.
Mzee Mashauri ni mjanja kupinfukia kwani alama zote alizopita aliweza kuzitofautisha ili kuwapoteza wale watakaofuata nyuma.

Itaendelea.......



No comments: