Riwaya:: NDOA NDOANO SEHEMU YA 14




Riwaya:: NDOA NDOANO
         
             SEHEMU YA 14

Endelea....
Njia ambayo aliweza kupita Mzee Mashauri na Familia yake ilikuwa ni ngumu kufahamika na watu wa Maposo,alitumia mbinu za uwindaji ambazo alikumbuka kipindi wapo na mzee Mashauri hivyo iliwafanya wabaki salama katika safari yao isiyokiwa na matumaini.

Lakini hata hivyo punde si punde walifika mwisho wa njia ambayo walitarajia kuwa itawafikisha mahali ambapo wao walikududia,Mashauri alimgeukia mkewe na kumhoji kama yeye anaikumbuka njia ambayo huwa wanaitumia sana katika kipindi cha zamani wakati wanahitaji kwenda kijiji ambacho wanahitaji kufika.

Haikuwa rahisi hata kwa mkewe kuweza kukumbuka hivyo iliwabidi watafute nafasi ya kujihifadhi ili wajue wanatoka vipi. Sikitu alikuwa hajielewi kutokana na usinhizi mzito ambao ulimfanya asijue kinachoendelea huku akiwa kabebwa mgongoni na mama yake. Mzee Mashauri hakuamini usalama ambao wanao pale kuwa ni asilimia ndogo sana za usalama,ndipo alinyoosha miguu kusimama kisha kuangaza macho pande zote.

Alipojihakikishia kuwa tayari kuko salama walikaa kwa ajili ya kupumzika. Mama yake mwamvita alijikuta akilia huku machozi yakimbubujika sana. 'Mke wangu mbona unalia mbele ya mtoto wetu kipi kimekusibu?'...aliweza kuuliza swali hilo ambalo lilichukua taswira ya ukimya wa muda mrefu kidogo mpaka kujibu 'Mh mume wangu hapa nahuzunika sina amani moyoni damu yangu iko wapi na sijui mwamvita wangu yu katika hali gani aaah jamaniii' Basi kauli hiyo iliweza kumuumiza hata Mashauri ambae alichukua jukumu la kumnyamazisha. Baada ya muda walipitiwa na usingizi.

Muda ulipita kidogo. Mzee Mashauri akiwa usingizini alihisi kama njozi ambayo inamjia lakini kwa upande ungine akihisi ni kitu cha kweli. Wasiwasi wake ulimfanya atoke katika dunia ya  usingizi na kuja dunia hai. Alifumbua macho alikurupuka baada ya kuona kundi la watu wa Maposo likionekana kwa mbali. Alishukuru sana kwani bila kuamka basi yangekuwa mengine.

Aliwaamsha Mkewe na mwanae wakaanza kutoka maeneo hayo na kukaa kando. Walishuhudia jinsi walivyokuwa wanahangaika hawajui wapi wapite baada ya njia kuwa mwisho. Hatimae waligeuz na kurudi nyuma ili kurudi kule walikotoka na ndio ukawa mwisho na usalama wa Mzee Mashauli na Familia yake.

Upande wa Mumwa akiwa na mwamvita wakiwa na kijana ambae aliweza kuwasaidia kuwapa kipando. Safari yao ilikuwa na misukosuko sana zaidi ya Mkwewe Mzee Mashauli kwani hali ya Mumwa ilikuwa tete hivyo kazi ya kumlinda ilibaki kwa Mwamvita ambae nae hali ya mkono wake ilikuwa mbaya baada ya kukatwa kisu na Maposo na kuanza kuoza mkono huo.
Kijana aliyewasaidia alifanya kazi nzito ya kuliendesha baiskeli ambayo ilikuwa maarufu sana ambayo inakokotwa na punda. Walichukua muda mrefu kukitafuta kijiji ambacho alizaliwa mumwa. 

Masaa kadhaa yaliisha wakiwa njiani ndipo nao waliamua kumpumzisha kiumbe ambae hatumii mafuta zaidi ya nguvu alizojaaliwa na Mungu.
Upande ambao waliweza kypumzika kumbe haukuwa mbali na ule ambao walipumzika Baba mwamvita. Usiku ulipoingia Mwamvita aliwasha moto ambao ulikuwa ni kama mwanga ambao ulitumika kujikinga na wanyama wakali. Moto huo ulimfanya Mzee Mashauli kuuangalia kwa makini sana wasije kuwa ni watu wa Maposo wamefanya kambi ya muda mfupi wakijiandaa kuwatafuta. 'Mume wangu ona Sikitu anahisi baridi kali sana ebu twende hata kule uliko moto tunaweza kusaidiwa.' Monalisa aliongea 'Mke wangu yahitajika umakini wa hali ya juu mana huku porini si kila moto ukajua watu wema wengine ni mashetani' alimkatisha tamaa mkewe aliyedai waufuate ule mwanga.

Lakini walikata shauri la kwenda kuufuatilia ule moto. Walitembea kwa tahadhari kutokana na kuwa ni usiku mzito sana.

Usiku huohuo kundi la Maposo lilifanya kambi ya muda maeneo ya porini huku wakipanga mikakati ya kuwatafuta kwa mara nyingine.

Mzee Mashauri alifanikiwa kukaribia na kuwaona waliopo pale. Ghafla Mwamvita alishtuka akachukua sime na kuonyesha kule ambako watokeako Mzee Mashauri na Mama yake.
'Naomba usitufate tuache hivi wewe ni mtu gani usiyejua kama hupendwi sikutaki na ukikaribia najichoma kisu..' Mwamvita alidhani kuwa ni walee vijana wa maposo kutokana na giza nene kutanda.
Mzee mashauri alishika mdomo kwa mshangao kwani yeye alikuwa anamuona vyema sana Mwamvita
"Haaa kumbe mwanangu mwamvitaaaa...."
Mama yake alipiga yowe kubwa la kuonyesha kutoamini kwa kuonana na mwanae mwamvita
'Mwananguuuuuu mwamvitaaaa....'

'Mamaaaaa...mama mamaaaa'

Alidondosha sime na wakakumbatiana. Hapo ndipo Mumwa aliamka na kuonana rasmi na wazazi wa Mwamvita. Kila mmoja alilia kwa furaha ya kuonana tena.
Mwamvita alitazama pale alipolala kijana hakumuona kabisa. Walimtafuta lakini hawakubahatika kumuona. 'Wanangu vijana kama hawa nawafahamu hebu tuondoke hapa tukae mbali alafu tuone'. Kweli walitoka na kukaa kando.
Ajabu yule kijana kumbe alifika hadi kwa wale watu wa maposo na kuwapa taarifa kisha wakafika pale. Lakini hawakubahatika kuwakuta. Ndipo mzee Mashauri akasema "unaona kumbe Kikulacho kipo miongoni mwako yule kijana mliemuamini leo hii anawafanyia hivi jee bila kukutana wanangu ingekuwaje?

Itaendelea



No comments: