Riwaya:THE TRUE LOVE. SEHEMU YA TISA (09).
Riwaya:THE TRUE LOVE.
SEHEMU YA TISA (09).
"Yaani mganga naomba ufanye kweli ili kijana huyo nimpate ". Aliongea Recho,mganga Sagora akawa anamkazia macho usoni bila hata ya kuyapepesa kushoto wala kulia hadi binti akajishuku kwa kitu asichokijua."Bi
nti,umeeleweka vizuri sana ila itakubidi siku ya juma mosi mapema kwenye mishale ya saa kumi na mbili uje hapa,maana siku hiyo ndo siku rasmi ya kijana huyo kukutana na binti mmoja maeneo furani,hivyo ni lazima hilo ulizingatia usilipuuze".Mganga Sagora aliyazungumza hayo na kumfanya Recho awe na maswali kadha wa kadha ya kumuuliza mganga huyo lakini kila akijaribu kutaka kuyauliza alijikuta akisita kwani kinywa chake kilikuwa ni kizito mno kwa muda huo.Alisimama akabaki akimtazama tu mganga Sagora baadae akamuaga na kumwambia atayatekeleza yote aliyomueleza.....baada ya kumaliza ,Recho hakuwa na muda wa kupoteza alianza kuondoka kuifuata gari yake aliyokuwa ameipaki pembeni karibu na ukuta wa nyumba ndogo ya Sagora ...aliifikia akapanda na kuiwasha hapo hapo."Huyo binti ni nani? Hapana kwa hapa ni lazima nifuatilie ili huyo msichana atakayekutana na Imma juma mosi nimjue". Alijisemesha hayo baadae akaanza kuidrive gari yake kurudi kwao.Upande wa yule Dokta kule hospitalini baada ya kumwambia Jack kwamba Imma si mzima hasa katika suala zima la nguvu za kiume,binti huyo alistaajabu sana,lakini pamoja na kustaajabu kiasi hicho hakuyaamini maneno ya Daktari huyo moja kwa moja."Uliniambia unaitwa nani kweli?" Aliuliza Dokta huku akiyatazama kwa uchu mapaja meupe ya Jack yaliyokuwa yakionekana japo si waziwazi."Naitwa Jack,nielekeze sasa ofisi ya Imma ilipo maana muda unaenda".Alisema Jack,dokta huyo akawa anasita sita mwisho akaona ni bora amwelekeze tu binti huyo ni wapi ofisi ya Imma ilipo."Unasikia Jack,nenda ofisi namba kumi humo ndo utamkuta Imma".Baada ya Dokta kumwelekeza,Jack hakusubiri chochote alinyanyuka akatoka nje bila hata ya kumwambia neno lolote Daktari huyo.Alipotoka nje,mwendo wake wa kuifuata hiyo ofisi ulikuwa ni wa haraka kwani alikuwa na hamu sana ya kuonana na Imma kipenzi cha moyo wake.Kwa huo mwendo alifanikiwa kuifikia hiyo ofisi akaenda na kusimama mbele ya mlango tayari kwa kuanza kubisha hodi,alibisha hodi kama mara Moja tu ,mlango huo ukafunguliwa akaonekana Imma mwenyewe akiwa ndani ya koti jeupe la kidaktari kama ilivyo kawaida yake ya siku zote."Waoo Imma ".Alisema Jack,huku moyo wake ukiwa na furaha ya ajabu hadi akawa anatamani kumkumbatia kijana huyo japo huo uwezo kwa huo muda hakuwa nao."Karibu Jack,ingia". Aliongea Imma,bila kusita wala kugonja,binti akaingia ndani ya ile ofisi,Imma akafuata kwa nyuma."Kaa tu hapo hapo Jack wala usisumbuke sana".Alisema Imma na kumfanya Jack akae kwenye kile kiti kingine akawa anatazamana uso kwa uso na kiti cha Imma,Imma alikisogelea kiti chake hicho akakaa wawili hao wakawa wanatazamana tu kwa takribani dakika tano bila kuzungumza chochote,ikumbukwe Imma hakuwa muongeaji sana.Sasa huo ukimya ulivunjwa na Jack kwa kuyaanzisha mazungumzo."Imma mambo?" Alianza kwa mtindo huo Jack."Poa tu,kwema Jack?" Imma aliitikia na yeye akamjulia hali."Kwema tu nakuona unazidi kung'aa tu Imma sijui siku hizi unakula nini". Aliongea Jack kisha akacheka huku akijaribu kuzielezea hisia zake kwa kumtazama tazama Imma usoni mwake."Kunawiri wapi Jack,kawaida tu sema wewe ndo unazidi kupendeza utadhani malaika". Aliongea Imma,Jack akacheka sana,kwa muda huo moyo wake kila kona ulikuwa umetamalakiwa na furaha mpaka akawa anatamani kuwa na Imma siku hiyo muda wote."Imma samahani ninaweza kukuambia kitu?" Jack aliuliza mara hii akianza kuvichezea chezea vidole vyake."Unaweza Jack,usisite niambie tu".Imma alimkubalia,lakini msichana huyo hakuanza kuongea direct alijifikiria kwanza."Imma una....una..una mh?" Alishindwa hata aanze vipi akaishia kushikwa na kigugumizi tu,aliushusha mkoba wake akaufungua na kisha kulitoa lile ua ambalo alilichuma kule nyumbani kwao."Imma naomba ulipokee hili ua".Alisema Jack huku akimkabidhi lile ua Imma....Imma akalipokea."Asante Jack kwa zawadi hii ya ua,ama hakika ua ni zuri sana tena linavutia". Aliongea Imma baada ya kulipokea ua lile,Jack akatabasamu akawa anatamani amfungukie Imma pale pale kuwa anampenda lakini akawa anaogopa kwamba huenda Imma atamuelewa vibaya."Au Jack una neno unataka kuniambia sema tu maana nakuona kama haupo sawa kabisa,au unaumwa?" Aliuliza Imma,Jack akakataa kwa ishara ya kutikisa kichwa."Imma nakuomba unitazame usoni japo dakika moja tu". Alizungumza Jack huku macho yake hayo akiyalegeza mithili ya mtu aliyekula kungu.Imma akaanza kumtazama usoni."Umeona nini Imma naomba uniambie".Alisema Jack baada ya Imma kumaliza kumtazama usoni."Nayaona macho mazuri,kutoka katika uso wa binti aliyebarikiwa na Mungu kuwa na urembo asilia na wa kupendeza ".Alisema Imma,maneno yale yakamchoma sana Jack mpaka mwili wake ukawa na msisimko wa ajabu.....binti alishindwa kujizuia."Imma,nakupenda peke yako,nakupenda mno Imma,natamani niwe wako kwani nimekuzimia sana.....Imma nimevumilia kwa muda mrefu ila uvumilivu huo wa kuendelea kunyamaza umenishinda,Nakupenda Imma". Aliongea Jack kwa kumaanisha,kila neno alilolizungumza lilitoka ndani ya moyo wake."Jack hata Mimi nakupenda sana,tena sana tu wala usijali". Aliongea Imma,Jack akasimama."Imma natamani nikubusu".Alisema Jack muda huu alizipiga hatua za mwendo wa taratibu kumsogelea Imma hadi akamfikia na kisha kumbusu."Ni hivyo tu Imma,nakupenda na juma mosi natamani siku hiyo tukafurahi wote". Aliongea Jack."Usijali Jack siku hiyo ikifika sote kwa pamoja tutafurahi tu".Alisema Imma."Unaupa amani sana moyo wangu Imma,basi mi nikuage uendelee na kazi nitakusalimia baadae,nipe na namba zako za simu". Aliongea Jack.....Imma akamwandikia hizo namba haraka haraka kwenye kijikatarasi akampa na hapo wakaagana kwa mara ya pili,Jack akatoka humo kurejea kwao akiwa na furaha na ajabu.Jack alifika kwao akamkuta dada yake Recho akiwa amekaa kwenye ile bustani yake akamfuata ili akamjulie hali kwani tangia kupambazuke siku hiyo hawakuwa wameonana.....alitembea akawa amemfikia,alisi
mama akaanza kutabasamu "Dada Recho habari za asubuhi?" Alisalimia Jack,Recho akawa kama hajasikia zaidi aligeukia pembeni na kwa kumtazama tu alionekana kuwa na hasira na tayari kuna chuki alikuwa ameshaijenga kwa mdogo wake huyo."Dada mbona umenuna kiasi hicho kulikoni au kuna kipi kimekusibu niambie dada angu!!" Alisema Jack huku akimbembeleza dada yake.Recho aliugeuza uso wake akamtazama sana Jack kisha akamsonya kwa hasira."Mi huwa sisalimiwi na wanafiki unaweza kwenda tu wala usijisumbue sana". Aliongea Recho,Jack akashindwa kumuelewa kabisa dada yake ni kipi kimempata maana alikuwa amebadirika kupita kawaida."Dada Recho kwani nimekukosea nini hadi ukanibadirikia kiasi hicho?" Aliuliza Jack."Utajua mwenyewe mimi nataka uniondokee mbele yangu wala usije ukanichefua,ondoka".Jack kwa maneno hayo ikambidi aondoke tu lakini akawa amebaki na maswali magumu sana kichwani mwake.Aliondoka huku akigeuka geuka nyuma akatembea hadi ndani na kuingia chumbani kwake.Sasa ile anaondoka tu,zilipita dakika tano,kwenye mlango wa geti akaonekana rafiki yake na Jack Minza akija,,akatembea haraka haraka akawa amemfikia Recho pale alipokuwa amekaa."Hahahaha!! Recho kwa hiyo utafanyaje sasa?" Minza alianza kwa kumwongelesha maneno hayo Recho maana ukweli kuhusiana na Imma pamoja na mdogo wake Jack ulikuwa umeshafichuka.Mtu pekee ambaye alimueleza Recho kwamba Jack anampenda Imma na ana mpango nae ni Minza maana siku za nyuma,Jack aliwahi kumwambia Minza kwamba hatokuja kuolewa na mwanaume yeyote zaidi ya Imma,hiyo ikawa kama siri ,lakini Minza siri hiyo akaamua kuivujisha kwa kumwambia ukweli wote Recho.
"Nitajua cha kufanya,mimi ndiye Recho ,,,huyo Jack ni mtoto mdogo sana kwangu,we niachie mimi nitajua cha kumfanya".Alijibu Recho huku mapigo ya moyo wake yakienda haraka haraka."Nakuaminia dada,sasa vipi huyo Jack amesharudi au bado?" Aliuliza Minza huku akiyaangaza macho yake huku na huko."Amesharudi yumo ndani ".Alijibu Recho."Poa hebu ngoja nikamuone".Aliongea Minza kisha akaanza kuzipiga hatua kuelekea ndani....Alitembea kwa mwendo wa kawaida akawa amefika,akanyoosha moja kwa moja hadi chumbani kwa Jack,kwa bahati nzuri akakuta chumba kipo wazi hakijafungwa.Aliingia akamkuta Jack amekaa kitandani huku akiwa amejiinamia.Tayari mishale ya saa tano za asubuhi ilikuwa imeshawadia."Jack mambo?" Aliuliza Minza lakini Jack kutokana na kwamba alikuwa ndani ya dimbwi refu la mawazo hakuisikia hata kidogo sauti hiyo ya rafiki yake Minza.Minza ikambidi arudie kwa mara ya pili huku akimtigisha ndipo Jack akakurupuka."Sh
oga angu vipi,na umri wote huu unakuwa na mawazo ya kizee kiasi hiki hadi husikii hata salamu yangu?" Alisema Minza."Hapana Minza kuna kitu kidogo tu nilikuwa nikikiwaza,vipi habari yako Minza?" Aliuliza Jack,Minza akakaa hapo hapo kitandani."Nzuri tu,unajua nimekutafuta sana hadi nikawa najiuliza huyu ameenda wapi,ila tuachane na hilo......nimekuja ili unipe ule mchongo wa juzi maana uliniahidi leo hii utanipa".Alisema Minza,Jack akamtazama usoni,akaachia tabasamu hafifu."Ni kuhusiana na Imma tu wala si mchongo mwingine.....juma mosi nina mpango wa kuonana na Imma ,si unajua ni kwa kijinsi gani ninavyompenda mwanaume huyo hadi sijielewi".Alizungumza Jack kwa sauti ya upole."Waoo!! Yaani mtashibana sana.....Sasa unaweza kuniambia ni sehemu gani mtakutana?" Aliuliza Minza."Itakuwa ni kwenye ukumbi wa hotel ya jiji la Tabori,ndani ya Mishomo corner nadhani hotel hiyo unaifahamu".Alijibu Jack,Minza akafurahi mno."Hotel hiyo naijua sana,yaani kwa hapo mmechagua sehemu sahihi na inafaa,,,Okey poa rafiki yangu ngoja mi nikuache nirudi nyumbani nikapike baba ameenda shambani asije akakuta sijamwandalia chochote".Baada ya Minza kumaliza kuyaongea hayo,alitoka chumbani kwa Jack,akaanza kuelekea nje.Baada ya kufika nje hakunyoosha moja kwa moja kwenda kwao bali alipita kwa Recho."Vipi umemkuta humo ndani ?" Recho alimuuliza."Yeah!! Nimemkuta,halafu sijui ametoka kufanya uasherati maana amechoka kuliko neno lenyewe la kuchoka". Aliongea Minza,Recho akaguna."Ehe amekuambiaje au amesemaje?" Aliuliza tena Recho."Nilimuulizia habari za Imma akadai siku ya juma mosi anampango wa kuonana na kijana huyo Tabori hotel ndani ya Mishomo corner". Aliongea Minza,hapo hapo Recho akawa anatabasamu."Umefanya jambo la maana sana kumuulizia hivyo,sasa we subiri nitakachomfanyia hiyo siku". Aliongea Recho baadae akamsihi Minza awahi nyumbani kwao,wataonana muda mwingine tena.Hivyo Minza alichomoka mkukumkuku kuelekea nyumbani ili akafanye yake.Mchana wa siku hiyo hiyo,ule mpango wa Wanjera kumuangamiza mama yake ulitimia kwa zaidi ya asilimia mia moja......Siku hiyo aliandaa chakula kama kawaida,,,chakula cha mchana tena chakula kitamu ambacho aliamini ni lazima mama yake akile .Alipika aina furani hivi ya chakula mithili ya pilau pamoja na nyama ya kuku,kuku ambaye alimnunua .Basi alikiandaa hicho chakula na kikawa tayari kabisa.Alitafuta sahani za maana akazipakulia chakula zote,lakini ile sahani ya tatu akaiweka pembeni.......
***************************
Kwa maana alitaraji kuiwekea sumu sahani hiyo na alipanga ndo sahani ambayo itatumiwa na mama yake.Kwa vile kile kijimfuko chake cha sumu alikuwa ameshakiandaa tayari hilo wala halikumpa shaka wala hofu ya a aina yoyote ile.Sasa aliibeba ile sahani,akaiweka juu ya chombo kimoja hivi mithili ya kinu kidogo,,,akasimama na kuanza kuchungulia dirishani,akatoka hapo na kuanza kuchungulia na mlangoni akajiona yupo salama hakuna anayekuja wala kumwijia na wala sauti tu ya kitu kinachoashiria kuja haikusikika.Furaha ikawa ni kubwa sana moyoni mwake na tabasamu likawa halikomi usoni maana kwa mara hiyo aliamini zile mali ni lazima zitakuwa zake,mamaye atakufa tu na kifo hatokikwepa kama siku ile....na kama Mungu wake alimsaidia siku ile basi leo itakuwa ni vigumu kukiepuka kikombe hicho.Mambo yakawa ni mazuri mno kwa Wanjera."Hahahaha !! Mzee ni lazima afe,kijana ni sawa anaweza kufa,lakini kwa Mzee lazima kufa....leo mama ni lazima amfuate baba kule alipo,haiwezekani mali hizi niziangalie tu,wee mi ndo Wanjera bwana". Alijiongelesha binti huyo baadae kama kwenye dakika mbili hivi ile sahani ya chakula akaiwekea sumu.Baadae alizitia ndani ya chombo kimoja akaondoka nazo hadi sebuleni,,kila sahani akaiweka kwenye nafasi yake huku ile yenye sumu akiiweka kwenye sehemu aliyokuwa akipenda kukaa mama Imma.Alimaliza akamfuata mwanae,baadae akaja na kumkaribisha na mama yake.Wote kwa pamoja wakajumuika kwa ajili ya kupata chakula hicho,mama Imma alisali,na hapo hapo wakaanza kula.Maskini mama Imma.
ITAENDELEA.............................................

No comments: