SIMULIZI:- ZINDUNA; (malkia wa majini) SEHEMU YA {01}





SIMULIZI:-
ZINDUNA;
(malkia wa majini)
SEHEMU YA {01}


             Endelea...........

"Miaka mingi iliopita Baba yangu alinipa story kuhusu jini lilivyomtesa zaidi ya miaka kumi, alisema jini yule alikuwa akimfanyisha Tendo la Ndoa kama punda usiku na mchana, hakupata nafasi ya kupumzika, kila wakati jini yule akitaka Baba Tendo la ndoa, ilimbidi baba yangu Akabiliane Na Swala hilo, aliendelea kunipa kisa hicho akisema.. "kibaya zaidi jini yule alinifanya mtwana wake sikufanya kazi yoyote ile mi nilikuwa wakushinda ndani kama utumbo, niliishi nae bila ya mtu yoyote kujua, siku nyingi zilipita nilijaribu kutafuta mwanamke nioe ili nimkomeshe lakini ilikuwa kazi bure kwani alikuwa akizifunga Hisia zangu za kiume mara nyingine nikiwa tu Mwanamke mwingi wakati wa Makabiliano ya  Tendo la Ndoa basi hapo hapo hisia unitoka kabisa hakuna mwanamke alievumilia hilo wote niliowaoa walinikimbia, lilitapakaa jina baya hapa kijijini lilionzishwa na wanawake kila nilipopita walinicheka na kunitupia maganda ya ndizi waliniita 'Towashi' mwanaume asie na uwezo wa Hisia, sifa hiyo sikuipenda hata na nje ya hilo ni aibu kubwa upande wangu, nilichoka kuvumilia vituko vya jini huyo niliamua kwenda kwa wataalamu wa maswala hayo lakini wengi walichemka, siku moja nilienda kwa mzee Miti Mingi ambae alikuwa mshauri mkuu pale kijijini wengi walimtambua kwa jina maarufu mzee wa busara. nilimfuta mzee wa busara na kumweleza yote nae alinipa njia baada ya kunielewa, alinielekeza mbali sana kutoka kijijini kwetu, ambapo alisema nitapata tiba na hilo tatizo litakwisha kabisa, nilienda na bahati nzuri mzee nilioelekezwa nilimpata nilimweleza shida zote na mzee yule alifanya matambiko ya siku saba, jini yule alitoka na nikachukua na mke kutoka kijijini kwao, nilirudi nae kijijini nikiwa kama shujaa kwani tatizo la Upotefu wa Hisia Kwa mwanume liliisha kabisa baada ya mwaka mmoja wa ndoa tulibahatika kukupata wewe,... mama yako akakuchagulia jina la Faraja, jina hilo likapita.." baba alinisimulia nilitaka kujua huyo jini aliemsumbua nilimuuliza "baba huyo jini alikuwa anaitwa nani?" nilimuuliza lakini kabla hajaniambia baba alianza kujinyonga nyonga shingo na haikupita muda akawa amepoteza maisha, sikuweza kumjua jini huyo.. siku nyingi zilipita tokea baba afariki hivyo niliendelea na tamaduni alizokuwa akifanya baba, niliendelea na kazi ya uvuvi kama alivyokuwa akifanya baba mama nae aliendelea na kazi yake ya ufumaji wa nguo mbali mbali hususani kofia za watemi, siku hiyo nilitoka baharini nikiwa na shamla shamla kibao kwani siku hiyo tulipata samaki wengi kupita siku zote hivyo nilichagua samaki mkubwa kama zawadi kwa mama yangu lakini sikujua kama siku hiyo ndio ilikuwa siku ya maagano mimi na mama yangu, kwani nilimkuta mama akiwa amefariki kwa style ile ile iliomuua baba, ilikuwa ni huzuni kwangu kuwapoteza wazazi wawili ndani ya mwaka mmoja, muda ulienda na taratibu ule unyonge ulienda unapungua nguvu hadi ikafikia wakati nikajizoelea kuwa mimi ni yatima. muda ulipita kutoka utoto hadi kufikia utu uzima sasa ni miaka 24, tokea siku ile wazazi wangu wapoteee ulimwenguni nilikua siamini kama kweli kuna kiumbe anaitwa Jini,...
       **************************
Baada ya kuwapoteza wazazi wote wawili nilijiuliza sina pakushika, sina pakukimbilia sina wa kumlilia shida zangu nani anisaidie? maswali haya yalinisumbua sana kichwani ila hatima yake niliipata kwa kuyajibu mwenyewe niliona the only way to survive nikupambana kwani mie ndio kidume, moyo wa ujasiri ulinizunguuka na hapo nikauendeleza uhusika wa baba katika uvuvi.. siku hiyo tulikuwa zetu baharini mimi na marafiki zangu wawili Omary na Leki,  tukimsubiri Bulicheka. aje twende, baada ya muda mfupi Bulicheka alitokea tukapanda zetu mtumbwi tukaelekea huko tulipozoea kuvulia, "Hebwana eeeh!! hii saa kumi na moja eti??" Leki aliuliza huku akitutizama "eeeh!! siunaona hata jua lilipo" Bulicheka nae alimjibu huku akizidi kupiga kasia kuelekea huko tulipo patungia Nina la 'Kisiwa cha samaki' kutokana na kuwa tunapata samaki wengi kupita kiasi,

"eeeh!! sa kumi na moja hii atabahari imetulia kabisa" nami nilichangia, tuliendele na safari yetu, yalipita masaa mawili tokea tuzungumzie hali ya hewa na ghafla bin vuu!! wingu zito lilianza kujikusanya angani hofu ikatanda baina yetu "mungu wangu mvua isinyeshe maana tuko sehemu mbaya sana hii" Bulicheka alisema huku akikata maji kwa spidi akisaidizana na Leki, aliekuwa upande wa nyuma, wingu lile halikuchukua muda angani na papo hapo mvua ikaanza kushuka kwa kasi ikiambatana na radi kari, mimi na Omary tulianza kufanya jitihada za kuchota yale maji yaliyokuwa yanajaa mtumbwini, "fanya upesi upesi, Omary mvua kubwa hii tutazama" nilimuusia Omary, tulijitahidi kadri tuwezavyo lakini wapi jitihada zetu hazikuzaa matunda kwani mvua ilikuwa kubwa sana, bado tunahangaika na maji ya mvua lilikuja wimbi kubwa la maji na kuufunika mtumbwi, kila mtu alitupwa upande wake, upande wangu nilijitahidi sana kujivuta nipande juu ili nipate hewa lakini hakuna ndio kwanza maji yalizidi kunivuta kushuka chini, nilijitahidi kuparangana kwa nguvu zangu zote nipande lakini hamna kitu maji yalizidi kunivuta mpaka chini kabisa ya maji, ambako kwa mara ya kwanza nilistaajabu ya musa na kuyaona ya Firauni. pumzi ilibadirika kabisa na sikuwa kama niko ndani ya maji kilichonishangaza zaidi ni pale nilipotua kwenye mji nikiwa mkavu sina hata tone la maji huku mavazi yangu yakiwa yamebadirika na kuwa meupe yenye kumeremeta, nilishangaa mijengo ya dunia ile ya ajabu vile yalivyo pambwa kwa madini kila nyumba ilikuwa inameremeta kwa mapambo mengi ya kuvutia huku watu wake wakiwa bize kuendeleza shughuri hiyo, nilibaki ni kizubaa nisijue pale nimefikaje "au nimeshakufa?? mbona huu ni ulimwengu tofauti na kule nilipokuwa naishi" nilijiuliza huku nikizidi kuyashangaa majengo yale marefu mazuri yenye urembo wa madini,

nilizidi kuzunguka huku na kule kuona kama nitafanikiwa kuiona njia ua marafiki zangu, lakini hamna nilichozidi kushangaa ni mabinti waliokuwa nusu uchi wakifanya kazi za kusafisha mapambo yale ya nyuma "mwanzo mpaka mwisho naona ming'ao tu hii kweli sio Dunia niliyokuwa nikiushi huku ni peponi bila shaka" nilijisemea kwa mbali nilianza kuona kuna kundi kubwa la watu lililokuwa limekusanyika ilikuwa kama gulio hivi, nilianza kulisogelea ili niweze kupata, ufafanuzi huenda ningepata njia ya kutoka kwenye ulimwengu ule ambao sikujua nimefikaje fikaje.. lakini nilipozidi kulifata kundi lile la watu ndio walizidi kuonekana mbali nilijikuta nikizunguka sehemu ile ile moja tu nilikata tamaa kusogea huko nilibaki nimesimama tu na hapo nikasikia kengere ikilia na wale watu waliokuwa mbali niliwaona wakikimbia kuelekea huko kengere iliposikika, nilijaribu kumgusa mmoja mmoja nimuulize lakini haikueezekana kila nilipofikisha mkono walionekana ni kama upepo, "Njoo nifate huku" sauti ya kike ilisikika kisha akanishika mkono niligeuka  na kumtizama alikuwa ni binti mmoja hivi mweupe mrefuu sana na mwenye meno meupe ya kuvutia na rangi ya kiini cha jicho lake yakiwa ya bruu, "we ni nani??" nilimuuliza, aliniangalia kidogo alafu akajibu "kuwa huru Faraja" nilishtuka kusikia mtu yule wa ajabu akilitaja jina langu..

ITAENDELEA,...........



No comments: