SIMULIZI:- ZINDUNA; (malkia wa majini) SEHEMU YA {02}






SIMULIZI:-
ZINDUNA;
(malkia wa majini)
SEHEMU YA {02}

         Endelea..........

ILIPOISHIA..
  "Tuliishia pale ambapo Faraja akiwa ameangukia katika ulimwengu tofauti na huu wa Dunia huku akishangazwa na miundombinu iliyojengea Taifa hilo la ajabu, akiwa hana hili wala lile aliikuja binti ambaye hakujitambulisha binti yule ilionyesha ni mwema sana na kilichomshangaza zaidi Faraja ni pale binti yule alipomtaja jina lake..

ENDELEA NAYO👇👇👇👇
 nilibaki nimesimama bumbuwazi limenipiga nikijiuliza "hii ni dunia gani hii jamani! amenijuaje jina langu" nilizungumza kimoyo moyo huku miguu ikianza kutetemeka kwa hofu kubwa, lakini binti yule alisema "nakujua muda mrefu tu faraja mtoto wa mvuvi, mtoto uliyepatikana kwa tabu nyingi mpaka mama yako kukupa jina la Faraja ili liwe linawafariji kila watapokuwa wanakuona, jina lako lilikuwa likimfariji baba yako hasa akikumbuka miaka kumi alivyoteswa na jini" bado binti yule alizidi kunitia presha na jamba jamba moyoni, nilipata na shauku ya kumuuliza kiundani zaidi, "inaonekana unaijua vizuri sana familia yangu eti??" nilimuuliza huku nikimkazia macho na masikio yakiwa madhubuti kulisubiri jibu la binti huyo ambae sikumfahamu hata alipotokea.. "haahah eeeh!! story yote kuhusu wewe naijua hata ya wazazi wako kwani mimi ni........" kabla hajajitambulisha kengere ilipigwa tena aliposikia sauti ile ya kengere alishuka chini na kugusisha paji lake la uso chini kwenye mchanga mlaini uliozunguka maeneo yale, na baada ya muda kama sekunde kadhaa aliinuka na kusema "Inatakiwa twende kuleeeee!! umepaona kule??" aliniuliza huku akinisonteshea kwa kidole chake cha shahada "ndio nimepaona" nilimjibu "kule ndio unatakiwa kwenda kuishi sasa kwani  leo ndio siku anaapishwa mtawala mpya wa majini" alisema yule binti "niiiini majini??? inamaana nipo kwenye ulimwengu wa majini???" nilimuuliza kwa mshituko mkubwa kufatia kile alichokisema "Ndio na mimi ndio suleyha nitakuwa mtumishi wako kila wakati" alisema binti yule aliejitambulisha kwa jina la suleyha, nilishtuka sana kupata habari hizo moyo ulinidunda kwa kasi nikimtazama binti huyo na habari alioisema yani hata likuwa haingii akilini kabisa "we usinichanganye bwana mi ni binadamu wa kawaida nitaweza vipi kuishi na majini?" nilimuuliza suleyha "binadamu sio wewe tu kwenye ulimwengu huu, binadamu wapo wengi sana" alinijibu suleyha "wako wapi??"nilimuuliza kwa shauku ya kutaka kujua huenda nikawaona marafiki zangu watatu tuliozama nao na mtubwi kabla sijaibukia huku kwenye ulimwengu wa majini, "Faraja maswali yako yote utapata majibu muda bado sana" alinijibu suleyha, "ila sasa huko ni mbali tunaendaje kwa miguu au kuna usafiri??" nilijikuta nikiuliza  huku macho yote nikiwa nimeyaelekeza kule suleyha aliponisonteshea, "usijari usafiri upo" alinijibu kisha akanivuta mkono na kunikumbatia kifuani mwake, "shikilia vizuri usije ukaanguka" alisema suleyha "ok ok, " nilimjibu "usiogope ndio tunaanza safari" alisema suleyha "siogopi" nilimjibu, kisha suleyha akajirusha kidogo juu na zikachomka mbawa mbili kubwa tukaanza kuambaa ambaa angani safari nikulisogelea lile jengo, nilijikuta uoga ukiisha kabisa tukiwa tunaambaa ambaa Angani kulisogelea lile jengo nilimuuliza swali suleyha "kwanini unipeleke kwa huyo mtawala mpya uliosema kuna haja gani na kwanini mimi??" nilimuuliza binti mrembo wa kijini suleyha, "kiukweli sijui kwa kuwa yeye ni kiongozi wetu hatuna budi kutii kile alichokisema" suleyha alijibu, nilibaki kimya tu baada ya kukosa jibu nililolihitaji, tulifika kwenye hilo jengo, jengo lililopangiliwa kwa namna yake kuta za jengo lote zilionekana ni mawe flani ya ajabu yenye kung'aa hapana mfano, "haya ni mawe yanaitwa lulu, hutoa mwanga mkali sana nyakati za jioni na mchana huwa meusi kabisa" alisema suleyha baada ya kuniona nimezubaa kwa muda nikishang'alia maajabu ya jumba lile, "Yanatokea wapi mawe haya?" nilimuuliza huku nikishika shika moja ya jiwe dogo lililokuwa chini likizagaa zagaa tu, "ni siri ya utawala mi mengine sifahamu kwani cheo changu nikidogo kwenye ulimwenguni huu" alijibu suleyha "Sawa suleyha tumeshafika ndio hapa,.. Sasa mbona amna mlango wala dirisha tunapitia wapi?" nilimuuliza suleyha, alicheka suleyha kisha akasogea karibu na ukuta kulikuwa na kengere ndogo hivi ikining'ia aliipiga kisha akarudi hatua mbili nyuma na kusimama akielekea kwenye ule ukuta huku akiongea maneno ya ajabu ambayo sikuyaelewa maana yake au hata kuhifadhi neno ingalau moja, alipomaliza tu kuongea yale maneno yake ile kengere ilijipiga mara mbili mfululizo na baada ya hapo ulitokea mwanga flani hivi uliojizungusha kwenye ule ukuta na hapo hapo ikaonekana njia ya kuingilia ndani ya ule mjengo, "Tayari Faraja karibu kwenye dunia mpya" alisema suleyha na kunishika mkono kisha tukaingia ndani ya jengo lile la ajabu, kuta za ndani za jengo lile zilikuwa tofauti na za nje kwani kuta za ndani zilikuwa zimechorwa picha za watu wenye maumbo mawili yani samaki mtu (mermaid au nguva ukipenda), nilitembea nikishangaa uzuri wa jumba lile lililotawaliwa na harufu nzuri za kuvutia, walikuja majini wengine walionipokea na sukeyha aliongea nao kwa lugha yao nisioijua! kwa maana hakuna nilichokielewa zaidi niliona wale madada wakijini waliovalia mavazi yao meupee huku kichwani wakiwa na vidani vya rangi ile ile nyeupe wakinishika mikono kuniongoza njia lakini kabla hatujafika mbali suleyha alisema "kumbukeni malkia anamsubiri" nilishtuka malkia ananisubiri kivipi kutolewa sadaka au vipi? nilianza kujirusha rusha ili niwatoke wale majini wawili mmoja akasema "Tulia kijana yapo mema yanakuja"

         Itaendelea..........

JAMANI EEEH!! YAPO MEMA YANAKUJA
HIVYO USIACHE KUWEKA MB MAANA Mmh.........
#BAKI____NA__MIMI



No comments: