SIMULIZI:- ZINDUNA; (malkia wa majini) SEHEMU YA {03}





SIMULIZI:-
ZINDUNA;
(malkia wa majini)
SEHEMU YA {03}


          Endelea........

TULIPOISHIA..
 Tuliishia pale ambapo faraja akichukuliwa na majini wawili kutoka mikononi mwa suleyha na kumpeleka sehemu nyingine, huku hofu na mashaka kwa Faraja zikimtanda,

SONGA NAYO..
 niliona kabisa wazi kuwa suleyha ameniuza ameniingiza kwenye domo la mamba kwani kila nilipojaribu kuwauliza wale majini maswali kuhusu wanaponipeleka walikuwa kimya tu, sikuwa na jinsi ya kufanya kujiepusha nao zaidi ilibidi niwe mpole nifate sheria zao kokote wanapotaka kunipeleka acha wanipeleke, Tulitembea sana kwenye jumba hilo lenye ramani ngumu kuikalili kwani kilichonifanya niugundue ugumu wake kwa haraka ni milango yake ilivyokuwa mingi yani tulikatiza mlango huu tunaibuka mlango huu yani alafu yote ilikuwa inafanana hakuna mlango hata mmoja uliokuwa tofauti na milango mingine, tumefika sasa alisema jini mmoja aliekuwa amenishika mkono wa kulia niligeuza shingo na kumtazama nae alinitazama pia, nikapuuzia kile alichokisema na kuendelea kuutazama mlango mmoja ambao tulikuwa tumesimama nje yake, "vua nguo" yule jini  aliongea kwa sauti ya kuamuru, "eeeh! hapana bwana yani nivue nguo kwa hiyo nitembee uchi??" niliuliza "Hutembei uchi Faraja we vua nguo tukakuoshe upendeze uende chumbani kwa malkia" jini yule wakushoto alionyesha upole kwa kunijibu taratibu tu. "sasa sijaona hata maji alafu mnataka nivue nguo hapana mnataka mnibake au maana sijawaelewa mpaka hapo??" bado niliendelea kutia ngumu, "ona faraja hiki chumba unachokiona ndani yake kuna bafu na bafu hili huwa hawaingii majini wa kawaida mpaka wale wenye vyeo vikubwa serikalini na malkia ametuambia tuje kukuoshee huku" jini yule alisema jambo lililozidi kukichanganya kichwa changu "mara nahitajika na malkia, mara bafu hili linatumika na watu wenye heshima zao kwenye serikali yao ya majini mimi na hawa majini ninamktaba nao gani mpaka wanitendee yote haya?" nilijiuliza bila kupata ufumbuzi,
         ★★★★★★★★★★★★

Baada ya kufikiri kwa muda mrefu niliona haina maana kujifanya ngarambe sehemu zenyewe hizo sizitambui nilijiamulia nitii tu sheria kwa kile watachokisema nami nitafatisha kuyaokoa maisha yangu huku nikifanya mpango wa kujua njia ya kunirudisha kwenye sayari yangu ya dunia,

Mlango wa chumba kile ulifunguka na kisha wakaniamuru niingie ndani, niliingia huku nikiwa uchi nguo zote nilizivua na kuziacha pale mlangoni, niliambatana na hao majini wawili, tulipoingia tu ndani lango lilijifunga na mwanga mweupe ukakiangazia chumba kile nakiri tokea niishi duniani sikuwahi kuona vitu vizuri kama vilivyokuwa kwenye chumba kile, mbele kidogo kulikuwa na baseni flani kubwa la kuogea lililopambwa vizuri na kujazwa maji hadi juu, beseni lile lilivutia hasa marembo yake ya dhahabu mixer pamoja na vitu vingine ambavyo sikuvitambua kwani duniani vitu vile sikuwahi kuviona katu, nikiwa uchi wa mnyama bila aibu nilijisogeza kwenye beseni lile na kujiingiza, kisha wale majini wawili nao wakachojoa nguo zao na kubaki Bila nguo kabisa, kitendo kilichonishangaza sasa ni pale Sikuwa na Hisia kabisa hari ya kuwa wale majini walikuwa Awana Nguo zao kabisa ila sikulitilia maanani sana sijui nilikuwa nimerogwa! maana kila jambo lililokua linaendelea mule niliona ni kawaida tu, mmoja kati ya wale wawili aliingia ndani ya lile beseni huku mwingine akiwa kwa nje akianza kuniosha taratibu, maji yaliyokuwa kwenye beseni hayachoshi kabisa kutokana na harufu yake nzuuuri ilionukia kama mdarasini mchnganyiko na iriki na kikubwa zaidi kilichonivutia ndani ni uvugu vugu wa yale maji kiufupi nilijikuta nikianza kuisahau dunia yangu, warembo wale wa kijini wenye chuchu ndogo kifuani waliendelea kuniosha taratibu kwa mtego laini kabisa usio chubua wala kuumiza ngozi, ukimya uliendelea kukizunguka chumba kile jambo lililonisukuma niulize kitu kwa yule jini aliokuwa akinisugua miguu, "sawa! yote nimeshakubali mnifanyie mnvyotaka ila kwanini mnipeleke kwa huyo malkia wenu?" niliuliza kisha nikakaa kimya kusubiri jibu kwa yeyote kati yao atayejisikia kujibu "wewe ni hitaji la malkia Zinduna kwa maana tokea ukiwa mdogo ameishi kukufatilia maisha yako, na hata ile sehemu ya kuvulia samaki yeye ndio alitenda yote hayo mpaka ukawa unapata samaki wengi" jini yule mkarimu alijibu "inamaana Faraja tokea zamani anawindwa na jini??" niliuliza tena "ndio Faraja wewe umekuwa kipaumbele sana kwenye kichwa cha malkia wetu Zinduna hata kabla hajaapishwa kuwa malkia" aliendelea kunitolea ufafanuzi, nilibaki kimya kwa majibu ya yule mrembo niliona yanatosha kwa maswali mengine nikikutana na huyo malkia wao nitamuuliza yote, "sawa we nirafiki bora sana kwangu kwa kipindi chote" nilisema nae akanijibu "ahsante " "nikuite nani??" nilimuuliza tena "niite salhat" "na mwenzio" "Anath anauwezo wa kuisikiliza nafsi yako ukizungumza" alijibu binti mrembo wa kijini salhat,
        ★★★★★★★★★★★

waliniosha vizuri tena taratibu na kuyang'arisha makucha ya vidole vyangu vya miguuni na baada ya hapo tulitoka na kwenda kuingia kwenye chumba kingine cha urembo kisha wakaanza kunipaka mafuta mwili mzima wakanichana nywele vizuri, mwili mzima ukatiliwa manukato yenye harufu nzuri hamna mfano na baada ya yote walinivisha mavazi mazuri kabisa ya heshima, kwa maisha ya kibinadamu mavazi yale yalimstahiki mtu mwenye cheo cha ufalme duniani, kisha wakanivisha kofia nzuuri iliyoundwa kwa dhahabu tupu, "vyote hivi ni vyangu jaman??" mpaka nilishangaa nikajikuta nauliza tu sio kwa thamani ile nilioipata kwenye ulimwengu ule wa majini, baada ya maandalizi yote, walinichukua na kuanza kunipeleka huko ambapo walisema ndio malkia yupo ananisubilia, tulitembea kwa mwendo wa madaha huku salhat na anath wao wakiwa pembezoni mwangu wakinisindikiza kama bwana harusi, kila hatua tuliyoikanyaga kukikaribia hicho chumba ambacho nilianza kukiona kwa mbali chini ya sakafu yake ilipotua hatua ulionekana mwanga yani kwa kila hatua, yani jamani sikuwahi kuona kokote kule duniani miujiza kama iliyopo ndani na nje ya jengo lile, tulifika sehemu hiyo hapo niliona jeshi kubwa la majini likiwa tayari kunipokea huku wakiwa na siraha zao pamoja na ngao, walianza kupiga zile ngao zao kwa pamoja kwa kutumia panga zao huku majini wa kike nao walipangwa kunilaki walianza kurusha mauwa wakati huo namsogelea huyo malkia wa majini ambae nimesikia amenisubiria kwa muda mrefu, tamaa ya moyo wangu na shauku ni kumjua huyo malkia wa majini, kwa mbali taswira ya sura yake ilianza kusogea karibu hakika ni mfano wa malaika kwa uzuri alionao binti yule kwani tokea mwanzo nilifikiri kuwa huyo malkia atakuwa ni mkubwa sana au mzee kabisa lakini kwa lile nililo liona ilinibidi niongeze mwendo kuwahi pale mbele nimuone vizuri malkia huyo wa majini. kadiri nilivyozidi kumsogelea ndio uzuri wa binti huyo ulizidi kunishawishi haswaa!! nilifika mbele yake huku macho yangu yote yakiendelea kumkagua kila sehemu ilionekana, shangwe na vifijo vilizidi kuongezeka hasa pale malkia alivyosimama na kunisogelea pale nilipo simama kama sanamu nisiejielewa kabisa, "Sema chochote unachotaka mfalme wangu" malkia alisema kwa sauti yake nyororo!!

JE FARAJA ATAOMBA NINI?? AU ATAOMBA ARUDISHWE DUNIANI???

Itaendelea.........

#BAKI__NA__MIMI



No comments: