SIMULIZI:- ZINDUNA; (malkia wa majini) SEHEMU YA {04}




SIMULIZI:-
ZINDUNA;
(malkia wa majini)
SEHEMU YA {04}


         Endelea......

ILIPOISHIA..
Tuliishia pale ambapo Faraja alipofikishwa mbele ya umati mkubwa wa majini huku muda huo akimuona malkia wa majini Zinduna mwenye uzuri wa namna yake, mwisho tuliona Faraja akipewa ombi achague chochote anachokitaka basi malkia Zinduna atatimiza bila ajizi..

SONGA NAYO......

"kichwani yalinijaa maswali mengi, nilijiuliza nimuombe nini ambacho sina kila nilichokifiria akirini mwangu kilikuwa hakikai kabisa "ninavyo vingi vya kumuomba sijui hata nimuombe nini? au nimuombe anirudishe duniani, hapana duniani huko maisha magumu nitaishi kwa kuvua samaki hadi lini huu ndio wakati wa mimi kulitumikia taifa la majini naimani ipo siku nitatoka kwenye ulimwengu huu ingawa siijui njia" niliendelea kujiuliza mwenyewe na kusahau kabisa kama hapo mwanzo nilipewa ombi na malkia Zinduna, alinishtua kwa kunigusa kwa kidole chake hapo ndio fahamu zikanijia na kulikumbuka swali lake haraka nikamjibu kwa sauti ya kawaida tu "Nataka niwe mtu huru kwenye ulimwengu huu" nilimjibu huku nikiendelea kuutathimini akirini mwangu uzuri wa malkia Zinduna, alicheka malkia kiasi akarudi nyuma nakuchukua kitezo  kimoja cha dhahabu kiliokuwa kinafukishiwa ubani akasogea nacho mpaka maeneno niliposimama kisha akapanda jini mwigine aliekuwa ameshika kidude hivi kilichofunikwa uzuri sikukijua kitu kile ni nini hata alipopanda jini yule mi yangu macho yalibaki kukikodolea kidude kile "haya ifungue" malkia Zinduna alimuamuru yule kijumbe aliekuwa na kile kifaa, alikifungua na alipokifungua Malkia Zinduna alichukua kitu kingine kilichokaa kama farasi ni kama mdori hivi wa kuchonga ila tofauti yake na midori mingine huo ulikuwa ni wa dhahabu hakuna kitu ndani ya jumba lile kilichopambwa bila dhahabu kiufupi nilijikuta nikilipa jina la jumba lile ni Jumba la dhahabu, malkia Zinduna baada ya kukitoa kile kimdori alinisogelea pale nilipo huku kitezo akiwa amekishika na kumkabidhi yule jini "sikia hii ni tufu! muhuri wa kijini nakuweka muhuri kwanzia leo uwe ni miongoni mwetu ukiwa na muhuri huu utapita sehemu yeyote ile na hakuna mtu yeyote atakayeweza kukudhibiti, tufu hii ni kwa ajiri ya watu maalumu tu na wenye dhamana na hii tufu" alisema malkia Zinduna kisha ile tufu akaizungusha mara mbili kwenye ule moshi wa ubani kisha akanibandika nao kwenye paji la uso ambapo ilitokea alama ya kung'aa malkia alinishika mkono tukawageukia wale wajini wote kisha akasema "Kwanzia leo Faraja ni mmoja wetu sitaki kuona wala kusikia manung'uniko kwa yeyote yule, naomba mumpenda mumjari kama vile mnavyojaliana nyinyi mkiona kuna jambo kakosea mje mnione mimi na sio kufanya uamuzi mkononi sawa!" malkia alimaliza kwa kuwauliza kwa heshima na utukufu wa malkia Zinduna wote walishuka chini na kupiga paji zao za uso mara tatu taratibu ikiwa ndio kama utamaduni wao kwa pamoja tena wakasimama na kusema "sisi ni watumishi wako wa milele tunapokea na kutii kile utachosema eeh!! malkia Zinduna" walisema maneno yao ya ujasiri yaliyonifanya nifarijike na kujiona sasa sitakuwa mpweke kwenye ulimwngu huo wa majini.. "umesikia.?? kuwa na amani" malkia alihitimisha maongezi yake kisha akaniamuru nirudi kwenye swafu nisikilize licha ya kuwa kiti cha mfalme kilikuwa wazi, nilisimama kwenye swafu lakini matamanio yangu yote yakikielekea kile kiti cha dhahabu akaliacho mfalme, "inamaana malkia Zinduna hana mume? eeh! hana msaidizi wake hapo wa kukikalia hicho kiti? huenda sasa ikawa bahati yangu kukikalia hicho kiti" nilizingumza kwa nafsi huku nikiendelea kukikata jicho kile kiti cha mfalme,
         ★★★★★★★★★★★★

"hiyo siku iliisha niliweza kupewa chumba cha kulala peke angu bila kuwa na msaidizi yeyote na nje ya chumba changu waliwekwa malinzi watiifu kabisa wa malkia Zinduna, kuimarisha ulinzi ili nisije kubughudhiwa na majini wenye roho mbaya, asubuhi yani hata sijui ilikuwa sangapi ila nahisi tu ilikuwa asubuhi nilipoamka nilikuta vyakula tayari vimeshaandaliwa mezani, jambo la kwanza kabisa nilichukua maji na kusukutua kwanza kinywa alafu ndio nikasogea mezani nipate hiyo chai ya kijini kilichonishangaza zaidi maandalizi ya chai ile hayakuwa tofauti kabisa na chai niliokuwa nainywa duniani "inamaana hawa majini wanakunywaga chai na wenyewe?" nilijiuliza baada ya kuionja ile chai ilinakshiwa kwa iriki karafuu na mdarasini, baadae niliona ni ujinga kujiuliza uliza maswali yasiyo na maana mwishowe nishindwe kunywa chai bure, nilikaa kimya nikaendelea kupata chai na baada ya muda kwa kukadiria ni kama dakika kumi hivi alikuja suleyha binti alienifikisha ndani ya jengo hili la dhahabu "naona umemka sasa Faraja" suleyha aliuliza huku nae akivuta kiti na kujiunga nami mezani "ndio jana nilichoka sana mlinizungusha sana kwenye jengo lenu hili" nilimjibu suleyha "aah!! pole sie wenzako hatuchoki tunafanya kazi usiku na mchana tunasafiri kama upepo kwenda tutakapo yani kiufupi hatuna muda wa mapumziko" suleyha alinijibu vizuri tu huku akinitazama machoni, macho ya binti yule mwenye kiini cha blue mpauko kila nilipokuwa nikiyatazama kuna kitu kilichokuwa kinaingia rohoni na kunitekenya kitu kile sikukijua nini, "ilaa!! ok sawa samahani suleyha naomba niulize swali kidogo kama hutojari" nilimuomba suleyha anipe nafasi nimpachike swali, nae suleyha bila hiyana alisema "kuwa huru nipo kwa ajiri yako" nilikaa kimya cha muda mfupi kisha nikajikoholesha na kumuuliza "Hivi Malkia Zinduna ana mume?" nilimtazama suleyha atoe jibu ila alionekana mdomo wake kuwa mzito kunijuza kuhusu hilo badala yake anasema "usije ukaniuliza tena kuhusu  malkia sawa??" alijibu kwa kuonyesha dhahiri hajafurahia kile nilichomuuliza, "sawa kama nimekuudhi naomba nisamehe" nilikuwa mpole, licha ya hivyo jibu la suleyha lilinitia shaka kujibu kwake alionyesha ni kama mtu alienawivu ndani yake, anyway isiwe tabu niliendelea kunywa chai yangu na baadae tukawa tumetoka, siku hiyo kulikuwa kumefana shamla shamla mbali mbali ziliendelea kwenye ulimwengu ule kama kawaida yangu nikiona kitu huwa sikifumbii mdomo nilimuuliza suleyha "suleyha mbona leo nje pamechangamka sana kuliko hata siku tuliyopita?" 
"leo wanasherehekea miaka kadhaa ya utawala wetu baada ya kuutoa kwenye utawala wa mabavu kwa majini waliotangulia" alinijibu suleyha "mh! na nyie huku kuna majini wanaowatawala kimabavu?" nilimuuliza "ndio wapo maruhani wabaya ambao wao husabisha maafa kila watapokuja kwetu Uwauwa kina mama watoto wadogo bila huruma" alisema suleyha "hee!! bado wanishangaza na nyie mnakufa na kuzaliana?" nilimuuliza suleyha ili nitambue undani wa majini "ndio! tunakufa tunaoleana, tunazaana na baadhi ya mahitaji kama ya duniani mwanamke wa kijini anayapata ikiwemo kupenda, kuolewa na kuachika" alijibu "mh! sawa kwa hiyo hao maruhani uliosema wao wanaishi wapi?" nilimuuliza "kiukweli hilo silitambui" alijibu suleyha "dah! yani nafurahi sana kuambatana na wewe kila hatua yangu  yani siijuitii kabisa" nilisema "hata mimi style yako ya kuuliza usilolijua imenivutia sana" alisema suleyha. tulizunguka sana siku hiyo nikiiona milki na fahari ya taifa hilo la kijini lililoumbika haswaa!! baadae tulirudi mjengoni huku shamla shamla za hapa na pale zikiendelea, kwa kuwa siku hiyo pia Malkia Zinduna alikuwa akisherehekea pia siku yake ya kuapishwa kwake kuwa malkia, hivyo ilitubidi tujumuike nae kwa pamoja katika chumba kile kilichoonekana ni chumba cha mikutano, majini wote wenye vyeo vikubwa, amiry jeshi, general, waziri mkuu, brigedia meja, pamoja na majini wengine wengi nao walihudhuria kwenye sherehe hizo, sherehe zilianza kwa moja kati ya jini  kukalibisha wageni wote waliohudhuria baada ya jini huyo aliepewa jukumu la kuwakaribisha wageni kushuka mimbari sasa ilikuwa ni zamu ya mtukufu malkia kusimama aseme neno kwa majini wake, alisimama kisha akasema "kiti changu cha umalkia nimekipata, na kiti kile cha mfalme bado sijamtambulisha mfalme wa kukalia kiti kile, najua itawashtua sana ila kwa leo jamani naombeni nimtaje mbele yenu na ikibidi hata leo aapishwe awe mfalme wangu wa kunisaidia majukumu mbali mbali ya kitawala" malkia Zinduna alisema, majini wote walitoleana macho wakisubiri kusikia na kuona huyo atakae chaguliwa na malkia, malkia alianza kumwangalia mmoja mmoja hakufika mwisho akasema "nakuhitaji Faraja wewe ndio uwe mfalme wangu" ebwana eeeh!! nusu moyo upasuke kwa mshituko niliopata kusikia jina langu likitajwa mbele ya halaiki ya majini lakini kabla sijasimama kusogea mbele ilitoka sauti kati kati yetu ikipinga uamuzi wa malkia kwa kusema "HALIWEZEKANI JAMBO HILO"

#Yapo_Mema_yanakuja#

        Itaendelea.........

ila tu usisahau
#KUBAKI_NA_MIMI



No comments: