SIMULIZI:- ZINDUNA; (malkia wa majini) SEHEMU YA {05}





SIMULIZI:-
ZINDUNA;
(malkia wa majini)
SEHEMU YA {05}


              Endelea........

ILIPOISHIA..
"Tuliishia pale ambapo malkia Zinduna aliposhangaza jopo la majini kwa kumchagua faraja kuwa ndio awe mfalme wake wa kukalia kiti cha mfalme kilichopo wazi, lakini muda huo iliibuka sauti ya kiume kati yao ikipinga uamuzi ule wa malkia,

ENDELEA NAYO......

##,,Kila jini aligeuka na kumtazama jini huyo alieipaza sauti kabisa mbele ya viongozi wakubwa wa kijini nami nilimuangalia vizuri jini huyo wa kwanza kupinga, alisimama jini yule  aliekuwa amevalia kanzu nyeupe na kichwani akiwa amefunga kiremba kikubwa sana ukimtizama kwa haraka hana tofauti na singa singa wale tunaowaona kwenye filamu za kihindi. "MALKIA HAIWEZEKANI KABISA KUFANYA HILO" alirudia kauli yake ile ile ya mwanzo kuonyesha msisitizo mkubwa, "MBONA IMESHAWEZEKANA! WEWE UNASEMA HAIWEZEKANI?" malkia Zinduna aliuliza "Haiwezekani sisi majini tupo chini yako tumefanya kazi zote ulizotuomba tumetimiza, tumelinda mipaka na kila jambo ulilolisema mtukufu malkia tulilitimiza iweje leo aje kiumbe mwanadamu atutawale? mtu asiekuwa na uwezo hata wa kushika panga apambane ndio umpe cheo cha ufalme hapana malkia utakuwa umetukosea sana majini wote" jini yule wa kiume mwenye umbo kubwa alitoa maelezo yake akitoa na sababu yake ya moyoni iliomfanya apinge uamuzi wa malkia. "Jamani maswala ya kazi hayahusiani kabisa na mapenzi mimi ndio mwenye mamlaka ya kuchagua chochote kile nikipendacho si chaguliwi na yeyote kati yenu" nae malkia Zinduna aliweka mkazo upande wake akionyesha wazi kile alichokisema hatanii kabisa.. marumbano  yalianza huku pande zikiwa mbili zikijitenga yani upande waliokubali mimi niwe mfalme na wengine walipinga vikari hawataki kutawaliwa na binadamu wakati majini wapo wenye uwezo mkubwa  wa kujibadirisha maumbo zaidi ya elfu, "Malkia tengua kabisa maamuzi yako lah! si hivyo kutazuka balaa humu ndani" Mtoto wa waziri mkuu alisema baada ya kuona fujo zinazidi kuwa kubwa, malkia alikaa kimya kiasi na baada ya hapo alimuomba kila jini aliehudhuria hafla hiyo atulie atoe uamuzi uliosawa kabisa, "Mimi ndio mtawala kwa sasa namaamuzi ya kutenda lolote lile, nauwezo wa kumfukuza kazi yeyote yule kama tu hatotii kile ninachokisema, kwa leo ngoja tuliache hili swala kama lilivo ila siku yeyote ile nitarudia tu kulitenda hili hili na siku hiyo siitaji maoni wala ushauri kwa kiumbe yoyote niacheni na maamuzi yangu baass!!" Malkia Zinduna aliongea kwa ujasiri mkubwa kama kiongozi mwenye msimamo wake alidhihirisha wazi wanawake sio watu wakukaa jikoni tu kupika hata wao wanauwezo wa kuviongoza vichwa vya maelfu ya watu, kwa maneno mazito ya malkia upande uliomkubali zaidi ulinyanyuka na kupiga makofi mengi huku wakisema "uishi maisha marefu mtukufu malkia, uishi maisha marefu mtukufu malkia", upande uliompinga malkia Zinduna walianza kunyanyuka huku wakiniangalia kwa jicho la husuda jicho baya hamna mfano, mmoja alijidhihirisha kabisa aliposema "Wewe nitakuonyesha" alisema jini yule kwa masikio yangu na macho yangu nilielewa kabisa jini yule ameijenga chuki kabisa, baada ya wale majini wakorofi kutoka na kuliacha kundi la majini waliokuwa wakimtii malkia Zinduna, nilisimama nakumfata pale mbele malkia ingalau nimpe neno moja, malkia alinitizama mpaka pale nilipomfikia "Lakini malkia..!" kabla hata sijaikamilisha sentensi malkia Zinduna aliniziba mdomo kwa kidole chake cha shahada huku akithibitisha kwa ulimi "shiiiiiiiii!!! kaa kimya kabisa nimeshayasoma mawazo yako kitambo" alisema malkia na kumuita suleyha aje anitoe pale mbele anirudishe chumbani mwangu, "mpeleke chumbani mwake na uhakikishe hatoki nje maana sasa atakuwa hatarini" malkia alimpa maelezo suleyha "napokea na kutii maagizo yako mtukufu malkia" suleyha alionyesha utiifu mbele ya malkia Zinduna kwa kuinamisha shingo yake na kuinyanyua,
       ★★★★★★★★★★★★

tulitoka kwenye chumba kile nikiwa nae Suleyha, tukiwa njiani kuelekea kilipo chumba changu suleyha alionekana  amebanwa na jambo fulani moyoni mwake ila alikuwa anashindwa kuliweka wazi "suleyha sio kawaida yako kutembea ukiwa kimya kiasi hiki, hutaki leo kuongea na mimi hata huniangalii tatizo nini?" nilimuuliza suleyha, lakini hakunijibu zaidi aliongeza mwendo tu nilimtazama suleyha ila sikumwelewa kabisa ana maana gani kutenda yale, "suleyha mbona hivo umekuwaje leo?" nilimuuliza lakini bure suleyha hakutaka kabisa kukifumbua kinywa chake kunijibu, haya! niliona isiwe tabu huenda kuna jambo nimemkwaza au vipi tulikaliana wote kimya mpaka pale tulipofika kwenye chumba changu, baada ya kunifikisha salama suleyha aliondoka nakuniacha nikiwa ni mwingi wa mawazo na kilichoniumiza zaidi kichwa ni swala la kuwa mfalme yani nitawale majini nikirudi nyuma tena kufikiria wale majini walivyopinga vikari yani nilikuwa nachoka "Hapa inaonekana itakuwa kazi ngumu kukipata kile kiti cha ufalme, malkia Zinduna ananipambania ili niweze kukikalia kiti kile changamoto nazo ndio kama vile hivi kweli nitakikalia? sijui tu kama itawezekana kama wameanza mgomo hata sijakikalia na jee nikikikalia si ndio vita kabisa? mmh!! lakini mimi ni binadamu tu sijui niwaachie wenyewe? aah!! yani hadi kichwa kinachoka sasa!" nilizidi kuyapanga maswali kichwani mwangu nikikifikiria kiti kile cha kifalme,

UPANDE MWINGINE....

baada ya wale majini waliopinga kutoka kwenye ile hafla huku wakiwa wamefura kwa hasira walikutana sehemu moja na wao wakakaa kikao chao wakipanga njia na namna watazotumia au watayoitumia kumdhibiti Faraja. mwenye kiti wa kikao hicho alianza kwa kusema "Tambueni kwamba sisi ndio watu pekee tuliosalia kwenye kabira letu la Aturu, ili tupate mazazi mema yatupasa tukipambanie kiti kile cha kifalme ima kwa damu, ima kwa siasa tusikubali kiti kile kwenda sehemu yeyote" alisema mwenyekiti wa kikao ambae ndio alikuwa mzazi wa yule jini aliezisha marumbano kwenye sherehe, "ndio baba umesema kweli, inatakiwa katika sisi apatikane mtu wa kukimiliki kile kiti akishakimiliki atamuua malkia na malkia akishakufa atachagua mwanamke wa kabira letu na utawala utakuwa chini yetu" alisema, mmoja tena alipinga "hapana kumuuwa malkia sio njia nzuri kiusalama mtaliingiza taifa letu kwenye hali mbaya maana malkia anawafuasi wengi na sio wafuasi tu hata ulinzi alionao ni mkubwa na walinzi wake wamebobea wameshiba mafunzo yote ya kivita, sasa sisi hatuna jeshi la kusema tumpige malkia jeshi hilo hatuna kabisa, hivyo! kwa ushauri wangu tumpige kisiasa asiweze kumpa kiti kile yule binadamu" yule jini aliongea point sana na majini viongozi wa kabila lile walitingisha kichwa ishara ya kukubalina na wazo la jini huyo, mipango yao nikuhakikisha binadamu hapewi kile kiti kabisa wao ndio wanataka kuweka matunda katika ufalme ili ukoo wao usipotee!!..
        ★★★★★★★★★★★★

Siku moja ilipita tokea lile sekeseke litokee nae suleyha alikuwa kimya tu, asubuhi hii aliponiletea chai nilichoka kuvumilia hali ile niliomuona nayo suleyha moyo ulinisukuma kutoka hapo nilipokuwa nimekaa na kumsogelea suleyha kisha nikamshika na kumbana ukutani ndani ya chumba kabla hajafungua mlango kutoka nje "Nambie suleyha tatizo nini mpaka unikalie kimya kiasi hicho, najisikia vibaya sana kukuona ukiwa katika hali hiyo" nilimweleza suleyha, suleyha badala ya kujibu swali aliuliza swali lililonifanya nichoke niishiwe na nguvu kabisa ya kuendelea kumuuliza swali lingine, suleyha aliuliza hivi "Unampenda Malkia Zinduna?" aliuliza nilishtuka sana na tena sikutegemea swali lile kutoka kwa suleyha nikajipa moyo kisha nikamjibu "ndio kwa sababu.....!!" hata sijamalizia suleyha alinikatisha na kusema "Baaassiii!! inatosha  nimeshaelewa Faraja" alisema kisha akanisukuma mikono yangu na kutoka huku macho yake yakionyesha ukweli wa moyo wake kuwa suleyha kaisha penda.

Naaam!!! Yapo mema huko mbele yanakuja!! usikubari kupitwa na kigongo hiki cha kusisimua

#Hakikisha_UNABAKI_NA_MIMI

ITAENDELEAAAA.



No comments: