SIMULIZI___ZINDUNA (malkia wa Majini) SEHEMU YA {06}




SIMULIZI___ZINDUNA (malkia wa Majini)
SEHEMU YA {06}

           Endelea........

ILIPOISHIA..
"Tuliishia pale ambapo suleyha alipoanza kujionyesha wazi wazi kwamba anampenda Faraja, nae Faraja hakuwa mwepesi kulitambua hilo kama jini suleyha ameshaanza kuufungua moyo yake na mfalme mtalajiwa,

ENDELEA NAYO👇👇👇

"Yani suleyha nashindwa kumuelewa kabisa sasa hivi kanibadilikia sana sio kama siku chache hapo nyuma nilipofika, sijui nimemkosea nini mimi jamani, sasa suleyha akininunia nitaipataje njia ya kurudi duniani maana najua suleyha ndio kila kitu na ndio nahisi yeye ndio mwenye nyaraka za siri kabisa za utawala huu, kwa maelezo yake suleyha tu natambua ni mtu mwenye kuyajua mengi yahusuyo huu utawala kwa ujumla, nitafanya kila niwezalo mpaka nijue njia ya kurudi duniani na nitamtumia huyu huyu seleyha ndio atakaenipa data jinsi gani naweza kuondoka kwenye ulimwengu siku yoyote nitayotaka" nilijisemea kisha nikarudi mezani na kuendelea kupata Kifungua kinywa cha asubuhi (chai)..
       ★★★★★★★★★★★

Usiku wake ulifika siku hiyo nikiwa ndani ya chumba tokea asubuhi kwa maana malkia Zinduna alijua wazi wale majini wasionipenda wangetafuta hila za namna yeyote kuhakikisha wananipoteza kabisa hivyo malkia Zinduna aliweka ulinzi mkali kwenye chumba changu sikutakiwa nitoke nje kuzurura hata kidogo nikiwa na shida kuna kengere ndogo imo mule chumbani niipige na watoa huduma watakuja na watumishi walioruhusiwa kuingia kwenye chumba changu ni watatu tu , suleyha, salhat na Anath, hakuna jini mwingine alioruhusiwa tofauti na hao watatu, huku nje ya chumba kukiwa na ulinzi mkali yani kama chumba kilichohifadhiwa madini mengi, hii ilionyesha tafsiri kubwa ya uhitaji wangu juu ya malkia Zinduna, usiku huo wa sherehe alikuja mjumbe mtukufu wa malkia mwenye kuaminika na kutoa kibahasha kilichopitiwa mlangoni kabla ya kunifikia kikinialika nijumuike usiku huo na malkia Zinduna ndani ya chumba chake, hivyo watumishi wangu watatu walioteuliwa na malkia Zinduna waliniandaa vizuri huku wakinipulizia marashi mbali mbali yenye harufu tofauti tofauti na kuleta muunganyiko mmoja wa harufu nzuri sana, kisha wakaniongoza njia kukiendea chumba cha malkia Zinduna, hatua zote tulizokuwa tukikanyaga kuelekea huko jicho langu lenye ute ute na chembe chembe za mapenzi lilizidi kumwangalia suleyha, wakati suleyha muda huo yeye yuko basy tu kuangalia mbele huku akiwa ameshika kitezo chake, "sijui anashida gani suleyha, sijui Malkia Zinduna ndio amemkataza asinisemeshe? Mmh!! yani hata sijui na mimi kwanini moyo wangu haufurahii kumuona akiwa katika hari hii" kimoyo moyo nilizidi kuongea, tulizipanda floo za jengo lile kubwa huku tukipita kwenye milango tofauti tofauti kama ilivyokawaida ya jengo lile la ajabu, mwisho tulifika floo ya juu ambayo ilitengwa rasmi kwa ajiri ya watu wakubwa wa nchi hiyo ya kijini kuishi tu, na wale majini wa hali za kawaida wao walikaa chini kabisa ambapo nilisikia walinzi waliokuwa wakituongoza njia wakipaita underworld, ulinzi uliopo floo hii sio wa kawaida kwani licha ya kuwa waliishi viongozi wakubwa wa nchi bali hata hazina kubwa za nchi hiyo zilifadhiwa huko hivyo swala la ulinzi kule ulikuwa ni la uhakika, tulifika sehemu mlinzi mmoja akatuambia tusimame, tulisimama sote na yeye alipita mbele na kusonga kwenye chumba kimoja hivi kilichopo mbele yetu chumba kile hakikuwa mbali sana kutoka pale tuliposimama hivyo alivyokuwa anakisogelea kile chumba hata alipokifikia tulimuona vizuri na baada ya muda kidogo alitoa ishara ya mkono ya kutuita nasi kwa pamoja tulianza kumfata, tuliingia kwenye chumba kile ambacho yule mlinzi muda mchache alikikagua, ndani ya chumba kile kulikuwa hamna mlango tena na wala malkia Zinduna hakuwepo hapo nilianza kuwaza "isije kuwa ni mtego nimesetiwa waniuwe" lakini yalinitoka mashaka baada ya kumuona suleyha jini niliemuamini kuliko yoyote kwenye dunia yao hiyo ya kijini, alikita mbele suleyha na kusimama mbele ya ukuta ule kisha akauweka mkono wake wa kushoto kisha na kwa juu yake kulikuwa na kengere ndogo sana aliipiga ile kengere kama mwanzo siku ile ndio naingia kwenye mjengo huo kisha akaongea maneno ya lugha yao ambayo nahisi kabisa ndio maneno ya siri ya kufungulia ile milango, "nimeshaanza kujua jambo moja moja ili kufungua milango ya jumba hili nilazima ugonge kengere kwanza, na pili kuyataja hayo maneno" nilisemezana na nafsi yangu huku muda huo ule ukuta ukiachia uwazi na mlango ukapatikana, baada ya ule ukuta kufungua njia chumba kilionekana kimoja tu na chenye ulinzi mkubwa korido yote kukifikia chumba walipishana walinzi kukilinda chumba kile nilitizama sana huku nikijisemea "Mmh! nimeshafika sasa!! kwa malkia Zinduna" kisha nikaingiza mguu wa kwanza kwenye zulia lililotandikwa mpaka mlangoni mwa mlango wa malkia Zinduna, "wataenda wawili tu na nyie wengine mtabaki hapa kuwasubiri" sauti ya mlinzi mtiifu wa malkia alisema na bila shuruti wote walipokea ujumbe ule, mtumishi alietakiwa kuambatana nami alikuwa ni suleyha, hivyo suleyha akiwa na kitezo chake alinisindikiza mfalme wake mtalajiwa, korido zima tulipopita walinzi wa malkia waliinamisha vichwa vyao kwa heshima kubwa hadi pale tulipoufikia mlango wa chumba cha malkia Zinduna, Tuliingia pamoja na suleyha na kumkuta malkia Zinduna akiwa ameketi kwenye kiti akitusubiria, na kitandani kwake walitengwa vigori gori, mabinti warembo kuwatizama usingechoka harufu nzuri ya chumba kile ukijumlisha na mapambo yani muda mwingine nilikuwa nikirudi nyuma sitamani hata kurudi duniani "ahsante suleyha kwa kuileta asali ya moyo wangu" malkia Zinduna alisema "Napokea na kutii amri yako eeh!! mtukufu malkia" suleyha alimjibu kwa heshima zote nakuthibitisha maneno yake kwa kukiinamisha kichwa, Malkia Zinduna alisimama na kunisogelea sehemu niliposimama kisha akaanza kunitoa jola la juu, huku akinitumbuiza kwa mipapaso flani hivi ya kunitekenya tekenya Mlkia Zinduna alisema "Nimekuandalia zawadi yako mfalme wangu" kwa haraka nilitaka niijue zawadi alioniandalia malkia Zinduna licha ya kwamba niliwaona wale vigori pale kitandani kwake wakiwa wamevalia mavazi hivi mepesi kama ya kulalia huku sehemu kubwa za mwili zikiwa wazi. "zawadi gani malkia wangu??" nilimuuliza kwa shauku ya kuijua hiyo zawadi alioniandalia "Sio leo nitakutunuku hiyo zawadi hapo kesho panapo majaliwa tutaenda kwenye bustani ya mapenzi ndio utaiona zawadi niliokundalia eeh!! mfalme wangu" Malkia Zinduna alisema,.. yote yafanyikayo mbele ya suleyha ndani yake ni maumivu makali kiasi kwamba anashindwa kuudhibiti moyo wake usimwage chozi wakati huo anapoona malkia akinishika shika kimapenzi,
        ★★★★★★★★★★★★

Usiku huo ulikuwa mzuri kwangu baada ya kuionja radha ya majini waliokuwa mafundi kuvitumia viuno vyao, kilichonishangaza siku hiyo na kuniacha na maswali mengi ni uwezo nilioutumia kuwapa burudani wale vigori, wakati mwanzo nilishindwa kunahisia nilipokuwa naoshwa na wale majini waliopewa dhamana ya kunitunza, sikuelewa kabisa pengine nilijiuliza huenda kwa kuwa nilikuwa sijaiozoea hari ya hewa kwenye ulimwengu huo, usiku huo wale vigori nilipewa kama zawadi tu huku malkia Zinduna yeye akikaa kando kuangalia uwezo wangu katika Kakabiliana na tendo la ndoa,. badae malkia alinipa sifa kwa kusema "nimefurahi sana kwa namna unavyo Kabiliana na Tendo la Ndoa na ninaimani wewe ndio chaguo langu kabisa, nenda kapumzike na kesho asubuhi tutaenda kwenye bustani ya Mahaba,.. huko nimepachagua iwe sehemu mahususi kwa ajiri ya kukupa zawadi hiyo maalumu kwako" alisema malkia Zinduna,....

Ni zawadi gani anayotaka kupewa Mh. Faraja na malkia Zinduna,..
 #YAPO MEMA YANAKUJA, Hakika Usibanduke Hapa Wewe BAKI_NA_MIMI

    Itaendelea..............



No comments: