SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {07}
SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {07}
Endelea..........
ILIPOISHIA..
Tuliishia pale ambapo malkia Zinduna alipomuahidi Faraja akisema ipo zawadi nzuri aliyo muandalia, na zawadi hiyo ili inoge zaidi yawabidi wakapeane wakiwa katika bustani nzuri ya mahaba.....
ENDELEA NAYO..
"Baada ya maongezi ya muda niliachana na malkia kisha nikatoka nje na kuwakuta walinzi pamoja na watumishi wangu wakiwa nje wakinisubiri, tulianza safari kurudi floo ya chini ambako ndio kunachumba kilichoteuliwa kwa ajiri yangu, tulirudi hadi kwenye chumba changu na baada ya kufika walinzi wote walibaki nje na suleyha pekee ndio alieingia ndani kunisafisha mwili. kama ilivyokawaida nilivua nguo zangu kisha nikaingia kwenye lile beseni kubwa la kuogea, muda wote Suleyha alikuwa mnyonge tu jambo ambalo lilikuwa linausumbua sana moyo wangu kila nimuonapo suleyha akiwa katika hali ile, hakuvua nguo alichukua mtego na kuulowanisha akahakikisha unashika povu zito kisha taratibu akaanza kunisugua "Umefarijika Faraja kwa zawadi ya malkia Zinduna?" hapo suleyha alifumbua kinywa chake tena na kuniuliza swali, "yeah!! kwa kua malkia Zinduna amekuwa akinijari sana sina budi kumshukuru tena" nilimjibu "mfano ikitokea akaja mrembo kabisa katika majini wetu akazieleza hisia zake kwako utampokea na kumuelewa?" suleyha aliongezea swali katika swali lake la kwanza, nilikaa kimya kwa muda mfupi kisha nikamjibu "Inategemea sasa na upendo wake maana huku sio katika ulimwengu wangu asije jini akaniingiza katika mtego kigezo ikawa mapenzi ili aniangamize, mi bado ni binadamu tu hata kama malkia amenipiga muhuri wa kijini ila asiri yangu mimi ni ya kibinadamu, tofauti kabisa na nyie, nyie mungu kawaumba kwa moto, na sisi binadamu katuumba kwa udongo sasa hapa itakuwa ngumu kumwamini, ambae kidogo moyo wangu unamuamini ni malkia Zinduna" "kwa maana hiyo mimi huniamini??" suleyha aling'aka baada ya kuona nimemtaja malkia tu wakati na yeye ana msaada mkubwa kwangu, nikashtuka suleyha alipoutupa mtego kwa hasira ndani ya beseni lile na kusogea pembeni kabisa kisha akakumbatia mikono yake, "shida nini suleyha mbona umekuwa na hasira sana kila ninapomtaja malkia?" nilimuuliza suleyha baada ya kuwa ameonyesha kiburi cha wazi wazi "lakini Faraja kumbuka na mimi nina umuhimu kwako sasa unaposema mimi huniamini sijisikii vyema kwa hiyo sihitajiki sasa kuendelea kukutumikia, nitafanya vipi kitu na mtu asieniamini??" suleyha aliongea kwa uchungu kitendo kilichonifanya nigundue kweli nimemkosea kwani bila binti huyo nisingeweza kufika ndani na kumjua malkia Zinduna hivyo nilishuka chini ili nimliwaze binti huyo mrembo katika warembo wa kijini, "Nisamehe mpenzi nilikuwa sijamalizia sentensi yangu wewe umenitakishia njiani tu,wewe jiulize nitaanzaje kuacha kukuamini suleyha wangu?" niliongea kumfariji binti huyo ambaye kiukweli ndio aliyejitoa kimasomaso kwangu kwa kila jambo yupo karibu nami kwa kila nililouliza hakuwahi kunificha, kwa kuwa jini huyo alikuwa muelewa alinielewa suleyha na kisha akarudi na kuendelea kuniosha hakuishia hapo bado aliendelea kuuliza maswali mengine mengi ila swali lililokuwa gumu kwangu kujibu ni pale suleyha aliposema "Iwapo utagundua kuna jini tofauti na malkia Zinduna anaekupenda je utakubari kushare nae penzi?" ni swali ambalo liliuyumbisha moyo wangu na kuhisi sasa kuna mbegu za mapenzi zilizoanza kumea kati kati ya moyo wa jini huyo suleyha, sikuwa na jibu la haraka la kumjibu siku hiyo zaidi nililibakiza moyoni mwangu likiwa kama baki au kiporo siku nitapoupata ukweli kuhusu suleyha ndio nitalijua jibu la swali lake,
★★★★★★★★★★★★
Usiku mzima swali la suleyha lilinisumbua kichwani kila lilipokuja akirini mwangu basi lilikuja na tafsiri nzima ya chuki ya mapenzi baina ya malkia Zinduna na kijakazi wake suleyha, kama ilivyokuwa ahadi yetu usiku wa jana ikifika asubuhi malkia Zinduna ataniijia twende tukatalii niione dunia yao na kikubwa anifikishe kwenye bustani ilioitwa bustani ya Mahaba,, masaa matatu baada ya kukucha na kuandaliwa vyema nilikaa kumsubiri malkia na haikuchukua muda malkia akaja na mlinzi mmoja tu, nilishtuka kwani haikuwa kawaida ya malkia kutembea na mlinzi mmoja, "Vipi malkia mbona leo upo na mlinzi mmoja?" nilimuuliza punde baada ya kusalimiana "Niendako ni salama sihitaji kuwa na walinzi wengi eeh! mfalme wangu" malkia alisema "anha! sawa nashukuru kwa kuja pia kutimiza ahadi yako" nilimwambia malkia, kisha nae akanijibu "Zinduna haongopi! lolote atalosema atatimiza eeh! mfalme wangu" alisema malkia huyo wa majini, "chagua yeyote unaemtaka akusindikize huko katika hawa" Zinduna aliongeza neno, nami nilimchagua suleyha, tuliondoka ndani ya jengo hilo la dhahabu na kutoka mbali kabisa kitendo kilichozidi kunishangaza sikuamini hata kama dunia ile ingekuwa na maeneo makubwa na mazuri kiasi kile, "ni umbali kiasi gani?" nilimuuliza malkia Zinduna baada ya kutoka mbali na jengo lile, "kilometa hamsini" "kilometa hamsini??? yani kilometa hamsini tutembee kwa miguu????" niliuliza kwa mshituko, "usiwe na shaka usafiri upo" nae Malkia Zinduna alinijibu "uko wapi?" niliuliza kwa maana sikuelewa sehemu yenyewe tuliosimama ilikuwa ni mpweke sana, malkia Zinduna ndipo akapuliza mruzi mkubwa na kwa mbaaaali ilisikikika sauti ya farasi akija mbio na ndani ya sekunde chache farasi yule alifika kwa kuonyesha utiifu mbele ya malkia Zinduna alinyanyua miguu yake kwa shangwe kisha akashusha "Anaitwa seif, farasi wangu huyu nilipewa zawadi na baba kabla hajafa, mpande hawezi kukudhuru" malkia Zinduna alisema, nilibaki kumshangaa farasi yule mweupe sana aliepambwa kama binadamu huku manyoya yake yakiwa mazuri ya mterezo, nilimpanda nae malkia akaketi nyuma yangu "seif tufikishe bustani ya mahaba" malkia zinduna alimsemesha farasi wake na farasi nae akasikia na kutii kile alichoambiwa alianza kukimbia kwa kasi ya kimbunga hadi kwato zake alipokuwa anakanyaga nilionekana zikitoa viashiria flani kama cheche za shoti au radi, na juu ya anga alimbaa amba suleyha, mwenye uwezo wa kutoa mbawa na yule mlinzi mwingine wa malkia yeye alibadilika na kuwa paka mkubwa mweusi.
Ndani ya nusu saa tuliweza kuzimaliza kilometa hamsini tukiwa nae seif farasi mzuri wa kiume mwenye kasi ya ajabu, tulifika na mandhari kwa kweli ya sehemu ile yalikuwa ni yenye ushawishi na mvuto haswa! kila sehemu ya eneo lile palipambika vizuri kila nilipotupia jicho kila upande rangi ya kijani na umanjano wa mauwa ulinivutia ilikuwa ni fahari kwangu kuona mambo mazuri ya ulimwengu ule, "Huu ni mwanzo wa bustani nzuri ya mauwa, bustani hii haihitaji jini wala mwanadamu kuitunza bali wapo wadudu wawili huifanya kazi hii, nyuki na kipepeo huakikisha ustawi wa ua lenye afya unapatikana, na kipepeo hulifanya ua liwe zuri lenye mvuto kwa kulilea vizuri, tizama rangi za pinki njano na weupe zinavopepea kuashiria amani na utulivu unaopatikana maeneo haya" ni maelezo ya malkia Zinduna akinielekeza bustani ile nzuri, "Kweli panastahiki kuitwa bustani ya Mahaba,. kwa uzuri huu, aah!! hakika ulimwengu wenu unavutia" nilimjibu huku tukiendelea kupiga hatua katikati ya maua yale yenye mvuto kuyatizama na harufu zake nzuri za kupendeza, ilifikia sehemu kuna miti miwili mapacha midogo midogo, malkia Zinduna aliniambia tukae huku wale majini wawili suleyha na yule mlinzi wake wakisimama nyuma kidogo kama hutua kumi tu, "najua utakuwa unajiuliza mengi kuhusu hili eneo kuitwa bustani ya Mahaba sio? na kwanini nimechagua sehemu hii iwe ndio sehemu ya kukupa zawadi" malkia Zinduna aliniuliza huku akinitizama "Ndio malkia wangu" nilimjibu "Hio miti miwili inahistoria waliolala sehemu hiyo ni watu wawili walipendana sana kupita kiasi, watu hao mmoja wao alipendwa na jini na wale wengine walikuwa wakipendana binadamu kwa binadamu waliishi kwenye ulimwengu huu, katika chuki za mapenzi yule jini aliamua kuwauwa wawili hao kwenye kibonde hiki hiki na kuwafukia kabisa kisha nae alienda kujitetekeza mwenyewe baadhi ya majini walihuzunika sana kuondokewa na binadamu hao walioacha mfano kwa majini wengine pamoja na binadamu wenzao, hivyo waliamua kuifanya sehemu hii kama mapumzikio kwao hao wapendanao, ndio hapo waliamua kuipanda miti hio miwili sehemu walipozikiwa baada ya kuwafukua, ajabu ni kwamba hadi kifo kilipowakumba walikuwa wamekumbatiana" malkia Zinduna alinipa stori, stori ilioijenga picha ya baadae na suleyha na yeye maana vyovyote vile navyo muona suleyha ameshaanza kulipanda ua la upendo kati kati ya moyo wake, "dah! stori imenisimua sana malkia" malkia alicheka kisha akakaa kimya kiasi na kusema "Zawadi pekee niliokwandalia," kabla hajaendelea alikatisha na baadae akaendelea "Kabla sijakupa zawadi hii niahidi utanipenda maisha yako yote?" "ndio nitakupenda kwa moyo wangu wote na mapenzi yangu yote nimekukabidhi eeh!! malkia wangu" nilimjibu "Wapo warembo sana kwenye ulimwengu huu je unaweza kutosheka na Zinduna pekee?" aliuliza "sehemu yote yenye nyama ndani ya moyo wangu nembo ya Malkia Zinduna imetapakaa siwezi shawishika kwingine" nilimjibu "Unaniahidi??" "ndio na kuahidi" tulikaa kimya kiasi na baadae nilifumbua kinywa na kusema "Malkia na mimi naombi" malkia nae akanijibu "kuwa huru eeeh!! mfalme wangu" nilikaa kimya tena kiasi kisha nikashusha pumzi taratibu na hapo nikasema kwa sauti ya chini "kabla hujanipa zawadi kuna kitu nataka uniahidi" bila kujua ni nini nilichotaka kusema malkia aliwahi na kujibu haraka haraka "Nakuahidi eeh! mfalme wangu" kisha nikasema "Je utakuwa tayari kunirudisha duniani???" "Nini????" malkia akauliza kwa kung'aka,
YAPO MEMA YANAKUJA.. malkia Zinduna atakubali kweli kumrudisha Faraja duniani ikiwa tayari ameshampenda????
Mb ndio habari ya mjini wajanja tunasemaga hivi
#BAKI NA MIMI
Endelea..........
No comments: