SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {08}
SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini)
SEHEMU YA {08}
Endelea........
ILIPOISHIA..
Tuliishia pale ambapo Faraja na malkia Zinduna wakiwa kwenye ile bustani iliopewa jina la bustani ya mahaba na muda huo Faraja aliomuomba malkia zinduna kama uwezekano upo siku moja aje amrudishe duniani,
ENDELEA NAYO.....
"Hapana Faraja kukurudisha duniani kwa sasa sitoweza coz nakupenda muda mrefu na hisia zangu nimezitunza kwa ajiri yako tu, natambua umepakumbuka kwenu ila tafadhari hebu ufanye kwanza moyo wangu ufurahie kisha utakwenda huko kwenu duniani" Malkia Zinduna alisema nilimsikiliza kwa makini lakini bado maneno yake hayakutosha kuushawishi moyo wangu hivyo nilizidi kuyafukua yaliyomo ndani kabisa ya uvungu wa moyo wake "Malkia ujue hata kama nitakuoa bado chuki itajengeka baina yako na wafuasi wako alafu isitoshe mimi ni binadamu na wewe ni jini kweli itawezekana?" nilimuuliza swali la mitego tu malkia Zinduna nimsikie atalipokeaje, kisha nikakaa makini kulisikiliza jibu lake "mimi ndio mwenye amri zote na majini wote wanafuata amri yangu isipokuwa wale majini wa kabila la haturu pekee ndio hupinga kila jambo na sio hili la mimi na wewe tu ni tokea enzi za mababu zetu" alisema malkia "haya turudi kwenye mada malkia, je nikikubali kukuoa na wewe utanikubalia kuishi kwenye maisha yangu ya dunia?" nilimuuliza tena hapo malkia Zinduna alikasirika na akaanza kujionyesha ubaya wa sura yake baada ya sehemu ya uso kuanza kujigeuza na kutoa magamba gamba kisha akasema "Duniani huendi katu nimehangaika sana kukuleta huku wewe unipe Faraja vipi ukienda duniani mimi nitaishije bila wewe?" Malkia Zinduna aliongea kwa sauti kali iliojaa msisitizo ndani yake, kitendo kile cha malkia kubadilika kidogo sehemu yake ya uso kiliulainisha moyo wangu na kuufanya upoe ile hamu na cheche za kuomba kurudishwa duniani ziliyeyuka ghafra na hapo moyo ukaruhusu mawazo mawili matatu nje ya lile la kuomba nirudishwe duniani "Mh! hapa niwe mpole kabisa nikileta ujinga nitapotelea huku na ile ndoto ya kurudi nyumbani itafia huku huku dah!" nilijisemea huku nikimtizama malkia Zinduna akirudi katika hali yake ya mwanzo "unajua Faraja moyo wangu hauna mipaka kwako, moyo wangu ni pande zito la nyama lililozungukwa na utaji wa Faraja katikati ya moyo wangu, ndani kabisa ya moyo wangu upo mfereji wa neema ambao hutiririsha mapenzi juu ya pendo lako hisia zangu za dhati usizifanye kuwa mzigo kwa moyo wangu natambua wewe ni binadamu lakini nikuuachia moyo uzungumze hilo kwani moyo wangu ndio wenye mamlaka ya kuamua maswala yote yahusuyo mapenzi, hadithi hii ya mapenzi niliiandika toka enzi na sikuishi bila ya kukuchunga nilijua wazi endapo ningekukosa moyo wangu uneugulia donda kubwa, donda ambalo lingeniachia kovu kubwa ndani yake, Faraja tafadhari ishi na mimi kama vile mtu wa kawaida na ifanye sasa kama hii ndio dunia yako ya kawaida upe amani moyo wangu Faraja, usiufanye moyo wangu kuendelea kumwaga chozi juu ya penzi lako" malkia Zinduna aliongezea neno huku akiongea kwa hisia kali, nilimsikiliza kwa makini nikaona wazi malkia Zinduna amependa ile radha ya kuendelea kuiwaza dunia taratibu kupitia maneno mazito ya malkia nilijikuta ikinibadirika kichwani na sasa niliwaza alilolisema malkia "Nakuahidi malkia sitowahi tena kukuudhi kwa neno la dunia" nilimuweleza malkia Zinduna, na muda huo malkia alitoa ile zawadi yake iliotufikisha kwenye bustani ile, ilikuwa ni pete nzuri iliotengenezwa kwa madini ya dhahabu hata sonara aliedizaini pete ile yaonekana ni fundi aliebobea katika fani hiyo, malkia aliitoa huku akiwa anaitazama kwa kuisugua Sugua katika vidole vyake viwili kidole ch gumba na shahada aliongea nakusema "Hii ni zawadi kwa mfalme, endapo utavaa pete hii haitaashiria mume tu hapana!, pete hii aliestahiki kuiva ni mfalme pekee ataechaguliwa na malkia hivyo nadhihirisha upendo wangu wa dhati kwako naomba nikuvishe pete hii, usije ukaivua utauvua ufalme wako, kumbuka kuvaa pete hii ni kitambulisho tosha kama mume na pia kiutawala utatambulika kama mfalme na wale wote wenye mipango ya kukuzuia kuwa mfalme hawatoweza kwani pete hii itazishinda chuki na fitina zao, na kuhusia tena usiivue pete hii kwa gharama yeyote!!!" Alisema malkia Zinduna kisha akaniomba ninyooshe mkono, nilinyoosha mkono wa kulia na malkia akachagua kidole kimoja cha ndoa na kunivisha pete ile "Nakupenda kweli kwa penzi lako niko tayari hata maisha yangu kuyatoa sadaka kwa ajiri yako" Alisema malkia Zinduna kisha akanichumu mdomoni, kitendo kile suleyha alikiona vizuri tu lakini ilibidi ajikaze kwa kuwa yupo mbele ya malkia wake, baada ya hapo tuliondoka bustanini tukiwa tumehakikisha tumesimika mnara wa mapenzi baina yetu kwani maneno na matendo ya malkia Zinduna yalitosha kunithibitishia ukweri wa moyo wake,
★★★★★★★★★★★★
Tulirudi mjengoni huku siku hiyo nikitembea kifua mbele kutokana na ile dhamana au zawadi ya malkia, pete ilinifanya nidunde nitembee kwa kujiamini sasa na kuona mimi ndio mfalme kwenye ulimwengu ule"Ilikuwa si katika ndoto zangu kuja kuishi kwenye maisha ya raha kiasi hiki nikiwa katika ulimwengu wa majini, rehma zako mwenyezi mungu zimeniweka hapa na utukufu wako mwenyezi mungu ndio umenifanya niishi vyema katika ulimwengu huu tizama ni muda mchache tu lakini umeshanionyesha njia ya mafanikio, leo malkia amenithibitishia wazi wazi kusudio lake la kuniita katika ulimwengu huu ahsante Mungu!" Nilizungumza na nafsi yangu wakati huo tunakata njia kukisogelea chumba changu, njia nzima tulimopita kila mtumishi wa jengo lile alipoona nimevalia pete kulingana na tamaduni zao walivyoelezewa basi walionyesha adabu mbele yangu kwa kuviinamisha vichwa vyao mpaka pale ninavyowavuka,
★★★★★★★★★★★★
Moja kwa moja nilijitupia kitandani baada ya kuwa tushaingia ndani ya chumba na kama unakumbuka vizuri nikiingia ndani sitakiwi kutoka tena nje ya chumba bila ruhusa na hivi nilivyopewa pete ya kifalme ndio kabisa hofu itazidi kuwa kubwa juu yangu hivyo niliona nijiongeze mwenyewe kwa usalama wangu zaidi, "Mheshimiwa mie natoka kidogo kuna mahara naelekea hivyo nitachelewa kurudi, naomba leo nikuache na salhat akutunze hadi hapo nitaporejea" suleyha aliongea kwa utiifu huku akiwa ameinamisha shingo yake, na sasa hakuonyesha ile hali ya wivu kama mwanzo ingawaje ilinishtua kidogo ila sikuitilia maanani sana nilihisi huenda suleyha amejitambua yeye ni nani na
malkia ni nani hivyo na mimi nilimjibu "dah! sawa ila nitaimiss! sana kampani yako maana wewe ndio pekee niliekuzoea, wewe ndio unajua leo nile nini, unajua leo nivae nini na mengine mengi kwani naona siku sijui nusu siku! ni kama mwaka mzima kwangu" nilisema huku nikiyaangalia macho ya binti huyo wa kijini "Heshima kwako mfalme wangu" aliongea huku jicho lake lote akitupia kwenye mkono nilivalia ile pete, "sawa nimekuruhusu kwa moyo mmoja enenda na kesho asubuhi tu nataka ninywe chai yako" nilimwambia suleyha "Napokea na kutii amri yako mfalme wangu" alisema suleyha na kisha akaondoka "Mh! ajabu yani kirahisi hivi amekuwa mtiifu juu yangu yaweza kuwa ametambua thamani ya hii pete, au ameona wazi kuwa mimi ndiye mfalme mtarajiwa nini? kama sio hivyo basi huenda akawa na jambo lingine nje ya haya" nilijisemea huku nikimtizama suleyha akiishiria nje ya mlango, "Sasa nimeamua kufanya jambo Malkia Zinduna naona anataka kumteka Faraja kiakiri ngoja nitahakikisha nasambaratisha uhusiano wao, Faraja ni wangu mimi" ni maneno ya suleyha akizungumza kwenye nafsi yake alipokuwa anatoka ndani mule,
UPANDE WA PILI
Baada ya suleyha kutoka kule chumbani na kuhakikisha ameweka mambo sawa alikuja upande wa wale majini walionyesha nia zao kuwa hawapo tayari kutawaliwa na binadamu, Hivyo alipofika alipokelewa vizuri na kikao cha dharura kikatangazwa na majini wote wakafika kwa muda uliotakiwa, "Nafikiri nyote mnanitambua mimi ni nani hakuna haja ya kuulizana maswali mengi ila tu tujadiri jambo kubwa lilonileta hapa" suleyha alianza kuongea na wale majini wenzake walikaa kimya kwa utulivu wa hali ya juu kuusikiliza huo ujumbe aliokuja nao, akaendelea kusema "Nyie najua mnampinga sana malkia Zinduna si ndio?!" aliuliza na wote wakatikisa vichwa vyao kisha akaendelea tena "Leo asubuhi malkia Zinduna amemvisha pete ya kifalme Faraja" wote wakashtuka "Unasema kweli??" mmoja wao akauliza kwa mshituko "Dhahiri mimi ni kijakazi wa Faraja niliona kwa macho yangu mawili" suleyha alijibu na kuwafanya wale majini viti viwe vya moto kwani waliona tayari wameshachapwa bao la kisigino ila suleyha akawatuliza mawenge na kusema "kwa kua mimi namuhitaji Faraja sitaki amuowe malkia nimekuja kwenu kuweka dili" alisema suleyha na wale majini wakakaa kwa umakini nakutega sikio kusikia dili hilo"nataka tumuuwe malkia" alisema suleyha na kuwashangaza wale majini wote wakishtuka kwa pamoja na kumtizama sana suleyha hawakuamini kabisa kile alichokisema "nahisi hii ndio njia nzuri ya kunifanya niwe na furaha" aliongeza neno, lakini yule jini mwenye maono ya mbali alisema "Hapana! sio njia nzuri kabisa siku chache zilizopita tuliwahi kulizungumzia hilo na muafaka wetu ikawa ni kumpiga malkia kisiasa ili yule binadamu asitawazwe kuwa mfalme hivyo basi rai yangu..!" alinyamza kidogo na wote wakayatega masikio vizuri kusikia hiyo rai, "Kwa vile wewe ni kijakazi wa yule binadamu na umesema amevishwa pete ili tumshinde malkia Zinduna na wewe umpate huyo Faraja yakubidi uilete pete ya kifalme, ukishaileta pete ataivaa kijana wetu hapo malkia hawezi kuwa na nguvu ya kumtangaza Faraja kuwa mfalme kwa kua Faraja hatokuwa na pete ya kifalme na sisi ndio tutaitumia hiyo nafasi kumng'oa madarakani, tukishamng'oa wewe ndio utakuwa malkia wetu na kijana wetu atakuwa mfalme hapo unaonaje??" jini yule mwenye maono alisema, walimkubali maana ushuri aliowapa ni mzuri waliona unafaida kubwa iwapo utafanikiwa, suleyha alikaa kimya kiasi kisha akatoa jibu lake "Sawa kwa vile ni dili basi nitahakikisha naileta pete, ila naombeni mnipe dawa au sumu ya kumuua Faraja taratibu" alisema tamaa ya kiti cha umalkia tayari ilishaanza kumuingia suleyha kwa maneno ya yule mshauri akaanza kupoteza ile mandhari ya mapenzi alionasa kuitengeneza kwa Faraja "kwanza yule ni binadamu hawezi kututawala kiasi hiki!!" mmoja kati yao tena akaongeza neno, maneno yote yale yalizidi kumshawishi na kuipandikiza chuki ili suleyha asimuone wa maana, alitoka jini mkubwa ambae ndio alikuwa mwenyekiti wa kikao na ndio mzazi wa yule jini anaetajwa kuwa mfalme, akaingia kwenye chumba kimoja hivi na baada ya dakika kadhaa alitoka na kichupa kidogo cheusi na kumkabidhi suleyha kisha akakitolea maelezo mafupi "hii itammaliza kwa muda mfupi sana, hakikisha kesho asubuhi unaitia katika chakula chake mimi na kifuniko kimoja tu na mchana wake fanya hivyo hivyo hakika hana muda mwingi wa kuishi atakufa" alisema, Suleyha alipokea kichupa kile na kukificha ili kesho asubuhi afanye hiyo kazi.
Asubuhi ilifika na tokea jana hakuwepo hivyo siku hiyo nilipoamka nilikuta chai alioiandaa salhat sikutaka kuinywa mpaka chai alioiandaa suleyha maana sababu ndio chai nilioizoea, haikupita muda nae suleyha alikuja na kisinia chake alichobebea chai pamoja na kikombe kile kile ninachokipenda kukitumia kila siku alijua kwa njia hiyo nisingeweza kung'amuka kwenye mtego wake, alikuja akitabasamu sana na alipofika alisema "Najua nimekutesa mfalme wangu nisamehe bure" suleyha alisema huku akiniminia chai na kunikabidhi mkononi salhat alibaki kutuangalia tu, "Kunywa mfalme kwa amani kabisa suleyha nipo kwa ajiri yako" alisema huku akinitizama kwa jicho la mlegeo,
JE suleyha ameshamtilia sumu Faraja?
Tukutane siku ya kesho kujua nini kilichoendelea
Yapo mema yanakuja usibanduke wewe,... #BAKI NA MIMI,
ITAENDELEA..............
No comments: