SIMULIZI:- >ZINDUNA (Malkia wa majini) SEHEMU YA {09}





SIMULIZI:- >ZINDUNA
(Malkia wa majini)
SEHEMU YA {09}


             Endelea.........

ILIPOISHIA..
Tuliishia pale ambapo suleyha alitoka kule kwa wale Majini waliompinga vikali Faraja asiwe mfalme, huku wakiwa wamemlaghai ampe sumu katika chakula ili afe kisha amvue ile pete aipeleke kwa hao majini..

ENDELEA.....

"Mh! hapana nitakuwa sijatenda haki kulifanya hili kwani Faraja ana hatia gani? nimuuwe kanikosea nini? wakati kijana wa watu hana makuu, kama ni vita ni yangu na Malkia Zinduna na sio kumshirikisha mtu asie na hatia, nitakuwa nimefanya makosa sana kabisa! yatakuwa matumizi mabaya ya akili, kama ni kiti cha malkia nahesabu nimekipoteza sasa nimwage damu ya mtu asie na hatia hii inamaana gani? nitafurahia hata hicho kiti chenyewe?" ni maswali kibao yaliyokuwa yanaranda randa kichwani mwa binti suleyha huku akikitazama kikombe kilichobeba chai tayari kukipeleka kinywani, lakini binti huyo kwa kuwa alikuwa tayari moyo wake  umeamua haki aliona sio vyema amuuwe kiumbe asie na hatia kwa tamaa za kuwa malkia aliona sio vyema kabisa kulitenda hilo nilibaki nikimtizama suleyha akikiangalia kikombe changu huku muda huo ndio nazidi kukifungua kinywa nivute taratibu kimiminika hicho, lakini ghafla suleyha alikisukuma pembeni kikombe hicho kisha akalilusha na lile sinia zima aliobebea ile chai nilistaajabu kuona tukio hilo suleyha alilolifanya mbele yangu, nilimwangalia kwa jicho kali kisha nikamuuliza "UMEFANYA NINI SASA SULEYHA???" nilimuuliza kwa ukari huku nikimtizama kama simba, lakini hakunijibu alibaki kimya tu akiangalia chini "WE SULEYHA SINAKUULIZA NDIO NINI HIKI??" nilimuuliza tena kwa ukali na muda huo salhat alianza kuokota vipande vya grass vilivyopasuka na kutapakaa ovyo! ovyo! mule ndani "Nisamehe mfalme wangu" suleyha alisema huku macho yake yakiwa na marengerenge madogo ya machozi yaliyokuwa tayari kuanguka kufuatia suleyha kuigundua haki  yakuwa angeua kiumbe asie na hatia, hata hivyo moyo wake ulikuwa unapata shida sana kuweza kuhimiri maumivu yaliyo ndani kabisa ya moyo wake, "Sawa suleyha naweza kusema bahati mbaya au nzuri lakini mpaka sasa sijaipata tafsiri nzuri ya tukio hilo ulilolifanya" bado niliendelea kusimamia pale pale nijue chanzo ni nini hadi ukisukume kikombe cha chai pembeni, "Nili...!" kabla hajatolea maelezo kitendo alichokifanya ilisikika sauti ya kengere, sauti hiyo ilikuwa sio ya kengere za  milangoni hapana, sauti ile ilikuwa niyataarifa kila usikiapo mlio wa kengere hiyo basi yakubidi kama unakazi uache uende kwenye chumba cha mkutano huenda kukawa na habari mpya, "Sawa suleyha hiyo bahati mbaya imetokea usilie sasa siwezi kufanya chochote kile sawa??" nilimweleza suleyha kwa upole nae aliitikia kwa kutingisha kichwa chake kisha nikatoka na salhat,
        ★★★★★★★★★★★★

Nilitoka chumbani huku maswali mengi yakiwa yamepangana kichwani mwangu kuhusu tukio zima alilolifanya suleyha kila nilipowaza hivi akili haikubaliani nalo nageuzia hivi lakini pia hivyo hivyo najikuta nawaza na kuwazua lakini kila swali ninalojiuliza linakosekana jibu akilini mwangu "yani suleyha anazidi kunichanganya kabisa, kila siku anakuja na mambo mapya na sasa hivi sio kama mwanzo alivyokuwa amechangamka mwenye sura inayovutia kwa tabasamu, sasa hivi amebadirika sana sijui chanzo ni nini hebu ngoja jioni ya leo nitamuuliza vizuri" Nilijisemea nakuongeza mwendo nikiwa na salhat pamoja na walinzi kadhaa, na nyuma yetu suleyha alikuwa akija taratibu huku akifuta machozi, tulifika mjengoni na kila mtu akachukua nafasi na kuketi tayari kusubiria kikao kianze na bahati nzuri mtu waliyekuwa wanamsubiria alifika, alikuwa ni malkia Zinduna, malkia Zinduna alipanda na kukaa kwenye kiti chake huku safari hii akiwa amevalia gauni lake reeefu lililoburuza gauni lenye rangi nzuri ya kuvutia huku kichwani mwake akiwa amevisha taji la kimalkia lips zake na macho viliendelea kuuonyesha uzuri wa malkia Zinduna, aliketi na kututizama huku macho yake sana yakinielekea pale chini nilipokaa, watumishi wake wakiwa na vipepeo pembeni walizidi kumpepea taratibu malkia Zinduna, na ndipo msemaji mwenye dhamana hiyo alisimama mbele akiwa na karatasi mkononi mwake yule mzungumzaji akaanza kwa kusema "Nitaarifa mpya na ngeni kabisa masikioni mwenu, itawashangaza sana na wengine itawauma pia, iko hivi: uongozi mzima wa ufalme kuanzia kwa mtukufu malkia umekaa na kujadiri swala zima la nani anaestahiki kukikalia kiti cha kifalme, kupitia viongozi wakubwa wa nchi hii walikaa wakalijadiri wakapata maamuzi yaliyosahihi na malkia amekata Shauri juu ya hili, hivyo basi! aliechaguliwa na kuridhiwa na viongozi wetu ni Faraja ibun Wahab, siku ya Ijumaa itakuwa siku rasmi ya kumtwadha, kumwapisha pamoja na kuwafungisha ndoa" Aliamliza yule mzungumzaji na jopo la majini wengi waliompenda malkia Zinduna waliamka kidedea na kuanza kupiga vigere gere, wengine mbinja yani kila jini alieweza kufanya lake alifanya ikiwa ni sehemu ya kusherehekea, Malkia Zinduna akasimama na kunyoosha mkono wake juu kila mmoja alipouona alielewa maana yake hivyo wote walikaa chini na kurudi kwenye utulivu ule waliokuwa nao mwanzo, kisha malkia akasema "Nje ya hayo nimegundua kuna ubadhirifu mkubwa wa matumizi ya mariasili nchi kwenye serikali hii, fedha zinazotoka bila kazi maalumu upotevu wa mali nyingi, hivyo kama kiongozi aliepita hakuweka mpango  mzuri wa kudhiti mali alikuwa na udhaifu mkubwa juu ya hili, hivyo kupitia madhaifu yake tunarekebisha na kuziba nyufa zote tuwe na taifa kubwa lenye nguvu na lenye kujitegemea kiuchumi" alisema malkia Zinduna kisha akakaa na kumuacha yule msemaje aendelee "Kama alivyosema mtukufu malkia kwa wale wote wenye madhaifu tumeamua kuvitengua vyeo na nafasi zao pia, waziri wa fedha, Chief general" waziri wa Dhamana na hifadhi ya nchi wote hawa wamefutwa kazi" wote aliwataja waliotakiwa kuviachia viti vyao, kwa hasira ya kuachishwa kazi majini wale walisimama bila kusubiri kikao kumalizika na nilipowatizama vizuri walikuwa ni wale wale walionipinga siku zote, liliniingia wazo kichwani nikahisi huenda malkia Zinduna amefanya hivyo kuipunguza nguvu yao ili wasije kumuharibia huko mbele tunakokwenda "Kweli malkia ni mwelewa sana na anajua kuzisoma sana akili za Majini na watu" nilijisemea nakutingisha kichwa nikiamini safari yangu ya kuwa mfalme itakuwa rahisi kwa kuwa wale wapinzani wameanza kupunguzwa makali, "na pia leo tutamtangaza jini mama wa watumishi wote wa kike katika jumba hili" yule msemaji akaendelea" hapo majini wote walikaa vizuri kusikiliza na kumuona aliteuliwa katika sekta hiyo, "Suleyha binti Ashirafa ndio alieteuliwa kuwa kiongozi mama wa watumishi wote wa kike humu ndani, hii itamsaidia malkia kumpunguzia uzito na wingi wa majukumu" alihitimisha na kuikunja karatasi yake, shangwe zikapigwa kila jini alifurahia mabadiliko yale, hata suleyha mwenyewe hakuamini wala hakutarajia siku moja malkia anaweza kumtoa katika utumishi na kumpandisha cheo kuwa malkia mama wa watumishi wote wa kike kwenye jengo hilo, alisherehekea kwa furaha kubwa hadi machozi yakawa yanamdondoka binti yule, "Nahisi malkia amefanya hili kuniweka mbali na suleyha, itakuwa kuna kitu alichogundua kinaendelea kati yetu licha ya kuwa kitu hicho ni siri yake, sio bure kumpa hicho cheo suleyha" nilijisemea kimoyo moyo huku nikimtizama suleyha alivyokuwa anafurahi, "laiti kama angejua ni njia ya kututenganisha sidhani kama angeendelea kuruka ruka hivyo" niliendelea kujisemea kimoyo moyo
    ★★★★★★★★★★★★

Baadae baada ya kile kikao kuisha tulikutana na suleyha nae suleyha aliniomba tuzunguke zunguke, sikumkatalia tulienda na walinzi wanne tu jambo ambalo lilikuwa hatari kwetu na malkia Zinduna angesikia ingeleta balaa, hatukujari kwa kuwa siku hiyo niliona ni siku nzuri ya kumuaga suleyha ilinibidi niambatane nae, tulizunguka sana maeneo ya nje ya jengo la kifalme hadi jioni ilipoanza kujihidhirisha kwa kiza kuanza kuuondka mwanga hafifu wa ulimengu ule,  niliona sehemu nyingi ambazo  mwanzo sikuzitembelea kwa kuwa suleyha yupo kwa ajiri yangu niliyajua mengi, baada ya mizunguko yote tulirudi mjengoni tulipofika nje ya chumba changu tulikuta wimbi kubwa la walinzi waliokizunguka chumba changu na nilipowatizama vizuri walikuwa ni walinzi wa malkia Zinduna..

JE NI WALINZI TU, AU NA MALKIA YUPO NDANI YA CHUMBA?

yapo mema yanakuja,......

        ITAENDELEA.........



No comments: