SIMULIZI:- >ZINDUNA (malkia wa majini) SEHEMU YA {10}





SIMULIZI:- >ZINDUNA
(malkia wa majini)
SEHEMU YA {10}

            Endelea...........

ILIPOISHIA..
Tuliishia pale ambapo suleyha pamoja na mfalme mtalajiwa Faraja, wakiwa wametoka matembezi na waliporudi chumbani, kwa nje ya chumba chake alikuta jeshi likiwa limetanda chumba kizima hawakujua haraka jeshi hilo ni la nani zaidi walihisi litakuwa jeshi la malkia Zinduna,

ENDELEA NAYO.....

Nilishtuka sana kuliona jeshi la walinzi wapatao ishirini wakiwa wamezengea chumbani kwangu na hasa kilichonipa homa ni juu ya suleyha iwapo malkia yupo ndani atamfanya nini ikiwa malkia alishamuonya na kumtahadharisha asinitoe nje, "Suleyha si walinzi wa mlkia hawa??" nilimuuliza suleyha huku jicho lote likiwa makini kuutizama mlango wa chumba changu muda huo ukiwa wazi, "ndio wenyewe Faraja" nae suleyha alijibu huku macho yake yote yakiwatizama walinzi wale waliokuwa wamesimama kama magogo hawatingishiki wala hawageuzi shingo zao, "Dah! sasa huku wameijia nini??" niliuliza tena "Itakuwa malkia yupo ndani kwa maana wakati tunatoka niliacha mlango nimeufunga na nje walikuwepo walinzi wanne pekee" suleyha alijibu, jicho la hofu lilizidi kuutizama mlango tu wakati huo tulikuwa tumebakiza sentimeta chache kuona kwa ndani, "Ni kweli ndio yeye siunona amekaa kwenye kiti anabembea??" suleyha alisema baada ya kutupia jicho kwa ndani na kumuona malkia akiwa amekaa kwenye kiti ananesanesa, alikuwa ametutegea mgongo tu, "Tumwambieje sasa?" aliuliza suleyha "Nitamwambia niliomba unitoe picnic" nilisema nikimpa mpango wa kumuepusha na adhabu atakayoipata kutoka kwa malkia kufatia jambo la kukaidi amri ya malkia wake, "picnic ndio nini?" aliuliza "aah! bwana nikujitetea tu mi mwenyewe sijui hata hiyo picnic ikoje"  niliongea kisha tukacheka kwa pamoja, tuliingia ndani kwa kujikaza na kumkuta malkia Zinduna akiwa Ananesanesa kwenye kiti hicho chenye spiringi, "Na kusalimu kwa utukufu wako malkia wangu" nilitoa salamu nzuri ili kidogo impunguzie makali ya hasira kwa maana hata bila kuambiwa ule mkao aliokaa kwenye kiti ulionyesha dhahiri amechukia "Nakuitika eeeh!! mfalme wangu" alijibu kimapozi huku akisimama na kugeuka taratibu kama hataki, sikutegemea kwani kile nilichokiwaza hakikuwa kilienda tofauti kabisa, "ulikuwa umeenda wapi muda wote huo mfalme wangu? hujui ulinitia hofu na moyo wangu haukuwa na amani kabisa muda wote huo?" malkia aliongea huku macho yote akimtupia suleyha, "sikujua kama leo utanitembelea malkia wangu nje ya hilo pia nilimuomba suleyha tutoke picnic" nilitumia ule ule uongo tulioutunga dakika chache zilizopita, "mmmh!! picnic? picnic ndio nini??" aliuliza malkia, kama unavyojua muongo huwa hakosi sababu pale pale maana ya picnic ikanijia akilini hivyo tena nikautumia uongo "Ni safari ya kuzunguka ndani ya jengo bila mlinzi ndio tunaita picnic" "mhuu!! kwani duniani ukizunguka zunguka ndio mnaita picnic?" aliuliza malkia "Ndio" nami nilimjibu "anha! sawa" alisema kisha akaendelea kumtizama kwa jicho baya suleyha "alafu wewe!! we siumechaguliwa kuwa mama wa Majini wote wa kike au??" aliuliza malkia na safari hii hakuitumia ile sauti ya mwanzo alitumia sauti ya ukali kabisa"ndi.. ndio malkia" suleyha alijibu kwa kutetemeka hadi maneno yakawa yanatoka kwa kukwama kwama, "nenda kwenye makazi yako na nisije nikakuona unazengea kwenye chumba hiki, kwanzia sasa nitaleta mtumishi mwingine atae mshuhulikia kila kitu mfalme, salhat na anath nitawahamisha vitengo na wao wawe na vyeo" aliongea malkia Zinduna, taratibu nilianza kuisoma akili ya malkia hapo nikabaini kabisa kuna jambo liko nyuma ya pazia ambalo malkia analificha "Napokea na kutii amri yako eeh! mtukufu malkia" suleyha aliongea kwa heshima na taadhima kama ilivyo kawaida yake na kuinamisha kichwa na kisha akarudi nyuma hatua kadhaa ili ageuke aondoke lakini kabla hajaondoka malkia alimsogelea na kumpa neno moja akisema "Farasi ni mmoja hawezi kuendeshwa na madereva wawili hata siku moja" aliongea  hivyo licha ya kuwa alitumia sauti ya chini (mnong'ono) lakini sikio langu lilikuwa madhubuti hivyo nililinasa hilo, "sawa hilo nalijua vizuri ila usiendelee kujifanya mwema mbele yake huku sura ya chui ukiificha ndani yako" alisema suleyha "Hahahahaha!! ni miaka imepita haitanidhuru chochote kile hata ukisema" malkia nae aliongea, muda wote waliongea kwa sauti za chini sana mpaka mengine waliokuwa wanazungumza sikuyanasa kabisa, "sawa ila hakuna siri malkia wangu siku atayogundua ukweli sijui tu kama mtaendelea kupendana" suleyha nae alimjibu malkia huku wakitizamana jicho kwa jicho, "huu ni ulimwengu wangu na amri zote ni zangu hata akigundua atakuwa amechelewa" malkia alisema kisha akawaita walinzi na kusema "Msindikizeni suleyha hadi kwenye chumba chake" aliwaamuru wale walinzi "Tunapokea na kutii amri yako eeh!! mtukufu malkia" walisema kwa pamoja kisha wakapiga vifua vyao kwa mkono wa kulia taratibu na badae wakaondoka nae suleyha, licha ya kuwa sikuyasikia mazungumzo yao pale walipopunguza sauti ila nilihisi kwenye ile minong'ono kuna kitu cha siri kinaendelea baina ya suleyha na malkia, "kuna jambo hapo kati kati kwanini wameng'ong'ona zaidi ya dakika mbili bila kuongea kwa sauti? kuna kitu kinachoendelea hapa sio bure" nilijisemea kimoyo moyo kisha nikageuka kumtizama binti suleyha akitolewa ndani ya chumba changu, nilitingisha kichwa kwani niligundua hiyo ni njia mojawapo alioitumia malkia kuniweka mbali nae,
     ★★★★★★★★★★★★

Hiyo siku tena iliisha na siku sasa iliobaki ni moja ili tukakamilishe ile ahadi yetu, Asubuhi sana niliamka na kukuta watumishi wapya, watumishi wale walikuwa wamevalia vigauni vyao vifupi vya rangi nyeupe huku kichwani wakiwa wamefunika kwa kofia za rangi hiyo hiyo, na mikononi mwao wakiwa wamevaa groves, walileta chai kama walivyoambiwa na mtukufu malkia kila siku asubuhi sana inatakiwa wanioshe kwa maji ya uvugu vugu na wahakikishe chumbani kwangu kila mara wanapuliza marashi sambamba na kufukiza ubani, haya yote nilipenda kumuona akiyatenda suleyha hivyo nilipokuwa nawaona wale wageni moyo wangu ulikuwa unakunjamana kwa hasira, mmoja kati yao alieleta chai kwa adabu na utiifu mkubwa alinisalimu kwa magoti kujidhihirisha yeye ni bora kuliko wote waliotangulia "Maamkizi mema eeh!! mtukufu mfalme" alisalimu "na kwako pia" hii ndio ilikuwa salamu ya watu wote waliondani ya jengo lile neno shikamoo kwao sikuwahi kulisikia kabisa, "chai ipo tayari mfalme wangu" alisema  "Sinywi na uondoke hapa" nilisema kisha nikageukia upande wa pili na kumtegea mgongo, alikaa kimya kidogo kisha akatoa sauti yake ya upole "mfalme chai itapoa" "We Hebu niache basi we vipi?? kama ni chai si unywe hata wewe nimeshakwambia sinywi bado unang'ang'ana unang'ang'ania nini sasa nimeshakwambia chai yako sinywi" niliongea kwa msisitizo ili binti huyo atoke lakini nilipogeuka na kumtizama alikuwa bado yupo na sinia lake amelishika tena akiwa amepiga magoti mbele yangu "dah! we binti king'ang'anizi aisee si uondoke jamani ebo!" licha ya kuongea kwa sauti ya juu hata wale waliokuwa wanapamba pamba kusimama lakini jini huyo alionyesha utiifu wa nama yake, "sawa mfalme usipokunywa sasa hivi hata baadae mi nitaendelea kuhakikisha haipoi" alisema jini yule kisha akasimama nakuitenga mezani, baadae malkia alikuja kunitembelea na kuwakuta wale majini wakiwa wameinamisha vichwa vyao tu huku mule ndani nikiwa nimevuruga vuruga "nyie kuna nini kinachendelea humu??" malkia aliuliza lakini wote walikaa kimya "Si nawauliza mmekuwa bubu eti??" aliuliza tena "Amekataa kunywa chai malkia na haya yote unayoyaona ametenda mwenyewe" mmoja katika wale wanne alijitoa kimaso maso na kuongea mbele ya malkia "Shenzi mtu mnashindwa kumshawishi awaelewe, alieandaa chai ni nani?" malkia akawauliza wote waligeukiana na kunyamaza kimya hakujitokeza alieandaa chai lakini yule mwingine alieniletea chai muda ule alijitokeza na kuwakingia kifua wenzake "Malkia ni mimi" "hapana malkia ni mimi" hapana malkia wote hao hawahusiki mimi ndio nilioandaa" "hamna acheni uongo mimi ndio niliipika hiyo chai" wote walijitokeza "anha!! nyie wajanja sio??" malkia alisema kisha akatoa sauti kumuita mlinzi mmoja katika wale aliokuja nao na mlinzi muda huo huo akawa ameingia ndani "peleka hawa gorigota wakapate bakora kumi kumi kila mmoja wao naona wameshindwa kufanya kazi" alisema malkia, kweli nilijisikia vibaya sana kuona wale mabinti wakichukuliwa kupelekwa kupata adhabu wakati mimi ndio chanzo moyo ulinisuta na hapo nikasimama "Hapana makosa yote ni yangu" nilisimama kidete kuwatetea wale mabinti wasio na hatia "waachie mimi ndio nilikaidi sio wao waachie hawana makosa, nilaumu mimi" nilisema huku nikimtizama malkia "sawa waachie" alimuamulu yule mlinzi akawaachia, "sawa yote yameisha jiandae tutoke kidogo twende matembezi" alisema malkia nami nikakubali kisha wale mabinti wakarudi kuniandaa,

Baada ya maandalizi ya nusu saa nilikuwa safi nemependeza huku harufu za marashi zikinyunyiwa nguo zote, tukiwa na walinzi sita wa malkia tu siku hiyo tulishuka floo ya chini ambayo siku chache hapo nyuma niliwasikia walinzi wakisema panaitwa 'underworld', nilifurahi kwa kuwa malkia alinipa nafasi ya kulizungukia jengo hilo, tulizunguka sana kwenye floo hiyo ambako kulikuwa na joto kali, tukifika sehemu moja ambapo kuna mafundi sonara waliochonga vitu vya kifalme kwa dhahabu iliyoyeyushwa, na wengine walikuwa wakifanya kazi ya kuzing'arisha, tulikuwa tumesimama kwa nje kidogo tukiangalia kupitia dirisha kubwa lililojuzunguka karakana hiyo, katika tupia tupia macho sehemu wanapong'arisha vile vitu vilivyotengenezwa nilishtuka baada ya kuona kuna mwanamke aliefanana kabisa na mama yangu aliepoteza maisha miaka kadhaa iliopita, "Mama???" nilijikuta nikiropoka na muda huo baada ya malkia kuligundua hilo alisema "TUONDOKE HAPA" alisema huku akinivuta mkono nitoke pale,

Hii ni kweli atakuwa mama yake, kama mama yake na huko anatafuta nini??
USIKOSE SEHEMU IJAYO,,,....

        ITAENDELEA,,,.....



No comments: