SIMULIZI:- >ZINDUNA, (malkia wa majini) SEHEMU YA {11}





SIMULIZI:- >ZINDUNA, (malkia wa majini)
SEHEMU YA {11}


           Endelea...........

ILIPOISHIA.
Tuliishia pale ambapo Faraja alipomuona mwanamke katika ile karakana, mwanamke yule akiwa amefanana sana na mama yake aliepoteza maisha miaka kadhaa iliopita..

ENDELEA NAYO......

"Nilijitahidi kujivuta kwa nguvu ili nisogee dirishani nikahakikishe kabisa kama ni mama au ni ndoto, "Malkia niachie kwanza mama yangu yuko pale" nilizidi kuongea huku nikimsonteshea malkia Aiangalie ile sehemu nilipomuona mama amesimama aking'arisha vile vitu vilivyochongwa kwa dhahabu "We hamna kitu hapo bwana" malkia alisema huku akizidi kunivuta mkono nisiweze kusogea pale "Niachie" niliongea kwa sauti kubwa jambo lililomfanya malkia asitishe zoezi lake la kuning'ang'ania mkono hivyo alimua kuniachia kisha akasema "haya kaangalie unachotaka kuangalia" alinichia mkono nami sikusubiri nilirudi haraka na kuchungulia pale dirishani hususani ile sehemu nilipomuona mama, niliangaza huku na kule lakini sikufanikiwa kumuona tena yule mtu aliefanana kabisa na mama aliekuwa amesimama pale dakika chache zilizopita, niliishiwa nguvu za kusimama baada ya kukosa kile nilichokitaka nilijikuta nikishuka chini taratibu huku nikiangusha chozi kama mtoto, kwani kile kidonda kilichoanza kupona kitambo nilijikuta kikitibuka upya na kuleta maumivu makubwa moyoni, malkia aliliona hilo hivyo alisogea pale nilipo na kunishika bega kisha akasema "undeworld kwa mgeni kupatembelea lazima yakukute haya sio hiari ila lazima, kuna mauza uza sana sehemu hii, ila kuwa na moyo mgumu ili uishinde mitihani ya huku chini, wapo wengine walishafika huku wakawa machizi kabisa, kwa kila binadamu anaefika huku hupatwa na mitihani tofuti tofauti kwaiyo jikaze tuondoke huku ukiendelea kulia haisaidii chochote na tena ushukuru sana hiyo pete imekulinda" alisema malkia nilishtuka sana na hapo nikafuta machozi "unasema pete???" nilimuuliza "ndio pete imekulinda na pete hiyo inauwezo wa kufanya maajabu makubwa iwapo Utaiomba" malkia alitolea maelezo ile pete, niliitizama kwa nusu dakika huku nikigeuza geuza mkono niikague vizuri na moyoni nikiendelea kujisemea "Anha!! alijua kabisa yatatokea haya lakini bado amenileta huku anamaana gani sasa? alafu kumbe hii pete nayo inamiujiza pia? sawa kama ndio nitaitumia hii hii siku nitayotaka kuondoka kwenye ulimwengu huu, licha ya kuwa naishi kwa raha kwenye ulimwengu huu lakini pia nikumbuke hawa sio wenzangu siku mambo yakibadilika watanidhuru hivyo akili kumkichwa tahadhari kabla ya hatari" nilijisemea na nikajifanya nimesahau kabisa kuhusu lile tukio nililoliona muda mchache kwenye chumba au karakana ile, lakini niliendele kuwa na mpango mwingine kabisa kwa kuwa ameshanipa maelezo kuhusu nguvu ya hiyo pete niliahidi siku moja nitarudi kutembelea underworld mpaka nihakikishe naujua ukweli kama yule niliemuona alikuwa ni mama au ni mauza uza alioyasema malkia,

Baada ya yote tulitoka chini kule na safari hii malkia alitaka kujidhihirisha kwa jinsi gani alivyo mwema kwangu, aliamua kunitembeza maeneo ya siri kabisa ya utawala wao ambapo alinipeleka kwenye chumba kikubwa kabisa chenye urefu kama uwanja wa mpira hivi, "nyie bakini hapa mtusubiri mpaka tutaporudi" malkia aliwaamuru walinzi wasimame nje ya mlango watusubiri mpaka pale tutapotoka ndani, "usiingie na viatu" alisema malkia baada yakuniona nikitaka kukanyaga sakafu ya chumba kile huku nikiwa nimevaa viatu, nilivua huku macho yangu yote yakikitathimini chumba kizima na vitu vilivyopo mule, vitu ni vingi na tena vinang'aa, harufu ya udi ndio pekee ilionipitia puani ingawaje sikuona sehemu yoyote udi unapowaka au moshi tu, nilitembea huku macho yakiwa juu juu kushangalia fahari na uzuri wachumba kile kilichoitwa chumba cha kumbu kumbu (makumbusho) malkia alianza kunitembeza taratibu huku akinionyesha michongo iliochongwa kwa dhahabu huku akiitolea na maelezo yake, na baada ya muda wa nusu saa hatukuweza kumaliza sehemu yote tulikatisha safari kisha tukafanya makubaliano siku nyingine tutarudi kuendelea kutalii ikiwa ni sehemu ya kunifurahisha, nilikubali na tukaachana njiani malkia akielekea juu kilipo chumba chake na mimi nikishuka chini kilipochumba changu "mh! bado haya maswali yananichanganya na majibu yake sijui nitayajibu vipi, pale nilimuona mama kabisa alafu malkia akanivuta akasema tuondoke, kitendo cha kuvutwa na kurudi ameshapotea hapa kuna siri imefichika haiwezekani yaje mauza uza ya hivyo bwana, kwanza sijui nisifunge tu hii ndoa? ila hapana hiyo ni mada nyingine ninachokiamua kukifanya kwa sasa namuoa malkia sio kwamba nampenda hapana nataka nimchunguze mambo mengi anayonificha, nikiwa mume wake nitabaini mengi eeh!! najua kwa hili nitamshinda ujanja" nilijisemea kisha nikaongeza mwendo kurudi chumbani mwangu,
   ★★★★★★★★★★★★

usiku mnene kabisa ambao ndio ulikuwa usiku wa mwisho na kesho ilikuwa ndio siku rasmi ya ndoa nilishtuka usiku sana kufatia ile pete niliopewa na malkia Zinduna kutweka kana kwamba ni kitu chenye nafsi, nilikurupuka kisha nikakaa kitandani nikiiangalia pete ile ya ajabu iliokuwa ikidunda dunda kama mapigo ya moyo yalivyo, nilishtuka sana kuona tukio lile wakati tokea nimepewa pete ile sikuwahi kuliona kabisa, "walinzi!!, walinzi.." niliita kwa uoga mkubwa huku nikiendelea kuitizama pete ile ilionipa wasi wasi na presha kubwa ya ghafra, ukimya ulitanda na hakuna sauti ya jini mfanyakazi au jini mlinzi alieniitikia wito wangu, hapo nilizidi kuogopa zaidi, kwa moyo wa kujikakamaza ilinibidi niamke nikawachungulie huenda wakawa wamesinzia lakini nilipotoa kichwa kuchungulia sikuona mlinzi yeyote pale, na sio kawaida ya walinzi kutoka chumbani kwangu kuniacha bila ya ulinzi wowote hofu na mashaka vilizidi kuuandama moyo wangu vilivyo peleekea mapigo ya moyo kushindwa kustahimiri kitisho hicho "Wameenda wapi sasa usiku wote huu" nilijiuliza huku nikiangaza hapa na pale lakini floo nzima ilionekana kutulia sana, "sijawahi kuamka usiku tokea nimefika huku, huenda labda kila siku usiku wanatoka na hurudi subuhi??" nilizidi kujiuliza huku ile roho ya pete nayo ikizidi kukidundia kidole changu "aah!! mi naivua bwana" nilijishauri nakuona jambo zuri nikuivua lakini kila nilipojaribu kuivua kidoleni ilikwama kabisa na haikusogea hata kidogo, nikiwa bado nahangaika na pete huku kichwani yakiwa yameganda maswali ya kwanini walinzi waondoke usiku ule, vilianza kusikika vigere gere kwa mbali vilivyopigwa kwa mpangilio maarumu huku vikifatana na sauti za ngoma "mh! kina nani hao tena wanasherehekea usiku hivi mh! hawa majini nao wanavituko nilijisemea na kulipuuzia lile niliona ni jambo la kawaida tena nilihisi hata wale walinzi huenda wamefata zile ngoma kwa kuwa majini niviumbe wanaopenda ngoma sana nilifikiri hivyo, "hawa washenzi sana wanaacha kazi wanaenda ngomani?" nilijisemea kisha nikageuka nirudi ndani lakini nilipogeuza mwili ili niingie ndani ile pete ndio ilizidi kudunda zaidi "sasa nahisi kitu kupitia pete hii" nilijisemea na kusitisha zoezi la kurudi ndani nilianza kupiga hatua za taratibu nikifatilia zile sauti za ngoma nione pale zinapotokea, sauti zilizidi kunivuta kushuka chini kabisa, licha ya ukimya uliokuwepo hata sehemu zote nilizopita palikuwa pametulia hakuna ulinzi kama panavyokuwa nyakati za mchana, nilivutika zaidi kwa kufata ngoma zile mpaka pale nilipofikia kikomo chake, ni chumba kimoja kilichopo kati kati ya underworld ile. floo ya chini ambacho chumba hichi mara chache nilizopita sikuwahi kukiona kikiwa wazi lakini leo nimebahatika kikiwa wazi "Mmh! makubwa usiku mnene kama huu hawa viumbe hawapumziki kabisa au nikina nani" nilijisemea kwa makisio tu kabla sijatupia jicho ndani nione kuna nini kinachoendelea, "mhuuu!! ngoja sasa ningalie wanafanyaga nini usiku??" nilizidi kujisemea huku nikiusogeza upande mdogo wa pazia jekundu lililofunikiwa mlangoni lahaulaaa!! nilipochungulia kwa ndani macho yangu yalikutana na umati mkubwa wa majini wakiwa wamekaa chini palipotandikwa kitambaa cheusi huku wao wakiwa wamevaa mavasi meusi na kichwani wakiwa wamejifunika kwa vitambaa vyeupe, walikaa mkao wa aina moja huku wote wakiwa wamenyoosha miguu yao, walivitikisa vichwa vyao kushoto kwenda kulia na kulia kirudi kushoto, hali ile ilinishtua sana mapigo ya moyo yalizidi kunienda kasi "mpaka nijue ukweli wanafanya nini hicho??" nilizidi kujisemea kimoyo moyo huku nikizidi kuendelea kuwaangalia walivyokuwa wakitikisa vichwa vyao na hapo sauti za ngoma zikendelea kulindima kitendo kilichowafanya majini wale waamke na kuanza kuchezesha vichwa vyao bila mpangilio maalumu, nilibaki kuwatolea macho mpaka niondoke na jambo na katika subiria hiyo nilishtuka baada ya kumuona malkia Zinduna akiwa mbele kabisa ya kundi lile la majini akigaa gaa chini huku lile umbo lake la ubinadamu likimtoka na kuanza kuja katika umbile tofauti na lile nililomzoea..

SASA siri yafichuka kuwa Malkia Zinduna sio kiumbe wa kawaidaa je Faraja atavumilia kweli???

     Itaendelea..........



No comments: