STORY TAMU YA JESTINA 7






Asubuhi ilifika na Alwin alikuja kuchukuliwa na profesa na safari ya kuelekea kwao ilianza, wazazi wake hawakuamini kama mtoto wao kapona hasa baba ake na kujikuta akimtwanga swali "miliioni saba laki sita hamsini na tano elfu mia mbili thalathini na moja gawa kwa mbili, jibu lake ngapi". "milioni tatu laki nane ishirini na saba elfu mia sita na kumi na tano" alijibu Alwin bila kusita na profesa akathibitisha jibu hilo. Kwa mara nyingine tena ndani ya miaka kumi furaha ilirejea ndani ya nyumba ya Mr Kelvin kwa kumpata mwanae Alwin. Machozi yaliwatoka wanafamilia hao huku wakikumbatiana kwa furaha iliopitiliza. 
Asubuhi ilifika na kila mtu aliingia katika mishemishe zake, "oyaa Frank bado hajaamka" Jay aliuliza. "nahisi atakuwa bado maana jana nahisi kanywa nyingi sana" James alijibu, "nenda kamcheki basi" Jay aliongea na James aliondoka kuelekea chumba alicholala Frank. Baada dakika mbili James alirudi mbio huku akihema kwa nguvu, "oyaa nini wewe" Jay aliuliza. "Frank... Fra...nk" alijibu huku machozi yakimtoka, Ilibidi Jay na wengine wakimbie kuelekea chumba alicholala Frank. Wote walipigwa na butwaa baada kukuta damu zikiwa zimetapakaa chumba kizima huku mwili wa Frank ukiwa hautamaniki hata kuangalia. Jay alitoa simu na kuripoti polisi, haukupita muda gari ya polisi ilifika pamoja na gari ya kubebea wagonjwa. Mwili wa Frank ulitiwa kwenye gari na kupelekwa hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi. 
Inspecta Hans ndie aliekabidhiwa kesi hiyo, "habari yako kijana mimi naitwa Inspecta Hans na ndie ninae shughulikia kesi hii" alimwambia Jay ambae alionekana kuchanganyikiwa "hebu nieleze kila kitu bila kunificha". "ukweli inspector Frank alikuja jana usiku akiwa na majeraha kadhaa kichwani huku akipiga kelele kuwa amemuona Jestina". "Lakini Jestina si ameshakufa muda mrefu sasa" aliongea Inspector Hans lakini lengo lake ilikuwa ni kujaribu kutafuta ukweli kwa sababu kesi ya Jestina aliifungua tena. "mimi simjui Jestina ndio nani" alijibu kwa kitete huku akiangalia chini. "asante kwa ushirikiano wako nikikuhitaji tena nitakutafuta" aliongea inspector Hans na kuinuka kisha akamfata James ambae alikuwa kafunikwa shuka na mkononi akiwa na kikombe cha kahawa. 
"habari yako kijana naitwa Inspecta Hans" alijitambulisha, "mimi naitwa James na ni rafiki mkubwa wa Frank", "Ok James naomba unieleze tukio lilitokea jana". Na yeye alieleza kama alivyoeleza Jay na pia alipoulizwa kuhusu Jestina alisema vile vile na waliobaki wote walisema vile vile. 
Baada kumaliza kuwahoji alirudi kituoni kwa ajili ya kuendelea na harakati nyingine, lakini wazo lilimjia aende kwa Alwin huenda angepata pa kuanzia. Bila kuchelewa alitoka na kuelekea kwa Mr Kelvin. "habari za saa hizi mzee wangu na samahani kwa usumbufu, kwa jina naitwa inspecta Hans nina maswali mawili matatu kwa ajili ya Alwin" alijitambulisha na kueleza shida yake. Mr Kelvin ni muelewa sana alijua hilo litakuwa ni swala la usalama hivyo alimwita Alwin na kumwambia nia ya inspecta. "karibu inspecta na jiskie huru kuniuliza chochote na nakuahidi nitakupa ushirikiano" alieleza Alwin na kukaa kwenye kiti. "sawa kijana, nimekuja hapa kwa jambo moja tu. Profesa Alexander Harison alinipa kazi ya kufatilia kesi ya Jestina lakin kazi hii siwezi kuifanikisha bila msaada wako na najua ntakuwa nimekutonesha kidonda lakini naomba unisamehe kwa sababu nimesubiri kwa muda wote uliokuwa huko sawa" aliongea Inspecta. 
"hapana Inspecta hujatonehsa kidonda, yaliopita yashapita tugange yajayo" alijibu Alwin huku akitabasamu. Kwa mtu wa kawaida angeweza kusema yuko sawa lakini kwa mtu wa mafunzo kama Inspecta Hans tabasamu hilo lilitafsiri mambo mawili moja lilikuwa ni chuki na pili kisasi. "sawa, sasa jana kumetokea kifo cha kijana mmoja anaeitwa Frank, nadhani unamjua". "ndio namfahamu vizuri", "ok, mpaka sasa kifo chake ni cha utata huku wenzake wakidai kuwa kimesababishwa na Jestina" aliongea. Alwin alitabasamu kidogo "unajua inspecta damu ya mtu haipotei bure, na huo ni mwanzo tu wamebakia kumi na tisa na leo usiku atakufa mwengine" alijibu Alwin huku machozi yakimtoka. "sasa anaefaanya mauaji haya ni nani" aliuliza inspector, "Jestina" Alijibu Alwin na kuachia tabasamu kubwa. Inspector akaona hakuna haja ya kuendelea kuuliza maswali , aliaga na kuondoka. 
Hofu ilianza kutawala katika mioyo ya wale walioshiriki katika kifo cha Jestina kwa njia moja ama nyingine. Mazishi ya Frank yalifanyika huku wengi waliomjua walikwenda akiwemo Alwin ambae alioneka kutokuwa na huzuni kabisa. Baada ya kumaliza watu walianza kutawanyika, ila wakati Alwin anaondoka alishikwa bega na alipogeuka "Alwin unanikumbuka" aliuliza inspector Hans. "samahani mbona sijawahi kukuona" alijibu na kumfanya inspecta ashangae kidogo, "leo asubuhi nilikuja kwenu na tukaongea mambo fulani kuhusiana na kifo cha Jestina" alifafanua labda alihisi huenda akawa amesahau lakini bado Alwin alishikilia kuwa hamjui na kuomba aondoke zake. Inspecta alimruhusu huku akiwa na maswali mengi sana kichwani ambayo yalikosa majibu "ikiwa huyu yule sie Alwin sasa atakua nani" alijiuliza mwenyewe. Kwa mchana huo hali ilikuwa shwari kabisa, usiku ulianza kuingia na kila mtu akawa anamalizia biashara zake ili arudi nyumbani kwa ajili ya mapumziko. 


Sara ni miongoni mwa watu waliokuwa wakimalizia shughuli zao, "Sara kwa heri tutaonana kesho" Bety alimuaga huku akitoka katika chumba cha kubadilishia nguo na kuondoka. Ghafla hali ya hewa ilianza kubadilika humo ndani, Sara alihisi kama kuna mtu mwengine humo ndani. "Sara....sara" alisikia sauti ikimuita lakini mtu hakumuona, alifunga kabati lake ambalo lilikuwa na kioo mbele. Alipoangalia vizuri aliona kuna mtu amesimama nyuma yake lakini alipogeuka hakumuona, sasa wasiwasi ulianza kumuingia moyoni. Mara akaanza kusikia vicheko na vilio, woga ulimpata na kuanza kukimbia kuelekea mlango wa kutokea lakini ghafla taa zikazimika na kumfanya ajikwae na kuanguka chini kama mzigo. "sara....sara.....sara" alisikia tena sauti ikimwita, "we nani" aliuliza kwa sauti ya kilio. "mimi ni kifo chako" alijibiwa na kuzidi kutetemeka, Sara alinyanyuka kutoka chini na alipogeuka aelekee mlangoni ndipo akamuona mwanamke amesimama mbele ake. 
"wewe ni nani" aliuliza huku akiokota mbao pembeni, "leo hunijui si ndio" alijibiwa na kwa mbali sauti hio ikagonga kwenye ngoma za masikio yake. "lakini usijali nitakwambia" alijibiwa na ghafla akapotea na kutokea nyuma yake, "geuka" aliambiwa Sara na kuanza kugeuka taratibu na macho yake yakatuwa usoni mwa Jestina na hapo ndipo akamtambua lakini kabla hajafanya kitu alichezea kibao kizito na kuanguka chini "nisamehe Jestina" aliomba sara. "wewe hukunionea huruma na kuamua kuniziba mdomo si ndio" Jestina alijibu huku machozi ya damu yakimtoka. "sasa nataka nikuonyeshe maumivu niliyoyapata siku ile" aliendelea kuongea na ghafla Sara akawa hatoi sauti kwa sababu mdomo wake ulizibwa na kitu kama kipande cha nyama iliyooza. Kutokana na harufu kali ya kipande hicho Sara alianza kuhisi kutapika lakini matapishi hayakutoka kabisa, hali ilizidi kuwa mbaya huku yakianza kutokea puani na kumfanya akose pumzi. Jestina alikuwa mbele ya binti huyo ambae siku ile anabakwa yeye ndie alimziba mdomo ili asipige kelele. Haukupita muda Sara aliaga dunia kutokana kukosa pumzi muda mrefu, kama kawaida Jestina aliandika kwenye ukuta kwa damu "AMELIPA" kisha akatoweka eneo hilo. 
Siku ya pili wale waliofika kazini mapema walishudia mwili wa sara ukiwa upo katika hali mbaya sana na pia kulikuwa na harufu kali ya kinyesi. Taarifa zilitolewa polisi na haukupita muda walifika sehemu ya tukio na kufanya kazi yao ikiwemo kuwahoji marafiki wa karibu na binti huyo. Baada ya hapo walirudi kituoni kuendelea na majukumu mengine lakini inspector Hans bado alikuwa njia panda asijue la kufanya. Sasa hofu iliongezeka kwa wale wote waliohusika na kifo cha Jestina "unajua mtu wangu sisi tulikosea sana" Jay alimwambia James. "oyaa acha uoga wewe lazima kuna mtu atakuwa anatufanyia uhuni tu" James alijibu. "inawezekana ikawa Alwin au maana tokea atoke hospitali ya vichaa mauaji yameanza" Jay aliongea. "kama vipi tumuibukie asilete mambo ya kijinga" James aliongea kwa hasira na wakakubaliana hivo. Safari ya kuelekea kwa kina Alwin ilianza na kwa sababu walikuwa na usafiri walifika mapema. 
"Alwin yupo" Aliuliza Jay bila hata kutoa salamu, "nipo niwasaidie nini" Alwin alijibu mwenenyewe baada kuzitambua. Walimuomba atoke nje na yeye bila kupinga alitoka, "dogo sikia unajifanya mjanja si ndio" James alihoji kwa hasira. "kwani vipi mbona siwaelewi nyinyi" alijibu bila wasiwasi. "kama hutuelewi basi ngoja tutakuonesha" Jay alijibu na kumpa ishara James waondoke. 
"James" Alwin aliita, alipogeuka akamuonesha ishara kwa kupitisha mkono katika shingo akimaanisha ni zamu yake usiku wa siku hio. Lakini alipotezea na kuondoka zake bila hata kugeuka nyuma, Alwin alirudi ndani moja kwa moja alikwenda chumbani kwake. "vipi wameshaondoka" Aliuliza Alwin, "ndio" alijibu Jestina akirudi katika umbo lake la kike. Huo ni mchezo wamekubali kuucheza huku Jestina akiitumia nyumba hiyo kama ngome yake na mtu yeyote atakaekuja kwaajili ya kesi yake basi hujibadilisha na kuwa Alwin. Na hicho ndicho alichokifanya siku ile alivyokuja Inspector Hans kwaajili ya mahojiano. Bado vifo vyote viwili vilibakia kuwa ni gumzo, daktari alieifanyia uchunguzi miili hiyo alikuja na majibu yale yale tu "yoyote aliefanya mauaji haya si kiumbe wa kawaida". 
************************************ 
"Matt mwanangu kwanini uliamua kufanya ushenzi ule" 
"Ah ni ushundani tu ndo ulionipelekea kufanya vile" 
"sasa umeona madhara yake nimetumia mabilioni ya mapesa kuwahonga majaji na wanasheria waifute kesi ile" 
"najua mzee, ila usijali kila kitu kipo sawa na muda si mrefu nitarudi nyumbani" 
Hayo yalikuwa ni mazungumzo ya Matt na baba yake kwa njia ya simu, baada kufanya tukio lile ilibidi Matt asafirishwe na kesi ile iuliwe kwa aina yoyote. Sasa anataka kurudi akiamini miaka aliokaa nje ya mji wake ingetosha watu kumsahau na hata wenzake walikata mawasiliano nae kwa sababu aliondoka kimya kimya bila kuwataarifu wenzake chochote. Ni baada tukio lile alilomfanyia Jestina, Matt alisafirishwa na baba yake na kupelekwa Ufaransa. 
"Baba naskia Alwin kapona" aliuliza Miryam, "ndio mwanangu kapona kabisa" Profesa Alexander Harison alijibu." Ah basi mimi namaliza mtihani wangu wiki ijayo baada ya hapo nitakuja, lakini usimwambie kitu Alwin" aliongea Miryam kwa furaha sana. Miryam hakuweza kuendelea kusoma Mashvile baada lile tukio na lilisababisha kifo cha Jestina pamoja na kichaa cha Alwin. Na baada baba yake kugundua hilo aliamua kumsafirisha kwa ajili ya kwenda kumalizia masomo yake nchini China na huo ndio ulikuwa mwaka wake wa mwisho wa masomo. Lakini haikupita hata siku moja bila kumuombea uzima Alwin.




No comments: