Tuwapende Mama zetu na Wake zetu Wanapitia Magumu Sana Kipindi cha uja Uzito.


Nilikuwa nikisikia wanawake wakisema nimepata shida miez tisa kumbeba mwanangu tumboni nilikuwa sielewi vizuri taabu na shida hizo ni zipi mpk wajisifie kila dakika kila saa na kila siku. Sasa nahizi taabu na shida wanazozipata. 

Maana mke wangu ndo kwanza mja mzito miez tisa kasoro siku chache sasa naona shida na taabu anazopata. Kulala shida kusimama kwake shida kukaa shida hakuna jema hata moja. Akilala kila anavyojaribu mara aweke mgongo chini anateseka, alale kiupande upande shida mpk namhurumia. 


Najaribu kuwaza ndivyo nilivyomtesa mamayangu hivyo nikiwa Tumboni??? Kama ndivyo kweli mama anatakiwa aheshimiwa na kupongezwa kwa uvumilivu wanaopitia mpk kutuleta duniani. 

Lakini kinachonifanya niwaze zaid je baada ya kuzaliwa mimi mtoto wa kwanza kama nilimtesa mama hivi ikawaje akaniletea mdogo wangu, hakukumbuka shida na taabu nilizomletea?? Daaaaah wanawake mnastahili pongezi kubwa kwa ujasiri na uvumilivu mnaopitia kipindi cha ujauzito. Japo nasikia mkienda mbele zaid kutununua kwa wauguzi na wakunga pia mnateseka zaidi 

HESHIMU NYINGI ZIWAFIKIE WANAWAKE NITAWAHESHIMU SIKU ZOTE ZA MAISHA YANGU




No comments: