CHOMBEZO: MPANGAJI EPISODE: 01
Nakumbuka siku hiyo nilishikwa na hamu ya kufanya ule upuuzi kiasi kwamba nilishindwa hata kwenda darasani. Kitendo kile kilifanya yule msimamizi wa wanafunzi pale shuleni kuniona kama naumwa,hivyo aliniongoza hadi hospitali moja ya pale Tabora na nilipofika, ndipo nikajidai naumwa zaidi. Nilijiregeza kiasi kwamba nilishindwa hata kutembea,hivyo nikaletewa kile kiti cha wagonjwa wasiyojiweza ili kinisaidie kuingia hospitali. Baada ya kuniingiza mle, yule mwalimu akabaki nje kwa ajili ya kusubiri majibu yatakayotoka kwa yule aliyenipokea.
Ile kufunga ule mlango niliyoingilia, nilinyanyuka haraka na kuanza kuongea na yule muuguzi aliyenipokea huku nikimshawishi kwa uongo mwingi ili asinidunge sindano zao,hasa diripu. “Kaka, unataka hela hutaki?”. Nilinyanyuka na kumtupia swali yule jamaa aliyekuwa anahangaika kunisukuma na kile kiti cha wagonjwa. Kitendo cha mimi kunyanyuka vile ghafla,kilimfanya kidogo ashtuke na kuhisi kuwa nimechanganyikiwa. “Wewe si unaumwa wewe? Au ndiyo Malaria inakupanda kichwani?.Aliuliza yule kaka. “Tulia kaka, skonga kuna ukame sana. Hapa bila kuzuga naumwa basi kule skonga ningebaka wenzangu. We sema, unataka hela au hutaki”.Nilijitetea kidogo na kurudi kwenye mada yangu. “We unataka ufanye nini? We mwenyewe kwanza ni mwanafunzi,halafu unaniulizia mfanyakazi kama nataka hela. Inakuwaje hiyo?”.Jamaa alikuwa mbishi kuelewa,ila nikamsawazisha. “Sikiliza Bro, mimi hapa siumwi. Cha msingi, wewe nibandike bandike hayo madiripu halafu muite huyo ticha aje kuniona. Usimruhusu aende kwa daktari,kwani ukifanya hivyo utakosa hela”.Nilimwambia hayo huku nikimwangalia usoni nikisubiri jibu lake. “Ehee, nakusikiliza dogo. Au ndo umemaliza?”.Yule muuguzi akauliza tena. “Kwani Bro hujanielewa wapi? Mbona unakuwa na fuvu gumu?”.Nilimuuliza kwa jazba kidogo huku nasukuma kichwa chake kwa kidole cha shahada. “Dogo sikiliza, hapa tunasaidiana. Mimi nikikuwekea hayo madiripu,nitapataje hiyo hela?”. Jamaa aliniuliza swali hilo. “Kumbe tatizo ni hilo. Akija we zuga kuwa unanihurumia sana,halafu mwambie bei ya haya madiripu pamoja na hela ya msosi wangu nitakao kula nikiwa hapa. Usimruhusu aende kwa daktari mkuu, maliza hapa hapa. Mwambie wewe utapeleka taarifa zote ofisini”.Nilimaliza na yule muuguzi kwa tabasamu,akachukua maplasta na kuanza kubandika ile mirija mikononi mwangu bila ya zile sindano, wakati huo ilikuwa ni mida ya saa saba mchana. “Sasa dogo, aking’ang’ania kwenda kufanya malipo ofisini je?”.Yule jamaa muuguzi aliniuliza baada ya kumaliza kunitundikia zile diripu uchwara. “Lile ticha siyo janja, halijui lolote. Yaani pale skuli kazi yake kusimamia makazi tunayolala na siyo kufundisha. Halafu mimi nina kadi hii ya bima ya afya, hivyo wewe usiwe na wasi. Mimi matibabu yangu ni bure”. “Ha ha haa, hapo sawa nimekuelewa. Sasa ngoja niende kwa ticha lako”.Jamaa akawa anaondoka kwenda kumuita mwalimu yule niliyekuja naye. Baada kama ya nusu dakika,waliingia huku mimi nikiwa kama sijielewi pale kitandani. “Ticha, aisee dogo anaumwa sana”.Nilimsikia jamaa akianza kuongea na ticha wangu. “Kwa hiyo ni nini kinamsumbua?”.Akauliza ticha. “Nimecheki mapigo yake ya moyo ndiyo yanaenda kasi sana,hivyo yaonekana ni BP. Ila usiwe na shaka sana. Wewe niachie elfu hamsini za matibabu pamoja na tupesa kidogo kwa ajili ya chakula cha mgonjwa akihamka. Siwezi kuendelea na matibabu bila kupata msaada wa kifedha ili tununue dawa zake na vitu vingine muhimu kama hizo diripu ambazo anatakiwa atundikiwe tatu”.Jamaa muuguzi alijielezea nia yake,na bila kipingamizi,yule ticha aliingiza mikono yake kwenye mfuko wa suruali na kuibuka na waleti iliyonona kiasi chake. Wakati huo mimi nilikuwa namuangalia kwa jicho moja la kuiba, na nilishuhudia akitoa noti saba za elfu kumi na kumkabidhi yule jamaa. “Sasa dokta, fanya harakati huyu mtoto apone. Mimi nitakuja kesho ili nijue ni nini kinaendelea, sawa dokta?Akiamka mpe salaam zangu”.Ticha alimalizana na yule jamaa muuguzi na kuanza kuondoka huku akisindikizwa na yule muuguzi ambaye kwa kumuangalia alikuwa ana ukame sana kifedha,hivyo zile hela kwake ilikuwa kama bahari kutokea jangwani. “Dogo tumewin. Kweli ili ni bonge la boya. Sasa sikiliza, kanipa elfu sabini, wewe chukua hii thelathini halafu pitia huo mlango kafanye yako. Huu wa kuingilia mimi naufunga, we ukirudi pitia mlango huo huo halafu njoo ile ofisi yangu kunipa taarifa,mwisho iwe saa kumi na mbili, sawa?”.Yule jamaa muuguzi alinipa maelekezo ya nini cha kufanya baada ya kuhakikisha yule ticha katokomea kabisa pale hospitali. Nilimjibu kwa kuitikia poa huku nazitoa zile diripu na kuanza kutoka nje.
Niligundua kuwa yule jamaa alikuwa ni muuguzi wa zamu ambaye ana cheo kidogo,na katika hospitali ile,wanafunzi walikuwa wana sehemu zao maalum kwa ajili ya kulazwa na siku hiyo kulikuwa hakuna mwanfunzi aliyeletwa zaidi yangu. Niliingia viwanjani na kuanza kutafuta mwanamke wa kutuliza maumivu yangu huku nikiwa na hamasa kubwa ya ujana wangu ambao sikufahamu kuwa ni maji ya moto.
Kiukweli soko lilikuwa limedoda siku ile, hadi saa kumi na moja na nusu, nilikuwa sijapata goma la kunisuuza maumivu yangu, hivyo niliamua kurudi zangu hospitali na breki ya kwanza ilikuwa ni kuingia kwenye ile wodi na kubandika yale madiripu na kisha kuanza kupiga kelele kana kwamba nilikuwa nimetoka usingizini. Haikuchukua hata dakika, yule jamaa alikuja huku katabasamu na kuniuliza. “Vipi dogo, umefanikiwa?”. “Aaah, huko majanga tu! wamehadimika kama bia ya bingwa”. “Kwa hiyo, vipi sasa?”. “Leo usiku nitatoroka, nitajifanya napunga upepo halafu naondoka. Nitarudi baadaye”. “Hapana dogo,hiyo ya usiku sikuruhusu. Ukipigwa je? We tulia, kesho tutapanga tena”. “Poa kaka, ila naumia mwenzako”. “Tulia dogo, vumilia hadi kesho. Sasa hivi naondoka, namuachia maagizo muuguzi mwingine. Toa hayo madiripu halafu jifanye umepata nafuu kidogo”.Jamaa aliongea hayo na kutoka nje ambapo aliniacha mimi nabandua yale maplasta na kisha kukaa kitako. Baada ya dakika tano,yule jamaa muuguzi aliingia na muuguzi mwingine ambaye nilipomtazama moyo wangu ukawa kama umekufa ganzi. Nikashindwa kuyatoa macho yangu usoni pake na kunifanya nizidi kushikwa namshawasha mwingine wa hali ya juu.
“Habari yako mgonjwa”.Ilikuwa ni sauti tamu na nyororo ikipita masikioni mwangu na kusababisha akili na ubongo wangu kuhama kwa muda na kujenga fikra za kishetani katika mwili wangu. “Dogo unasalimiwa, mbona umekaza macho? Malaria ndiyo inazidisha kasi nini?”. Aliuliza yule jamaa muuguzi kitu ambacho kilinifanya nitoke katika yale mawazo yangu potofu. “Hamna Dokta, sema akili yangu inawaza itakuwaje hadi kesho ikiwa hivi hivi. Poa dada, mambo vipi?”.Nilimjibu yule jamaa muuguzi na kumsalimia yule muuguzi aliyeingia naye. Muuguzi yule alikuwa ni mdogo kimwili na mwenye rangi ya kuvutia sana. Alivalia gauni lake la kiuguzi ambalo kifuani lilimshika vizuri na kusababisha kile kifua chake chenye marimao mawili yaliyokomaa kubetuka kidogo na kusababisha hamsha nyingine katika mwili wangu. “Poa tu! Hali yako inaendaje?”.Aliuliza tena yule dada. “Mimi poa na ninamshukuru Dokta kwa kazi nzuri hadi hivi sasa naongea na wewe”.Niliongea maneno ambayo ni msomi pekee angejua nina maana gani. Hiyo shukrani kwa dokta haikuwa kwa ajili ya kunitibu, ila utaijua baadaye napoendelea kukusimulia.
:::NINI KILIJIRI KATI YAKE NA DOKTA?
USIKOSE EPISODE 02.
No comments: