CHOMBEZO: MPANGAJI EPISODE: 12
Ilipoishia jana…
mnamo mida ya saa tano likawa linapiga honi kuashiria kuwa linaanza kuiacha ardhi nzuri iliyopo pale Ubungo. Naam,sasa safari yangu ya Arusha,ikawa imeshika hatamu.
Songa nayo sasa..
Mida ya saa mbili za usiku,mimi na abiria wenzangu,tukawa tumekanyaga ardhi ya jiji la Arusha ambapo kwangu mimi,ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kufika.
Nilitabasamu kwa furaha pale nilipochungulia dirishani na kumuona kaka yangu akiwa anatazama kila abiria anayeshuka katika basi lile. Hapo hapo na mimi nikaanza kuzihesabu hatua taratibu na kuelekea zilipo ngazi za basi lile. Nikazikanyaga kwa uangalifu huku nashuka chini,na kitendo cha furaha kikatokea kwangu.Kitendo hicho kilikuwa furaha sana wakati kinatokea muda ule,ila kama ningelijua,wala nisingelisema na kufurahia kuwa kile ni kitendo cha furaha.
Kitendo chenyewe kilikuwa ni kuikanyaga ardhi ya Arusha. Jiji ambalo linasifika kwa kuwa na vitendo vingi vya kihalifu kulikoni miji yote ya nchi hii pendwa ya Tanzania. Jiji lile pia,lilisifika kwa kuwa na bei za juu katika vyakula kuliko kitu chochote.
Jiji lenye mahoteli na kumbi kubwa na za kuvutia. Na ni jiji lenye madini hadimu ya Tanzanite pamoja na vivutio vya kitalii. Welcome to Arusha,ndivyo kibao cha kile kituo cha mabasi kilivyosomeka.
Kaka aliponiona,alitabasamu na mara moja alikuja pale nilipokuwa nimesimama kabla sijaanza hatua zangu kumuelekea. Alipofika alinikumbatia kwa furaha na kunisalimia kwa amani tele. Na mimi nikarudisha fadhira hizo sawa na alivyofanya yeye. Akachukua begi langu la nguo,kisha akaanza safari ya kutoka katika eneo lile la kituo cha mabasi yatokayo mikoani.
Kaka yangu huyu,yeye alikuwa ni mchuhuzi wa madini mbalimbali yanayopatikana Arusha. Kwa kazi hiyo,ilimfanya awe bize sana katika kutafuta madini na wateja wa kununua madini anayoyapata kutoka kwa wachimbaji wa pale Arusha.
Hivyo ilikuwa ni nadra sana kukaa nyumbani hata kwa siku mbili. Kwa kifupi alikuwa yupo bize kila muda. Kwa ujio wangu,ilikuwa ni ahueni kwake,kwani sasa angekuwa ana uhuru wa kufanya kazi zake hata kwa miezi kadhaa bila kuonekana pale nyumbani.
“Dogo karibu sana skani. Hapa ndipo kwangu”.Kaka alinikaribisha kwake baada ya safari iliyochukua kama dakika thelathini kutoka pale kituo cha mabasi.
“Bonge la hause mzee,upo peke yako au na watu?”.Nilimuuliza baada ya kushuhudia ule ukubwa wa nyumba kwa kule nje.
“Aaah,nipo na baba mwenye nyumba. Yeye anakaa kule na familia yake”.Kaka akanijibu.
“Na nyie ma-bro kwa kupanga tu!Kha! Si mjenge sasa?”.Niliongea huku nikionesha nakerekwa na wao kupanga panga.
“Mi nyumba yangu ipo Fire pale,nimeinunua,sema bado naikarabati. Nadhani baada ya miezi mitatu,itakuwa tayari kwa mimi kuingia”.Kaka alinijibu na kunifanya niridhike kwa hatua yake aliyofikia kwenye kujitafutia makazi yake binafsi.
Kaka alikuwa kajipanga kweli kweli ndani kwake. Alikuwa anakila kitu ambacho kijana wa kileo alitamani kuwa nacho. Kwa kifupi alimzidi yule kaka yangu wa Dar hasa kwa thamani za ndani.
Alinionesha lilipo bafu,na mimi nikanyanyuka na kwenda bafuni humo na kuoga.Kisha nikajipiga mambo katika mavazi na manukato,na baadae nikaelekea sebuleni ambapo nilikuta chakula kimeandaliwa.
“Dogo piga msosi huo,mimi tayari”.Kaka alinikaribisha,nami nikavuta kiti kwa nyuma na kuanza kujipakulia chakula kile.
“Sasa Bro,huu msosi nani kakupikia?Mbona sioni mtu hapa wa kupika menyu ya ukweli kama hii”.Nilidadisi kaka kwa swali.
“Huyo shemeji yako,sema huwa ashindi hapa. Nilimwambia leo unakuja ndo maana akaja kunisaidia kupika”.Kaka naye hakuwa na kificho,aliniji na mimi nikakosa swali wala kauli ya kuendelea kudadisi.
Baada ya kumaliza chakula na kujiona kuwa nimeridhjka,nilimuaga kwa kumwambia kuwa naenda kulala. Naye kaka akaniruhusu,basi maisha ndiyo yakawa yameanza hivyo pale Arusha.
********
Kesho yake asubuhi na mapema,kaka aliniamsha kwa kuniambia kuwa anaenda kazini hivyo aliona ni vyema kwenda kunitambulisha kwa baba mwenye nyumba yake na familia yake kwa ujumla.
Nikanawa uso wangu haraka,na kisha nilimfuata kaka mgongoni hadi kwenye mlango ambao kaka aliugonga na baadae ukafunguliwa na mzee mmoja ambaye hakuwa mzee kiasi kwamba alihitaji fimbo,bali uzee wake,ni kwa sababu alikuwa kaenda umri mkubwa kushinda sisi.
“Shikamoo mzee”.Kaka aliamwamkia mzee yule na mimi nikafanya vivyo hivyo. Mzee akaitikia na kutega sikio kaitiwa nini asubuhi ile.
“Mzee huyu ni mdogo wangu,kaja jana. Naomba umtambue,anaitwa Prince. Leo atakuwa hapa na nyie”.Kaka alinitambulisha kwa mzee yule kwa haraka,kisha akasubiri majibu kutoka kwenye mdomo wa mzee yule.
“Ahaa.Prince. Karibu bwana. Mimi naitwa Mchungaji Donyo,na nina familia nyingine utaiona baadae,sasa hivi,rudi kapumzike kwanza maana safari ina uchovu wake”.Mzee yule alijitambulisha na kutupa ruhusa ya sisi kwenda kupumzika huku kaka yeye akiwa kama kapewa mbawa za kwenda kazini kwake.
Mida ya saa sita,kijana mie mpole na mtulivu lakini muuaji wa chinichini,nilikuwa naswaki katika bafu la nyumba yetu lililo mle mle ndani.
Baada ya kumaliza kuswaki,nilifungua jokofu na kukutana na maziwa fresh yakiwa kwenye box. Nikagida kwa ajili ya kuifanya afya yangu izidi kuwa imara,wakati huo nilikuwa sina tena wazo na wakina Tuse ambao niliwaacha na maisha yao ,na mimi nikaendelea na yangu. Nilichokumbuka ni kuwatumia meseji tu! Kwa kuwaambia kuwa nimefika salama Arusha.
Kaka yangu kama kawaida nilim-bipu,na alipopiga nikampa hali halisi ya safari yangu na sikuacha kumshukuru kwa ukarimu alionionesha wakati nipo kwake.Hayo ndiyo niliyoyafanya kabla sijatoka nje kuangalia mazingira.
Nilipotoka nje sasa. Aisee Arusha kuna baridi nyie,dah! Yaani nilijikuta natoka mara moja na kuingia ndani haraka. Nilivyofanya vile,nilisikia vicheko vya kike nyuma yangu. Niliguna na kujiuliza ni wakina nani hao walionicheka?
Kwa kuwa P nilikuwa si mtu wa kuogopa sana watoto wa kike,nikarudi ndani na kuchukua sweta la kaka,nikaliweka mwilini. Miguuni nikaweka soksi ndefu kabisa na sendro juu yake,na mikononi nikamaliza na grovu zile za sufi ambazo kaka alikuwa nazo za kutosha ndani kwake.
Baridi ya Arusha ilikuwa kama mateso kwangu kwani kule Dar es Salaam,kulikuwa hakuna hali ya vile hata mara moja. Kwa kifupi Dar,baridi yake ilikuwa inakuja na joto fulani hivi.Hali ile inaitwa jotoridi ,kwa wale wanajografia,kama nimekosea samahanini.
Na hali ile huja kwa sababu ya uwepo wa bahari ambayo kuna kipindi inavukishwa(Hali ya kutengeneza mvuke),na ule mvuke unaenda angani na kutengeneza wingu ambalo linasababisha mvua,au kama sijakosea,mvuke ule unaenda angani na kulainisha hali ya hewa ya kule na kuifanya iwe ya mvua. Hapo tunapata mvua.
Sasa ule mvuke wa bahari,ndiyo haswaa unaleta joto katika jiji la Dar es Salaam,na ndiyo maana mikoa ambayo ipo mbali na bahari,huwa na baridi la hatari. Kama Mbeya,Rukwa na Iringa,huko achana napo aisee.
Hayo ya wasomi,na mimi nilikuwa nataka niwaoneshe kuwa sipo nyuma katika elimu yangu japo sijafika mbali. Turudi kwenye mada.
Basi nilipovaa yale mavazi,nilitoka nje na kuanza kuangaza ni wapi vicheko vile vilitokea,sikuchukua hata dakika mbili,niliona kuna chumba ambacho moja kwa moja akili yangu ilisema kule ni jikoni. Nikanyoosha mwanaume hadi kwenye kile chumba,nikaita hodi nayo hodi yangu ikaitikiwa na sauti moja hivi ambayo ilinifanya nitabasamu kwa faraja kimoyo-moyo.
“Kumbe kuna demu hapa?”Nilijiwazia moyoni baada ya sauti ile ambayo wala sikuifikiria mara mbili kuwa labda itakuwa ya mwanamama. Kwa utaalamu wangu,nilikadiria ile sauti ni ya binti wa miaka kumi na saba hadi tisa.
Kamanda baada ya kuitikiwa hodi yangu nikasukuma mlango kwa utaratibu na kuingia kwenye kile chumba,na kama mawazo yangu yalivyoniambia,kule kulikuwa ni jikoni,sema miaka nilikosea kukadiria,ila iligusa kiasi fulani.
Eee bwana nilikutana na wasichana watatu. Mmoja alikuwa mdogo mdogo,kwa kumkadiria alikuwa anamiaka kama kumi au kumi na moja,mwingine alikuwa ndiyo anaanza kuja kuja ukubwani,alikuwa na miaka kumi na tano au kumi na sita. Halafu kulikuwa na mkubwa wao sasa,tena nahisi yule ndiye alijibu hodi yangu,huyu kwa kumuangalia alikuwa na miaka ishirini hadi ishirini na mbili.
Ngoja sasa nikwambie kitu kilichonifanya nishindwe kwenda mbele wala kurudi nyuma baada ya kuingia mle ndani.Hapa nitakwambia sifa za yule mkubwa na huyu wa kati,yule mwingine achana naye,alikuwa bado mtoto sana. Haniwezi.
*****Episode ya 12 inaendelea....*****
No comments: