CHOMBEZO: MPANGAJI EPISODE: 16



ILIPOISHIA...

Baada ya kuanika akanifata pale nilipo na kisha akaanza kuongea maneno ambayo,dah! Sikudhani mtoto kama yule angeweza kuyanena.

“Nasikia unamla dada”.Alianza.

“Mh!We Shei unawehuka?”.Ilibidi niulize.

“We sema tu! Unamla dada?’.Alikazia.

Songa nayo..

“Embu kaendelee kufua”.Nilimkatisha maswali yake.

“Basi sasa,mimi nilikuwa nataka kukusaidia jambo lakini yaonekana huna mpango”.Aliongea huku ananiacha pale peke yangu.

“We Shei embu rudi rafiki yangu”.Nilimwita.Naye bila hiyana akarudi.

“Niambie kuna nini?”.Nilimuuliza.

“Sema kwanza. Unamgonga au humgongi”.Kicheko kilinibana hasa nikiangalia anayeniambia hayo.

“Poa. Nimefanya naye. Kuna nini kwani?”.Nilimjibu na kumtupia swali.

“Ulitumia ndomu?”.Swali lingine lilikuja kwangu.

“Sasa wadhani mimi namuamini msichana kama yule hadi nisitumie kinga?Kinga sitatumia kwa mtu nayejua hana tabia za ajabu”.Nilimjibu.

“Ahaaa. Hapo basi,hilo muhimu sana. Yule ni dada yangu lakini kuwa makini naye,unaweza kuzikwa. Hapo kaenda viwanja,akirudi yupo bwii”.Aliongea Sheila na kuondoka eneo lile kwa ajili ya kwenda kumalizia kufua.

Maneno yake yalikuwa kama yameamsha jambo na kutaka kulijua zaidi. Nikasema lazima nijitahidi ili nihakikishe maneno yale kutoka kwa Sheila.

Basi siku hiyo nilikaa nje kwa muda mrefu kuliko siku zote ili tu! Nimuone huyo Farida na muda anaorudi na kuhakikisha maneno ya Sheila.

Ndipo mida ya saa nne na nusu za usiku,nilisikia mtu kama ananyata kuingia eneo lile la nyumbani. Na mimi niliposikia hivyo,nilijificha kwa pembeni kidogo ili nisionekane pale atakapotokeza.

Mara nilimuona Farida akiwa kavalia kimini kimoja matata sana na brazia moja ya ajabu mno.

Kile kimini kiliishia juu ya mapaja,hali ambayo kama akiinama basi nguo yake ya ndani ingeonekana,wakati huo ile brazia ilikuwa ni kama chandarua,yaani ilikuwa inamatobo matobo halafu ndani hakuvaa kitu chochote. Hali hiyo ilifanya chuchu zake zitoke nje kupitia yale matobo ya brazia aliyovaa.

Aliangalia huko na huko kisha alitoa kimkoba chake na kunyofoa khanga mbili. Moja aliivaa chini na nyingine aliitanda kwa juu. Na baada ya kufanikiwa hilo,alienda hadi lilipo-dirisha lao na kuanza kumuita Sheila kwa sauti ya chini,na baada ya Sheila kuitika,aliulizwa kama baba yake yupo. Akajibiwa hayupo,na ndipo ahueni ya Farida iliposikika kwa kushusha pumzi moja ndefu.

Mimi kama kawaida yangu,huwa sipendi sana kumficha mtu. Baada ya Farida kutoka pale dirishani,alienda hadi ulipo-mlango wao wa sebuleni. Na mimi niliona huo ni muda muafaka wa kujifichua mahala nilipokuwepo.

Kwa mbwembwe nyingi nilianza kwa kupiga mruzi wangu uleule ambao haulewekagi ni wimbo gani unaimbwa katika ara ile ya mruzi.

Nilimuona kama kashtuka lakini alijitahidi kuficha hisia zile na kunifata hadi pale nilipokuwa nazuga napiga mruzi.

“Kwani P ulikuwa hapa muda mrefu eeh”.Aliniuliza swali ambalo wakati linakuja lilikuja na harufu ya pombe.

“Unakunywa na pombe mwenzetu?”.Nilimuuliza swali badala ya kujibu swali.

“Aaagh. Imetokea tu leo,nikajikuta nimekunywa”.Alinijibu huku akiangalia pembeni kama mtu atafutaye kitu pale nje.

“Mmmh,kwa hiyo na hayo mavazi ya ndani nayo utasema umetokea tu! Kuyavaa,si ndio mama?”.Nilimuuliza swali lingine.

“Daah! Yaonekana ulinisubiri kitambo,kama mzazi wangu vile”.Alinijibu Farida kwa maneno ambayo yalikuwa yana nia ya kuanzisha vurugu.

Sikuwa na wasiwasi na shombo zake bali nilimchukulia kama mtu asiyejielewa afanyalo. Nilimuangalia usoni kwa macho yaliyojaa hasira zilizochanganyika na huruma juu ya maisha yake, na yeye aliniangalia kwa macho yake ambayo yalikuwa makavu na tayari kwa ajili ya vurumai. Wakati huo Sheila alishafungua mlango na kubaki mlangoni akitutazama tunachofanya.

“Hongera kwa maneno yako matamu. Lakini nimeona kila kitu. Umependeza sana kwa yale mavazi,ila nashangaa kwa nini uliamua kuvaa mikhanga”.Niliongea huku bado macho yangu yakiwa usoni pake.

“Hayo hayakuhusu babu wee. Jali biashara zako na si kukaa kwa kaka yako na kusubiri kumuona Farida kavaaje au anafanya nini. Baridi limekupiga kutwa nzima,kisa unamsubiri mwana wa Donya. Utakufa na Athima mtoto wa kiume,unaelelewa na ndugu zako. Tafuta vyako bwege wewe,msyuuu”.Aliongea Farida kwa nyodo na kunifanya nichanue tabasamu la kejeli kutokana na maneno yake yaliyomalizika kwa msonyo mrefu kutoka kinywani kwake.

“Ohooo. Kumbe na wewe una kidomodomo eeh. Pole sana binti,kama ulidhani mimi nitakuja juu,umebugi sana. Na jambo usilolijua,litakusumbua sana. Na mwisho wa siku utabaki unasonya misonyo tu!. Endelea na kazi yako ya umalaya,si ndio inakufanya ulete dharau na kuniona mimi bwege?Kwa kuwa wewe unatafuta kwa kutumia mwili wako na mimi nakaa kwa kaka yangu bila kazi,si ndio eeh”.Niliongea huku nampa mgongo kwa ajili ya kuingia ndani kwangu.

“Wewe unadhani Mwana FA aliimba bure? Ingekuwa vipi kama kungekuwa hakuna malaya,si ubakaji ungeongezeka kwa kasi ya ajabu. Acha niwe malaya ili niwalinde wadogo zangu wasibakwe kwa kuwamaliza hamu wanaume wenye tabia hizo. Usidhani malaya kaumbwa ili awe malaya,saa nyingine ni maisha tu!”.Maneno hayo yalinikumbusha maneno ya Mama Tuse na Tuse mwenyewe.

Niligeuka nikamwangalia sana Farida,kisha nilitikisa kichwa kwa masikitiko na kurudi tena pale niliposimama mwanzo.

“Hivi wewe Farida,hapa kwa baba yako umekosa nini wewe?Utake nini usipewe? Utake uende wapi ukataliwe? Na wewe unadiriki kusema eti hukupenda kuwa malaya?Unafanya kwa sababu ya jambo?

Jambo gani ambalo unalifanya linaleta faida kwa baba yako? Hao uanaosema unawalinda wasibakwe,wewe uliwahi kubakwa hapo mwanzo?Wewe ulilindwa na nani ili usibakwe?Embu acha chenga,tena bahati yako,ungekuwa anga zangu ningekuchapa viboko kwa kuwashushia heshma wazazi wako waliokulea kwa kila hali huku wakihakikisha unapata kila kitu muhimu.

Nimekutana na malaya mimi,malaya ambao kama wangekuwa ni wewe,sidhani kama wangefanya yale. Wanamalengo kuliko hata ya mtu ambaye si malaya. Eti na wewe unasema hukupenda,tamaa za mwili na vitu vikubwa,zitakuponza wewe”.Niliongea kwa hasira sana maneno hayo,na yeye alitambua kuwa nimepata moto hivyo alikaa kimya bila kusema chochote hadi pale nilipoingia ndani kwangu na kusikia mlango wao ukifungwa.

****************

Kesho yake Farida hakutoka nje kwa sababu ya aibu. Na mimi nilishukuru sana kwani maneno yangu yawezekana yalimuingia ipasavyo.

Siku ikapita bila kumwona na hatimaye wiki ikakata pia bila kumwona bali kumsikia akimuita mdogo wake,ila nahisi alikuwa anatoka,sema akiniona anakimbia au kujificha.

“Atajua mwenyewe.Meseji sent”. Ni maneno niliyojisemea siku moja baada ya kuona kimya chake kikiwa kikubwa.

******************

Kwa upande wangu, muda wa kukaa pale nyumbani kwa kaka,ulibaki kama wiki mbili na nilikuwa tayari kwa kuondoka baada ya wiki hizo.

Nilianza kuwaaga pale nyumbani hasa wale niliyokuwa nawaona. Tulikuwa tumezoeana sana,hasa utani wangu ndiyo kama chachu kwao ya kuwa wanyonge baada ya kusikia naondoka.

Wakati nimebakiza wiki moja niondoke pale nyumbani,likatokeza tatizo kubwa jingine. Hili ni tatizo kubwa kuliko matatizo yote niliyowahi kuyapata maishani mwangu. Tatizo hili naweza sema ndilo haswaa,lililonifanya nione Arusha chungu na mbaya sana kuliko mikoa yote niliyowahi kutembea.

::Usikose Episode ya 17........



No comments: