Kuwa Na Mahusiano Ya Kimapenzi Na Wanawake Wengi Hakukufanyi Kuwa Kidume



Ni jambo la kawaida kukuta wanaume wakipiga stori na kujisifia kutokana na idadi ya wanawake walionao. Baadhi ya wanaume hudhani kua kuwa na wanawake wengi, kutembea na kuhudumia wanawake wengi ndiyo kunakufanya kuwa kidume kamili, kunakufanya kuwa rijali na kunakufanya kuheshimika mbele ya wanaume wenzako na mbele ya wanawake. Hiyo si kweli na mara nyingi kuwa na wanawake wengi inaweza nikuwa unajidhalilisha tu.

Mwanaume kidume ni yule ambaye anakuwa na mwanamke mmoja lakini anamfanyia mambo mpaka wanawake wengine mia moja wanamtamani, wanatamani kuwa na yeye na hata kufikia kujitongozesha kwake. Hapa nifafanue kidogo, unaweza kuwa na wanawake mia, lakini kama wote huwaridhishi, kwanza kitandani na pili katika kuwatimizia mahitaji yao basi utaambulia kutukanwa na kuonekana fala tu mtaani.
Lakini kama una mwanamke mmoja ambaye unamhudumia vizuri, hakosi chochote kutoka kwako, unamuonyesha mahaba tena yale ya kwenye TV. Lakini huishii hapo, kitandani unamfanya kuongea lugha 100 kiasi kwamba hatamani mwanaume mwingine, kiasi kwamba anashindwa hata kunyamaza kila siku kukusifia kwa marafiki zake, basi sio tu kwamba hao marafiki zake nao watakutamani bali pia watakuheshimu kwakuwa wanajua wewe ni kidime kweli. Hivyo acha kujisifia una wanawake mia wakati hata huyo mmoja huwezi kumridhisha!




No comments: